Nyuki Washambulia Majeruhi wa Ajali Uturuki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyuki Washambulia Majeruhi wa Ajali Uturuki

Discussion in 'International Forum' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 30, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Iliwabidi waokoaji wabuni njia za kujikinga wasishambuliwe na nyuki
  Watu zaidi ya 20 wamelazwa hospitali nchini Uturuki baada ya gari lililokuwa limebeba mizinga ya nyuki kugongana na lori na kusababisha nyuki wenye hasira wawashambulie majeruhi na watu waliokuja kuwaokoa majeruhi. Gari lililokuwa limebeba mizinga ya nyuki liligongana na lori na kisha kupinduka jana katika mji wa Marmaris uliopo kwenye ufukwe wa bahari ya Mediterranean kusini magharibi mwa Uturuki na kupelekea nyuki wenye hasira wawashambulie majeruhi na watu waliojitokeza kuwaokoa majeruhi wa ajali hiyo.

  Watu sita walijeruhiwa kutokana na ajali hiyo na watu wengine 20 wakiwemo polisi na watoa huduma za kwanza ilibidi wawahishe hospitali baada ya kushambuliwa na jeshi kubwa la nyuki wenye hasira kwa muda wa lisaa limoja.

  Ili kuwaokoa majeruhi wasiendelee kushambuliwa na nyuki hao ilibidi kikosi maalumu cha wataalamu wa nyuki kiitwe kuja kuwafukuza nyuki hao.

  Katika majeruhi sita wa ajali hiyo, majeruhi mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 18 alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali lakini sababu ya kifo chake haikutajwa kama imetokana na nyuki hao au majeraha aliyopata kutokana na ajali hiyo.
   
Loading...