Nyumba ya kupanga NHC (shirika la nyumba)

Nyumba ya kupanga NHC (shirika la nyumba)

Smartbeing

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2014
Posts
323
Reaction score
427
Natafuta kupanga ktk shirila la nyumba la taifa (NHC), sasa nimesikia utaratibu mwepesi ni kuwatafuta wanaokaa humo ambao wanaondoka ndo taratibu za kwenda ofisini NHC zinafuata, otherwise ni foleni ndefu ukianzia NHC.

Naomba kwa yule ambae anamfahamu mtu ambae anaondoka ktk moja ya nyumba hizo hasa ubungo au upanga anisaidie info na kujua mkono wa kwa heri inakuwaje kwa anaeondoka maana ndivyo nilivyopata taarifa.

Aidha naomba mtu ambae ana-taarifa zaidi kuhusu nyumba hizi anishirikishe especially kwenye mambo ya ubora/uchakavu, kero zake na rent inayolipwa NHC.

Happy new year 2015 in advance
 
Watanzania bwana,siunde kwenye ofisi zao ukapate maelezo?ccm imewazoesha vibaya.
 
mkuu izo nyumba wanarithishana hamna anaekubali kuachia au labda ununue jina na uende badilisha NHC kuna jamaa yangu amepata hapo shekilango kwa kununua na kubadili jina fasta
 
Mtu kukuachi nyumba unaeza muwekea mezani mpk 5m otherwise ngumu kumesa
Mpaka january hali itakuwa mbaya zaidi kwa wapanganji wa NHC, kuna baadhi ya wazee wamepelekewa kodi itakuwa 1M maeneo ya kinondoni karibu na Stanbic Bank, mwingine upanga mtaa wa lugalo 900K kwa mwezi.

Tunakoelekea nhc itakuwa ya walionacho ama zitamilikiwa na wahindi tu. Kutoka shirika la umma mpaka la biashara, maana wanataka kodi iwe sawa na za watu binafsi. Kama CEO $19,000 je Directors na Managers watalipana kiasi gani!!
 
Natafuta kupanga ktk shirila la nyumba la taifa (NHC), sasa nimesikia utaratibu mwepesi ni kuwatafuta wanaokaa humo ambao wanaondoka ndo taratibu za kwenda ofisini NHC zinafuata, otherwise ni foleni ndefu ukianzia NHC.

Naomba kwa yule ambae anamfahamu mtu ambae anaondoka ktk moja ya nyumba hizo hasa ubungo au upanga anisaidie info na kujua mkono wa kwa heri inakuwaje kwa anaeondoka maana ndivyo nilivyopata taarifa.

Aidha naomba mtu ambae ana-taarifa zaidi kuhusu nyumba hizi anishirikishe especially kwenye mambo ya ubora/uchakavu, kero zake na rent inayolipwa NHC.

Happy new year 2015 in advance


za ubungo mpya zinaanzia dola 500 kwa mwezi,,, za zamani kodi haifiki laki na nusu ila kuipata hiyo ya zamani tafuta mtu anaekaa umpe hela, wao wanaanzia milioni nane. ukishaichkua unakuwa wewe ndo mpangaji na unaendelea kulipa kodi ya mwezi kama kawaida .... ni nyumba nzuri zina parking , space ya kutosha (hazina uswahili), sebule.vyumba viwili, choo na jiko but sio vikubwa sana...
 
So na kwenyewe kodi inaongezeka duuuh. Ila hiyo ya kumuwekea mtu 5m au 8m labda kodi iwe 50k. I thought bei zipo chini. Mkuu Aye huyo wa Shekilango amepata mpya au ya zamani, na analipaje?
 
Mpaka january hali itakuwa mbaya zaidi kwa wapanganji wa NHC, kuna baadhi ya wazee wamepelekewa kodi itakuwa 1M maeneo ya kinondoni karibu na Stanbic Bank, mwingine upanga mtaa wa lugalo 900K kwa mwezi.

Tunakoelekea nhc itakuwa ya walionacho ama zitamilikiwa na wahindi tu. Kutoka shirika la umma mpaka la biashara, maana wanataka kodi iwe sawa na za watu binafsi. Kama CEO $19,000 je Directors na Managers watalipana kiasi gani!!

Kasome na wewe uwe CEO
 
mkuu izo nyumba wanarithishana hamna anaekubali kuachia au labda ununue jina na uende badilisha NHC kuna jamaa yangu amepata hapo shekilango kwa kununua na kubadili jina fasta

Ukisikia mtu nishtue mkuu
 
Kasome na wewe uwe CEO

Maskini ya mungu wee!! Huo mshahara ni kidogo sana compared with my income!! Nilichokisema hapa nhc siyo SU tena kama linavyojitambulisha. Nawahurumia wale wazee walio staafu na hawalipwi tena mshahara. Na kwa taarifa yako tu, nhc walitegemea wapate faida kwenye miradi mipya, mwishowe wameambulia hasara. Ili kuweza kujiendesha na kurudisha mikopo wameamua kupandisha kodi kwenye nyumba za zamani zilizopo mijini.

Wewe ni mmojawapo wa kuwawanyonya Watanzania!!!
 
So na kwenyewe kodi inaongezeka duuuh. Ila hiyo ya kumuwekea mtu 5m au 8m labda kodi iwe 50k. I thought bei zipo chini. Mkuu Aye huyo wa Shekilango amepata mpya au ya zamani, na analipaje?

nimep mtu milion tano kisha nilipe kodi ili na mie nionekane nimepanga kwenye nyumba za shirika au? si bora hiyo milion nane niifanyie biashara na huku nimepanga nyumba za watu binafsi jamani
 
Huku Tandika zinauzwa Milioni Tano Hadi saba. Gorofa ni kuukuu hivi maji hayapandi na kodi yake ni laki moja inalipwa kwa miezi mitatu mi tatu yaani laki tatu kila baada ya miezi mitatu. Nyumba ni kasebule kadogo vyumba viwili vya kulala kajiko kadogo pamoja na toilet. Ukishainunua gharama ya kuikarabati yaani kui pimp kuweka tiles nini inagharimu zaidi ya milioni tatu hivi. Faida yake ni stress free environment hakuna faza house wala nini. Njoo nikudalalie huku au ni PM.
 
kweli kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.

Kwa sasa wanaotesa ni wale waliopangishwa nyumba na NHC enzi hizo. Mtu akitaka kuhama eti anamuuzia mtu badala ya kutoka tu na kuacha NHC waweke mpangaji wanaemtaka. Nafikiri huko ni kukosa usimamizi mzuri katika shirika. Kataa wote wanaouziana au kurithishana.

Pili, hivi inakuwaje mtu kumlipa mtu milioni 5~8 ili tu ukaishi NHC na bado unaendelea kulipa kodi kila mwezi?...Kiukweli naona kuna matumizi mabaya ya fedha hapa. Halafu utakuta mtu hata hizo M5 au M8 anakopa. Sidhani kama hii ni akili nzuri.

Ni mtazamo wangu tu
 
Hilo linajulikana umeniambukiza wewe mtindio wa ubongo@ asakuta same
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom