Mnada mwingine mahekalu ya Lugumi

Mnada mwingine mahekalu ya Lugumi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mnada wa mahekalu ya mfanyabiashara Said Lugumi, ambaye kampuni yake inadaiwa kodi na serikali, unatarajia kufanyika kwa mara ya nne baada ya kushindwa kupata wanunuzi katika minada iliyopita.

Kampuni ya Udalali ya Yono ya jijini Dar es Salaam, imesema inajipanga upya kwa ajili ya kuuza mahekalu hayo na kwamba tarehe rasmi ya mnada huo itatolewa rasmi hivi karibuni. Nyumba hizo zilianza kunadiwa Septemba 9, mwaka jana na kufanikiwa kuuza nyumba moja iliyoko Upanga, Dar es Salaam kwa Sh. milioni 700.

Hata hivyo, serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haikuridhika na bei hiyo na kuamua kuufuta, ili kufanya tathmini na hatimaye iuzwe tena. Novemba 9, mwaka jana, mnada mwingine ulifanyika ambao ulimwibua mtu aliyetokea kuwa maarufu, Dk. Louis Shika au mzee wa ‘900 itapendeza zaidi’.

Dk. Shika alijipatia umaarufu baada ya kushinda dau la kununua nyumba hizo kwa Sh. bilioni 3.3 na baadaye kushindwa kuzilipia kama masharti ya mnada yalivyotaka. Nyumba zinazopigwa mnada ni tatu ambazo kati ya hizo, moja ni ya Upanga na mbili zilizopo Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na Nipashe jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Scholastica Kevela, alisema baada ya kufanyika minada mitatu na kukosekana mtu aliyefikia dau la serikali, kwa sasa wanajipanga kutangaza mnada mwingine.

“Kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya mnada mwingine na tutautangaza wakati wowote na safari hii tunajiweka sawasawa kuhakikisha zinauzwa,” alisema.

Awali, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo, alipoulizwa hatua gani inaweza kufuata ili kurejesha kodi inayodaiwa, alisema TRA imezikabidhi nyumba hizo mikononi mwa dalali ambaye atatangaza na kuendesha mnada mwingine kufudia deni hilo.

“Tumezikabidhi mali hizi mikononi mwa dalali kwa hiyo atatangaza lini zitapigwa mnada,” alisema.




Chanzo; Nipashe
 
Dr. Shika sijui yuko api nimemkumbuka tu
 
Back
Top Bottom