Nyumba za Prefab Tanzania

Kwa sisi tunaojenga nyumba kwa kudunduliza na kisha kuhamia kabla haijakwisha vizuri, prefab itakuwa haifai kwani bei zake ni za juu.
 
Kuna kampuni Tanzania wanafabricate hizo Prefab buildings
Alaf Aluminium na Humanne Homes
 
Duh,wakuu hizo bei wengine na vinyumba vyetu vya 25m,tunapita tu na kujifariji kwa macho.
Bonge la Mjengo
Ile nime print picha yake nimebandika ukutani ili niwe naonaona kama nimo ndaniyake.
Lazima ujirafiji mwenyewe,alllaaa
 
hizo nyumba za prefab ni gharama mkuu kwa mtanzania wa hali ya kipato cha chini hawezi mudu labda wenzetu ila mm nimezipenda ingawaje mfuko hauruhusu bora nijenge kanyumba kakawaida tu ila nikapambe kaonekane kapo kwenye fashion ya kisasa kulikokujipeleka huko mwisho wa siku inakuwa majanga bure
Kwa wale walio hudhuria Maonyesho ya Kilimo 88 pale Dodoma, kuna kampuni moja ya prefab houses imeishaingia nchini, ofisi zake ziko pale Milenium Bussiness Park. Wamejenga nyumba za mfano pale Nzuguni.

Kwa dar es Salaam, pale eneo la Makumbusho kuna duka la Prefab houses na sample zake pale nje ya ofisi hizo.

Tatizo: Nlipofuatilia cost ya kujenga hizi prefab za Milenium Business Park, cost ya kujenga a small house ya 3 bedroom, one master, jiko, sitting na dinning, ilifika M.78. Kwa M.30, unajenga nyumba nzuri tuu matofali ya playform ukujenga mwenyewe, ukiwacontract NHMBRA (Mwenge) itakicost m.40 tuu.
 
Back
Top Bottom