Nyumba inauzwa Kitunda Kivule

Nyumba inauzwa Kitunda Kivule

Mipangomingi

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
2,713
Reaction score
2,062
Wana JF, leo nikiwa natoka kwenye pirika zangu, nimekutana na dalali eneo la Kivule Matembele, ameniambia kuna nyumba inauzwa eneo la Kivule/Kitunda kituo cha Daladala Msikitini mita kama 200 kutoka barabara kuu ya Kivule. Ina vyumba 3 vya kulala (1 Master); Jiko, Public toilet, Sitting room, Dining room, Car Park ya ndani, Fence, Tiles, Gypsum ceiling borad, Umeme, Maji na Underground water reservoir, Gari inafika: Bei niliyoambiwa na huyo dalali ni 65M.

Mimi si dalali, nilikusudiwa kama mteja, lakini katika uliza yangu nikapata namba za mwenyewe anayeuza. Kwa kuwa binafsi sihitaji nyumba au niseme sina fedha, nikaona ni bora nishee na wana JF wenzangu. Namba za huyo mwenyewe (sio dalali) ni 0714047718. Mniwie radhi sina picha japo kwa jinsi nilivyofahamishwa hiyo nyumba itakuwa naijua.

Mniwie radhi kwa wote mtakaohitaji picha za nyumba husika na pia sina maelezo ya ziada zaidi ya hayo niliyopewa na dalali, hivyo maswali yote mnaweza kuwasiliana na namba hiyo ambayo kitu kizuri ni kwamba si huyo dalali tena aliyeniambia mie, (Hawa kina kitomari siku nyingine nao huwa wanatuua kwa kutaka chao cha juu).
Jumapili Njema
 
Samahani bwana Mipangomingi na wengineo, hii Kivule ni Ilala au Temeke? naona inanichanganya kidogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom