Nyumba za kupanga ni shida

jr.kiyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
785
4,847
Nimepanga maeneo ya uswazi fulani nyumba ina vyumba vinne na maliwato mawili kwa upande wa wapangaji ila mwenye nyumba ana choo chake ndani.

Kilichotokea sijui, narudi zangu kwenye harakati za mtu mweusi nafika home nakutana na utaratibu mpya wa matumizi ya maliwato.

Kila liwato moja ni vyumba viwili na ni marufuku kutumia liwato lengine,mfano mzuri asubuhi nilistak kwa muda kwani upande wangu niliyepangiwa nae kwenye matumizi ana familia kubwa hivyo lazima usubiri na wakienda wanaenda kwa msururu huku liwato lengine lipo wazi, basi nikaingia kwa dharura,bwana we nimejuta hapa nafikiria kuhama hii nyumba.
 
Hapo wewe ni chura, wanakupiga teke. Muda si mrefu utakuwa na nyumba yako.
 
Huna haja ya kuhama kwa hiyo sababu mbona ni ndogo sana na huko unapohamia unajua kuna sheria gani?
Hapo ulipaswa uombe samahan tu kwamba ulibanwa usingeweza kujizuia wangekuelewa unaonekana Maskin jeur ww mi nilijua unahamia kwenye mjengo wako?
 
hata ukihama huko uendapo napo utakutana na changamoto zake, kikubwa ni kutoa kighetto chako hata cha vyumba viwili kuanzia
 
ulitakiwa uombe ruhusa kwa walioruhusiwa kutumia hicho choo...

kuhama sio suluhisho utakutana na wenye nyumba vichaa zaidi..

na hii awamu ya magufuli.. wengi wamevurugwaa sana wana hasira hao
 
Cha mtu Mav** ... Wenye Nyumba wanajua kumtia mtu hasira ya kujenga. Cha msingi hakikisha unajichanga unajenga yako ili uweke maliwato kila kona..usipate kelele za yoyote.
 
ukiona watoto wanakimbizana kwenda chooni ujue huyo baba nuksi hebu mshukuru
 
Vumilia tu mkuu hakuna jins.
Ukipenda raha waswahili wanasema nunua ya kwako.
Jitahid kuamuka asubuh ili kuepuka foleni
 
Ahaaaaaaaaa loh uswaz shidaa. Jitahidi utaft chuma ma sebule afu self coz choo ya ndani ina raha yake wakati unaendelea nachart ahaaaaa
 
Sijaelewa, fafanua ulikumbwa na masahibu gani.....nini kilifuata baada ya kuingia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom