Nyuki wameingia ndani,baadae wamekufa wenyewe

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,297
3,971
Kuna nyuki waliojitokeza ghafla tu na kuanza kupenya ndani kabla sijafunga madirisha vuzuri.
Wakati ninafikiria nifanye nini kuwaondoa,niliwasha feni ili kuwavuruga.Niliwaona wamejikusanya sehemu moja ya kioo cha dirsha,wakatulia.
Hata hivyo baada ya muda,walianza kuanguka chini na wakafa.

Je hali hii ni ya kawaida ukizingatia ninaishi mjini na hii ni mara ya kwanza ninakutana na kitu hiki?
 
It's normal circumstances in countryside,mi pia walikuja japo naishi nje ya mji kidogo. Ila pia wakaniambia ni bahati mana walikuwa hawana shida baadae wakaondoka in case of town sijajua ila nikuwa na imani mkuu
 
Yes uwa wanasema nyuki wakija kwako ni bahati,pia ni ishara ya ulinzi.
 
Kama unatoka makabila yenye asili ya uwindaji au upoli Poli. Hiyo kwako Ina maana mbaya.

Hao ni wazee wa ukoo. Walinzi wa ukoo,kama wamefia kwako kuwa makini. Inawezekana umepigwa pigo au utapigea pigo. Ambalo wao hawaliwezi kulihimili.

Kama mna asili ya kutambika kwenu fanya hivyo haraka sana na toa sadaka haraka.

Kuwa makini ni ishara mbaya kiloho. Hauko salama Tena na upo katika vita kubwa ilio kuzidi umri.
 
Hakuna lolote mkuu. Ni jambo la kawaida. Nyuki akishafanya mapenzi na malkia wa nyuki anakufa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom