Nyumba mbili za Lugumi zauzwa kwa Dr. Shika kwa Tsh. 2 bilioni. Mnunuzi abainika kuwa ni tapeli, mnada kurudiwa

Kitendo cha Mama Yono kutangaza mara kadhaa kua mshindi atapanda gari ya serikali wakiwa na maafisa usalama ili waende Bank ilijonyesha walishakua na wasiwasi na huyo bidder. Lakini vilevile ninavoona uwepo wa askari wengi, TRA na watu kutoka vyombo vingine vya usalama kama alivokua akinadi mwendesha mnada kunatoa taswira mnada huo ni zaidi ya mnada wa kawaida na labda kuna kitu wanahisi. Ndio maana kuna wanaosema yeyote atakae nunua nyumba hizo ataanza kufatiliwa ijulikane source ya hela yake,ulipaji wake wa kodi n.k. Tuangalie sinema hii hadi mwisho

Basi huyu mzee kaona isiwe tabu,msururu wawatu TRA na Usalama wote hao kastukia dili akaghairi.
 
Kuna niwanda 30 tuvisubirie kutoka kampuni yake. Nasubiri nyuma ya pazia ya snema hii.
 
akipepewa siku ya mnada baada ya kuwashinda wenzake kwa dau la milioni mia kila nyumba \\

1.jpg
Hahahahaha kama nawaona vile
 
lugumi hanauwezo wa kuhama alilala maskini akaamka tajiri hana lolote hyo historia yake nisawa na mwanafunzi aliyemaliza darasa la saba
 
Huyu ni muhaya wa Muleba, wala hajatoka Urusi.
Aliomba laptop ili alipie kwa mtandao. Inawezekana tatizo ni hatukujipanga kupokea pesa kimtandao. Serikali haina utaratibu huo. Sasa Hutu pesa zake ziko nje. Ilitegemewa anunue kwa akaunti zetu za madafu.

Mimi nafikiri apelekwe mahakamani, kuna kitu kikubwa tutajifunza, na kitabadili mifumo ya nchi kifedha.
Hutu ana akili timamu, ukizingatia aliomba apewe laptop afanye malipo. Pesa alizokuwa nazo haziko ktk akaunti zetu TZ

Akitoka waandishi wamuhoji anaweza akathibitisha kuwa ni timamu, tapeli au wa kupelekwa mirembe
 
Jaman kumbe yule Dr bilionea aliyetaka kununua nyumba za lugumi ni Msukuma?

Ama kweli miaka kumi hii ni ya Wasukuma,sio bure!
IMG-20171111-WA0007.jpg
 
Hivi kumbe passport za tz wanaandika jina la cheo Dr kwenye passport?halafu jina limeandikwa full katika sehemu moja?Hii passport itakuwa fake.
 
Hivi kumbe passport za tz wanaandika jina la cheo Dr kwenye passport?halafu jina limeandikwa full katika sehemu moja?Hii passport itakuwa fake.
Ahahah,unataka kusema huyu bwana kaongopea jeshi la police?
 
Back
Top Bottom