Nyuki wema, nyuki wabaya!

Nyuki wema, nyuki wabaya!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,101
Reaction score
828,958
Preamble! Chitchat sio sehemu salama sana siku hizi....! Uongozi usipokuwa makini JF itapoteza heshima yake

Sasa tuendelee na mada yetu
Je unajua kuwa Nyuki ni mlinzi kiroho na ni silaha pia ya kutumiwa pia na watu wabaya?
Hulka ya nyuki kuruka mbali na udogo wake ule na kurejea kwa usahihi sehemu alipotoka, hulka yake na kuweza kuchagua maua ya kunyonya ute a kutengeneza asali kwenye maua na mimea isiyo na sumu, hulka yake ya kuchagua choo kwa ajili ya kupata pia ute wa malighafi unamfanya awe na nguvu ya kipekee kiroho... Si kila choo nyuki anaingia na si kila ua nyuki anatua....
Sasa kutokana na sifa zake hizo..... Kuna wakati unapoingia kwenye mapambano ya kiroho na unapokuwa umeanza kupata kinga... Let's say kuogea chumvi nk... Usishangae kuona kundi la nyuki linakuja na kufanya makazi hapo kwako.... Lakini hapa kuna mawili... Zingatia sana haya...

1. Wakija hapo na kuwa wapole bila kuleta dhahama yoyote jua hapo umeletewa ulinzi na hupaswi kuwaogopa wala kuwabughudhi.. Wapo hapo kwa nia njema kabisa na kitisho cha hatari kikiisha watajiondokea wenyewe na kupotea kusikojulikana

2. Kama utakapoanza tiba yoyote ya kiroho na likaja kundi kubwa la nyuki na kuanza kuishambulia familia yako ama wewe mwenyewe na watu wengine karibu ya hapo.... Jua wazi vita ni kubwa na hao maadui zako wanataka kukuwahi na wameshaona udhaifu kwenye tiba yako hiyo hivyo nao huwatumia nyuki hao hao lakini wakiwa ni wa kichawi kuja kukudhuru... Maranyingi wanaweza kuja maramoja na kuacha madhara makubwa ama la wanaweza kurejea kila wakati na kuchimba bit tu! Utawambuaje hawa? huwa wanachagua wa kushambulia tofauti na nyuki wa kawaida waliochokozwa ambao humuuma yeyote!!!
Kwahiyo makinika sana Unapoanza hizi tiba za kiroho kwa kila jambo linalokutokea.... Na hili la nyuki ulipe kipaumbele kwakuwa laweza kukutokea hata nje ya makazi yako... Unajikuta wanakuzigira na kukuzunguuka tu bila kukuuma.. Ama la wanakushukia na kufanya yao
 
Mkuu nataka kuanza Rasmi somo la Meditation kwa hapa Bongo sijui
ni wapi, halafu nina safari ya India ambayop itanichukua miezi miwili
vipi inatosha huko kujifunza kwa hiyo miezi 2, na wapi nitapata mafunzo hayo.

Pole kwa kutoka nje ya Mada lakini nyumba iliyopo karibu na Mkutano
ndiyo ambayo watu huomba maji.
 
Ngoja niangalie hawa ninaowafuga ni aina ipi(maana wamehamia muda kweli kweli hapa kwangu)
Wananyan'ganyana chakula na kuku wangu... uzuri hawana uhasama na watu wa nyumba hii. Nikiwafukuza wanarudi
 
Hongera sana kwa Dar nenda Mindu street ni barabara ya pili ukitoka ya kuingia Muhimbili ukitoka Fire hesabu nyumba ya tano hivi mkono wa kulia utakuwa umefika!
Kwa huko India utafaidi japo sijui unaenda mji gani anza kabisa ku Google meditation centers za huko
 
Sawa na Ahsante Mkuu, kumbe ni hapo kuna ukuta una maandishi
mengimengi ya Kifalsafa, Vipi Lugha inayotumika hapo maana ndio wasiwasi
wangu mkubwa kabisa.
 
Sawa na Ahsante Mkuu, kumbe ni hapo kuna ukuta una maandishi
mengimengi ya Kifalsafa, Vipi Lugha inayotumika hapo maana ndio wasiwasi
wangu mkubwa kabisa.
Kuna mwaliko hapa tunaweza kukutana huko
IMG-20180520-WA0278.jpg
 
Kweli kabisa mkuu chitchat ni full fujo,, huwa nachungulia tu nasepa
 
Lakini yule waziri mkubwa kabisa wa awamu ya kilimo kwanza alituhimiza sana tuwafuge, sasa mbona kututisha,,? Maana yawezekana wakaja kutoka kusikojulikana wakamshambulia jirani na familia yake ikasemwa ni nyuki wa jirani nanii wale...
 
Tuelewane.... Ninaozungumzia mimi sio hao wa kufugwa..... Wanatoka kusikojulikana
 
Ngoja niangalie hawa ninaowafuga ni aina ipi(maana wamehamia muda kweli kweli hapa kwangu)
Wananyan'ganyana chakula na kuku wangu... uzuri hawana uhasama na watu wa nyumba hii. Nikiwafukuza wanarudi
Usiwafukuze waache... Wanga hawawezi kamwe kusogea hapo
 
Back
Top Bottom