Nyuki kuokoa hekta 7,270 za misitu ya Pugu na Kazimzumbwi

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Kazi12.jpg

Alphonce Matata (aliyeshikilia sega) akiwaonyesha maofisa wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika, Alicia na Anna Salado (wa pili na wa kwanza kulia walio katika mavazi maalum) wakati walipotembelea msitu wa Kazimzumbwi kushuhudia urinaji wa asali.

JUMLA ya hekta 7,270 za misitu ya hifadhi ya Pugu na Kazimzumbwi zinaweza kuokolewa kutokana na miradi ya ufugaji wa nyuki iliyoanzishwa sasa, imefahamika.

Misitu hiyo, ambayo ni miongoni mwa Misitu ya Hifadhi 486 iliyopo nchini, imekuwa hatarini kutoweka kutokana na shughuli za kijamii hususan uvamizi wa mipaka na ukataji wa miti kwa ajili ya uchomaji mkaa ambao kwa muda mrefu umekuwa ukifanywa na wananchi mbalimbali.

Meneja wa Misitu hiyo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Mathew Mwanuo, anasema kwamba, misitu hiyo iliyopo katika wilaya za Ilala mkoani Dar es Salaam na Kisarawe mkoani Pwani, imekuwa hatarini kutoweka licha ya jitihada za serikali za kukabiliana na wavamizi hao.

Soma zaidi hapa=> Nyuki kuokoa hekta 7,270 za misitu ya Pugu na Kazimzumbwi | Fikra Pevu
 
Back
Top Bottom