Nyumba za Mchechu ni Bomu linalo subiriwa kulipuka (Mtazamo wangu)

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,568
4,233
Hizi nyumba za Mchechu za rank mbalimbali naona ni Bomu linalosubiri kulipuka kwani ukiangalia maeneo (nyingi) zinakojengwa na gharama zake kuwa ghali sana hapo hujaweka riba ya mamilioni ya kurudisha kwenye ma bank.

Ninavyo ona; Kuna miradi ambayo imeelekezwa maeneo yasiyovutia au pengine kwenye maeneo ambao waakaji hawana uwezo wa nguvu ya pesa Ina maana; hizo nyumba zitachhukua muda mrefu kuuuzika Ukizingatia waafrika hawana utamaduni wa kununua apartment (kununua vyumba kwenye ghorofa)….kwa mtazamo wangu muda sio mrefu sana Mabenk yata anza kudai hela zao huku nyumba hazija uzika. Huu mzigo utarudi serikalini…hivyo naomba wahusika waliangalie hili mapema

Ninavyo ona mimi, Gharama za ujenzi wa Nyumba hizo ukizingatia viwanja wanapewa karibia bure (kwa maeneo ya mikoani) hazina uhalisia. Kiwanja bure, matofali ya bei poa, mabati ya kawaida, Nyumba ya vyumba viwili ya bei nafuu kabisa ina anzia shs 36,000,000 Kijijini????? mijini ndio usiseme ni majanga!

Kwa mtazamo wangu hili ni bomu…na Serikali ijiandae kubeba mzigo huuu!!!!!
 
Kumbe ni Mtazamo, Uonavyo wewe, na sio kwamba umefanya research na ukaweza kugundua vitu fulani fulani.

Unaongea kinadharia zaidi.
 
Kumbe ni Mtazamo, Uonavyo wewe, na sio kwamba umefanya research na ukaweza kugundua vitu fulani fulani.

Unaongea kinadharia zaidi.
Unataka utafiti gani wakati ni kweli hawezi jenga nyumba kwa gharama hiyo unategemea nini yatabaki madeni ya serikali ambayo ni sikivu
 
Wandugu nauliza HIVI WIZARA YA UJENZI MBONA HATUSIKII UFUKUAJI WA MAKABURI. AU HUKO HAKUNA DALILI YOYOTE YA UFISADI. NAULIZA TU
 
Back
Top Bottom