Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,384
2,000
Mvua zinazoendelea kunyesha katika Maeneo mbalimbali Mkoani Njombe zimesababisha Maafa ya kuezuliwa Nyumba za Baadhi ya Wakazi wa Kijiji Cha Ikisa Kata ya Uwemba Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Jacktan Mtewele (CCM) Diwani wa Kata ya Uwemba amesema Tukio la kuezuliwa Nyumba sita za Wakazi wa Kijiji hicho lilitokea Januari 14/2021 na kusababisha Familia hizo kukosa Mahali pa kuishi.

"Mimi Kiongozi wenu Baada ya kupata Taarifa hii nimekuja niwafariji Wahanga pia nimeona nibebe Baadhi ya mahitaji ikiwemo Unga, Mafuta na Fedha kiasi cha Tsh, 25,000/= ili kuziwezesha Familia hizi japo kupata Chakula wawapo kwenye Maeneo ya kujihifadhi katika kipindi hiki, pia tunaendelea kushiriki Mchakato wa Ujenzi wa Nyumba hizi" Jacktan Mtewele.

Betina Msemwa ni Moja ya Wakazi wa Kijiji Cha Ikisa walioezuliwa Nyumba zao alisema Tukio hilo lilisababishwa na Upepo Mkali ulioambatana na Mvua kubwa iliyonyesha kwa Saa kadhaa Kijijini hapo.

"Upepo huo sijawahi uona Tangu nizaliwe, ulianza kama Jambo la kawaida, lakini ulikuja kuzuka kwa nguvu ukiambatana na Mvua hadi kuezua Nyumba hizi tunaomba Sana Serikali na Wasamalia wema Watusaidie" Betina Msemwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe, Deo Mwanyika Katibu wake Bw, Andreas Mahali aliyefika kwenye Tukio na kuwafariji Wahanga alisema Wamekubaliana na Diwani wa Kata ya Uwemba Mhe, Jacktan Mtewele kuwa Baada ya Kikao cha Tathimini ya Tukio hilo Ofisi ya Mbunge itahakikisha inazishika Mkono Familia zilizo patwa na Janga hilo.

"Leo tumefika hapa ili kuwashika Mkono na kuwafariji Wahanga wa Tukio hili, lakini Tumekubaliana na Diwani wa Kata hii kuwa Baada ya Kikao cha Tathimini Ofisi ya Mbunge itarudi tena hapa kuona namna sahihi ya kutoa Msaada kwa Familia hizi" Alieleza Mahali Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ikisa Leonard Kadaga alisema Serikali ya Kijiji hicho inafanya Mpango wa kuandaa Mazingira ya kuwahifadhi Wahanga wa Tukio hilo huku akiomba Wadau Mkoani Njombe kushirikiana na Serikali ili kurejesha Makazi ya Wananchi hao ambao kwasasa Hawana Sehemu ya kuishi.

"Nyumba hizi kwasasa haiwezekani Watu kuishi humu, Sisi Serikali ya Kijiji Tunaandaa Maeneo ili kuwahifadhi Wahanga lakini hata Chakula hawana inabidi Tufanye Mpango wa kuwaandalia, pia tunaomba Wadau na Serikali Watusaidie katika hili" Alisema Kadaga Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Cha Ikisa. 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom