Mbunge wa babati Pauline Gekul amenunua nyumba kupitia mnada wa NMB akaipangisha, jamaa akaona isiwe tabu nae kamchezea shere kaenda kulicheza CRDB wamekuja kumfurumusha mpangaji wa mbunge. Kinachonisikitisha badala ya mbunge kumsaidia mpiga kura wake kuondokana na deni yeye kaipandilia nyumba juu kwa juu, hili ni jambo la hovyo sana kufanywa na mtumishi wa umma. Sasa anasingizia eti wapinzani wake kisiasa.
=====================
Nyumba ya mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara, Pauline Gekul (Chadema) iliyopo kitalu X mjini humo, imezua tafarani baada ya mpangaji wake kuondolewa kwa nguvu huku vyombo vyake vikitolewa nje.
Inadaiwa nyumba hiyo ilinunuliwa na Gekul kwenye mnada ulioendeshwa na benki ya makabwela ya NMB mwanzoni mwa mwezi uliopita kisha akampangishia mtu aliyeondolewa juzi na madalali wa benki ya CRDB.
Akizungumza jana kwa njia ya simu, Gekul alisema yeye aliinunua nyumba hiyo kupitia mnada uliondeshwa na NMB kumbe huyo mtu aliyekuwa anaimiliki alichukua mkopo kwenye benki mbili pamoja na CRDB ila haki yake haitapotea.
“Mimi nimewekeza mjini Babati nikiwa mzalendo nikiona siyo lazima niwekeze jijini Dar es salaam, Arusha au Dodoma, kwani napenda kuishi na wananchi wangu ila huyo mpangaji wangu hata taarifa hakupewa,” alisema Gekul.
Alisema tangu ainunua nyumba hiyo imepita mwezi mmoja ila mwanasheria wake anafanyia kazi suala hilo kuhakikisha kuwa anapata haki yake hivyo wakazi wa mji wa Babati wasiwe na wasiwasi wowote juu ya tukio hilo.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa mji huo walidai kuwa suala hilo linaendeshwa kisiasa kwani Gekul alinunua kihalali nyumba hiyo ilipo karibu na shirika la Sido ambayo iliuzwa kwa mnada hadharani baada ya benki ya NMB kuiuza.
“Mji wa Babati hivi sasa upo chini ya Chadema kwani mbunge Gekul ni Chadema na pia halmashauri ya mji wa Babati ni Chadema, hivyo wapinzani wetu wanatumia nafasi hiyo kutuhujumu,” alisema John Tluway mkazi wa mji huo.
Chanzo: Mwananchi