Kusema la ukweli sisi wanawake huwa tunachangia waume zetu kwenda nyumba ndogo. Tukisha olewa na kuweka ndani ndio tunaona tumefika. Tunasahau wakati tukiwa wachumba tuliokuwa tunayafanya hata mkitoka kazini wote ile jioni mzee akiitaji kula matembele mbio unakwenda kuandaa, tena wafanya kumbembeleza " Honey leo njoo ule kwangu bwana.... akimaliza ugali na tembele unaachia viwili vya nguvu akha mtu anaende kwake kulala akiwa mweepeeesiii.
leo uko ndani akitaka unadai umechoka kwani mwanzoni ulikuwa huchoki ana hukujua unahitaji kuwahi kwenda kazini asubui. Wakati style zote ulikuwa unampatia uwe umechoka au hujachoka ulikuwa radhi kumtimizia ilimradi tu asiende nje kwa mrembo mwingine. Leo ati umechoka kilicho kuchosha ni nini?
Wanawake tubadilike. Tuliwazoeshe wenyewe hawa waumezetu kipindi cha kuchumbiana.!
Sio nawasema wanawake tu nanyi wanaume pia ukisha amua kuowa basi wale uliokuwa nao nyuma waache, eti mmnakamsemo kenu " PENZI LA HAWARA HALIFI" ukiwa unapewa huduma zote hadi kubebwa mgongoni kinachokupeleka nje kipi? Tulieni na wake zenu.
Kumbuka yale uliokuwa unamfanyia mkeo kipindi cha uchumba utakapo acha kumfanyia basi nae kwasababu anakosa ile huduma ya mwanzo ndipo anapokwenda kwa mlizi,shamba boy, dereva hata house boy pia. Utakuta mwanaume akisharudi mkewe yuko moto jamaa anagusa tu alafu anakoroma unategeme nini kama mkeo haendi kupindwana wafanyakazi wako.
Simpo. Dawa ni kupeana sana, mno, kabisa, every time, mpaka hamu za kwenda huko nje zinakuwa hazipo. Kama huwezi hivyo, utajiju...Huwezi kwenda nje kama huna hamu.
Temea mate chini Kaniki 🙂, umeshasikia msemo wa kipya kinyemi!? Unaweza hata wewe mwenyewe ukabaki unashangaa kutokana na performance yako pamoja na kudhani kwamba 'huna hamu'.
kama umeshamwambia mke na hajaonesha dalili za kubadilika au kukuelewa unadhani nini hutokea? ni kumtafuta msaidizi wake ili uendelee kumpenda mkeo au la utamchukia moja kwa moja.
Raha ya nyumba ndogo ni kwamba inajituma ipasavyo maana inakula kwa jasho lake. Halafu kwenye nyumba ndogo hata ukitaka kujiexpress yourself unapita bila kupingwa
Wakati mwingine hakuna kipya unachokipata huko ila ni ile kubadilisha mboga,si unajua hata maharage uwa matamu kwa sharti ufululize nyama na samaki.
Wengi wetu tunapokuwa ndani ya ndoa ujisahau sana hivyo tukawa si wabunifu,unachoka maana hakuna kipya.Sasa unapoonjeshwa kisamvu tena hata nazi hakina,unabaki ukijiramba midomo.Na kwa kuwa hauendi kwa nyumba ndogo mara kwa mara,siku zote unakuwa na hamu nae.
Kitu kingine,ni heshima isiyokuwa na maana tunayojifanya kuwa nayo ndani ya ndoa,wakati kwa nyumba ndogo kule unakuwa free,unajiachia unavyotaka.Sasa wewe kila siku kifo cha mende,usichoke.Wewe unategemea siku ukipigiwa mbuzi kagoma kwenda,utabaki hapo.
Mbaya zaidi wanawake katika sita kwa sita uwa kama bendera,sasa ukikuta na mwanaume mwenyewe ndo kama mie,anajua kuvamia tuu kwa staili ile ya kifo cha mende tuu,lazima utaibiwa tuu.
Ishuuu inakuja siku umepita katika jukwaa la kikubwa,una mastaili kibao.
Mama naniii leo geukia huko,au kaaa hivi,wewee majibu yako
"Hayo kawafanyiege hao hao hawala zako sio mimi"
Kwa nini usigande kwa nyumba ndogo
MwanajamiiOne
ugumu upo mahala fulani, kwa kuwa wanaume ndo wanaolalamika kupunguziwa ratio ya mgao wa kumbikumbi hivyo suala la akina mama kubadili mboga ni juu yao kwani inasemekana na ainajulikana kwmaba wanawake ni wasiri mno ndo maana watoto huwa ni wa mama, kwa baba ni jina tu.
Hivyo kabla mume ahajafikiria kubadilisha mboga inawezekana bibie ashakula michuzi aina yote mpaka akakinai..
Jamani wanaume huwa watoa weekness pointi za wake zao kwa hao wanawake wa nje, mf. utasikia mwanamume anasema nyumbani sifanyiwe hiki wal hiki so yule wa nje anapata nafasi ya kufanya hivyo, na wanakuwa washindi. WANAUME KUWENI HURU KUZUNGUMZA NA WAKE ZENU NINI MFANYIWE ILI MRIDHIKE. Pili ni kina mama/wanawake pia hawawi huru kueleza waume zao nini wanataka wafanyiwe waridhike. WANAWAKE PIA HUWA WANAONA WANADHALILISHWA MARA TU MUME ANAPOJARIBU KUWA MUWAZI KULEZA NINI ANATAKA, UTASIKIA MKE ANASEMA SITAKI UMALAYA WAKO, UNANIFANYA MIE CHANGUDOA, MARA OOOH HIVYO MIE SIWEZI NA PIA KUJIFANYA UMEMZOEA SANA MUMEO TO THE MAXIMUM NA HAWATAKI KUAPPLY NJIA MPYA KATIKA MAPENZI.
ah we acha tu.Duh kumbe!!
Ila hii dhana ya kina mama kuwa wasiri inatucost wengi. kuna uwezekano kabisa kuwa mkeo ni mwaminifu kwako but kwa vile unaamini kuwa wanawake ni wasiri waweza jikuta umemtreat kama among them cheaters!!
Enewei mbona akina mama wengi wana nyumba ndogo hamsemi ila ngoma mnaipigia kwetu tu?!!!