Nyuma ya Legacy kuna maumivu

Cobra70

Senior Member
Jan 2, 2020
167
363
Nawasalimu wadau wa JamiiForums,

Kwanza nitoe pole na kwa masikitiko makubwa kwa wananchi wa Tanzania pamoja na familia yake kutokana na kifo cha raisi wa awamu ya nne hayati John Pombe Magufuli na pia bila kumsahau aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar hayati Maalim Seif.

Pili: niombe watanzania kutambua mchango na umuhimu wa vyama vya upinzani hasa katika kutia chachu ya maendeleo ya nchi kwa kuibua agenda chokozi, kushauri na kuimarisha ustawi wa nchi mana ili uendelee inaihitaji upinzani na bila upinzani huwezidhihirisha uwezo wako. Kwa hili pia nashauri watu wawe huru kuchagua agenda wanayoipenda na nani wanahitaji awafanyie kazi, kwa asili ya binadamu ni wapinzani ndio maana mawazo, maoni na maono yetu hayawezikuwa sawa kwa wote hivyo kuwaminya wengi wenye maono yanayoendana hili si sawa na halina afya kwa ustawi wa nchi. Kwa ustawi mzuri wa nchi wapinzani wanatakiwa watoke vyama tofauti tofauti ila ukiwaminya na upinzani ukatoka ndani chama kimoja hii ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yetu mana yanayowezatokea tunaweza tukajuta maishani mwetu.

Tatu: Nashauri watanzania tuisome na kuielewa katiba ya nchi yetu pamoja na kuisimamia kidete, kwani kwa kuikanyaga kimaksudi katiba ya nchi inawezasababisha migongano ya mihimili mikuu ya nchi na kuumiza wananchi wasiokuwa na hatia. Hii mala nyingi inasababishwa na uroho wa madaraka kwa watu ambao tumewaamini, kukomoana na kulipa visasi kwa kufanya hivyo ni kumkufuru Mungu kwani viongozi wa nchi huapa kuwa wataisimamia na kuilinda katiba ya nchi ee..h mwenyezi Mungu awasadie. Dhambi ya kumkufuru Mungu wote tunaijua.

Nne: Ili nchi isonge mbele inatakiwa watanzinia tuache UNAFIKI kama kiongozi anakosea aambiwe kuwa anakosea na kama anafanya vizuri asifiwe. Huu ni ugonjwa mkubwa unaendelea kuwatafuna vijana wanaamini kwa kujipendekeza kwa viongozi wakubwa kwa kutukana wenzao, kuwaumiza wenzao, kusifia matendo maovu ya viongozi wao, kuuza sura, kufitinisha, kusaliti wenye uhitaji kimaksudi kuwa inaweza kuwa nyenzo kwao ya kuonekana na kupata TEUZI.

Tano: Watanzania tumuunge mkono Mh. Rais Mama Samia Suluhu kwani yupo hapo kwa mujibu wa katiba ya nchi na tujue pia kila anapoingia raisi mpya kwenye hatamu huwa anaingia na mfumo wake ambao anahisi utamsaidia ili nchi ipige hatua ya maendeleo kwa haraka. Yanayotokea bungeni ni wasi wasi tu na mishtuko ya baadhi ya wabunge hasa kwa wale walionufaika na awamu iliyopita mana kwa sasa hawajui kesho yao ipoje wenda kwa nafasi zao walizokuwanazo na ushawishi waliokuwa nao na pia kwa biashara na tenda walizokuwanazo au milango waliopitia kuingia bungeni.

Wengi wao wamekuwa wanaongea hadi wanatoa macho kwa kutetea LEGACY ambayo sio agenda ya nchi. Ni haki yao kupiga kelele Mana kama ukizoea Kubebwa na aliyekubeba hasiwepo ni lazima uwe na wasiwasi na hofu kubwa. Niwaondoe tu wasiwasi vijana tuache MITELEZO na KUBEBWA tufanye kazi na kuwajibika kwa kufanya hivyo mtaonekana kwa viongozi wa nchi katika teuzi na pia wananchi si wajinga watawaona na hawatawaangusha katika CHAGUZI. Tumuachie mama afanye kazi tutampima kutokana na utendaji wake na namna anavyokabiliana na changamoto zinazowagusa wananchi moja kwa moja na maslai mapana ya nchi.

Tujifunze kuwa LEGACY ya mtu inatafsiriwa tofauti kati ya mtu na mtu kwa namna gani mtu amenufaika kwa mtu tofauti na hapo mtakuwa mnapiga KELELE zisizokuwa na maana na hamtakaa elewana na pia wananchi tutawapima nyinyi akili na uwezo wenu kuwa finyu na kuwatilia shaka njia mlizotumia kuingia humo bungeni kwa kujisifia na kukashifu vitu vya nyuma na kusahau changamoto za mbele ambazo nyingi.
 
Back
Top Bottom