Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mwalimu aliyenifundisha somo la sayansi kimu shule ya msingi aliniambia kuwa maana ya neno uchafu ni kitu chochote kile ambacho hakipo katika sehemu yake, hata kama kitu hicho ni kisafi na kimewekwa katika sehemu safi.
Sahani ya chakula inaweza kuwa safi halafu ikawekwa juu ya kitanda, huo ni uchafu hata kama kitanda ni kisafi na sahani ni safi. Trei tupu ya mayai inayowekwa juu ya kiti cha sebuleni ni uchafu hata kama ndio kwanza imenunuliwa na kiti ni kisafi.
Nimeikumbuka elimu hiyo ya usafi baada ya jana kukatiza maeneo ya mkwajuni pale bondeni kama unaelekea magomeni au unarudi kinondoni studio. Nyumba zilizojengwa mabondeni zimebomolewa lakini mabaki ya nyumba hizo bado yapo mpaka leo. Nilichokiona ni uchafu kwa sababu mabaki yale ya nyumba yalipaswa kuondolewa kutoka katika eneo lile mara tu baada ya zoezi la ubomoaji kumalizika.
Kuendelea kuwepo kwa mabaki yale kunaweza kuwapatia maumivu makubwa ya kisaikolojia wale wote waliobomolewa nyumba zao. Wakati zoezi la ubomoaji likiendelea, kupitia taarifa za habari za usiku, tuliweza kuwaona kina mama na watoto wakilia kwa uchungu. Watu hawa wanaishi na makovu mioyoni mwao. Kila wanapokatiza katika eneo lile na kuona mabaki ya nyumba zao, yale maumivu ya ya zamani yanawarudia tena, kidonda kinakuwa kimetoneshwa.
Katika hali ya namna hii ni rahisi sana kujenga taifa lenye watu wenye mawazo ya uasi kwa kila kinachofanywa au kukusudia kufanywa na serikali. Kwa sababu watu wanaishi huku wakiwa na ushahidi tosha wa mambo ambayo kwao wanaona ni ukosefu wa ubinadamu wa makusudi, ambao wametendewa na serikali yao.
Waziri January Makamba najua huwa unapita sana mitandaoni, wewe na wasaidizi wako, fanyieni kazi ili suala la kuondoa mabaki ya nyumba zilizobomolewa, kwani mazingira ya aina ile haswa eneo la mkwajuni, yanatuaibisha kama nchi inayopambana kurudisha heshima ya utalii. Na pia kibinadamu sio uungwana kwa wale ambao walibomolewa nyumba zao halafu kila siku wanapopita karibu na maeneo yake wanayaona mabaki ya nyumba zao.
Waziri January Makamba fanyia kazi suala hili, kama fedha ya kulipa dereva wa greda ilikuwepo na ipo, kama fedha ya kuwalipa polisi ili ubomoaji ufanyike bila ya vurugu ilikuwepo na ipo, kama fedha ya kuwalipa wataalam wa ardhi ilikuwepo na ipo, kwanini ikosekane fedha ya kuondoa mabaki ya nyumba zilizobomolewa?.
Waziri January Makamba fanya kazi suala hili, sio vibaya ikiwa zoezi la kuondoa mabaki ya nyumba zilizobomolewa likaanza hata mapema wiki ijayo.