Nyota yako leo alhamis juni 26/2025

Nyota yako leo alhamis juni 26/2025

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
NYOTA YAKO LEO ALHAMIS JUNI 26/2025:
IMG-20250625-WA0021.jpg

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILREKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI
MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Nyumbani kimeingia tafrani hali si shwari simamia jambo hili kwa umakini Kuna tuhuma nzito zinazowagawa kuhusiana na uadui wa siku nyingi Kaa chini na wazee na mtafute njia ya kulimaliza kabla halijafikia pabaya Kuna mambo ya kishirikina ndani yake.

★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Jipange kwa kuanzisha shughuli zako nyingine hiki ni kipindi kizuri sana kwako kufanya hivyo Kuna misaada na mikopo utakayo fanikiwa kuipata changamkia fursa hiyo Kuna habari za mimba na mtoto zitakufikia tarajia kupata kitu kipya sio vibaya kufanya sherehe kwa leo.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Leo utapokea pesa na kazi mpya ambayo ulikuwa umeahidiwa Utalipwa madai yako baada ya malalamiko na kupigizana kelele Omba masaada utapata japo hautakuwa wa kudumu Ni siku nzuri kwenye mambo ya uchumi na kipato.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Kutakuwa na maelewano mazuri na wenzio siku nzuri kwako kukutana na jamaa zako na kujadiliana Kuna makubaliano ambayo mtayafikia kuna kuingia mkataba wa jambo fulani utajikuta kwenye mahusiano mapya na mmoja wa jamaa au ndugu yako wa karibu.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Shughulilikia mambo ya nyumbani inaonekana shida zako zinahusiana na mambo kutokuweka sawa ongea na wakubwa watakupa maelekezo ya nini cha kufanya acha dharau Lipe uzito suala hili kabla halijakukalisha chini omba msaada na itakubaliwa.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Unahitaji msaada katika mipango yako mabadiliko unayoyataka bila kusaidiwa huwezi kuyafanikisha Omba utapewa lakini sio kwa kipindi hiki shughulikia masuala ya mkopo na elimu ya watoto Utapokea mualiko wa sherehe kama ni peke yako usiende.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Siku yenye utata utakutana matatizo madogo madogo yanayojirudia
Utapata mafanikio lakini ni baada ya kuzuka rabsha cheo unachokitarajia kina gombaniwa na viongozi wako lakini utakipata baada ya msuguano mkubwa masualavya biashara yatakuwa ni ya kugombea chukua tahadhari yanaweza kukufikisha pabaya.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Siku nzuri na maelewano utajikuta umeingia kwenye penzi jipya na mtu uliye zoeana nae Utahudhuria kikao utakachofanya na wenzio na kitakuwa kizuri mtaingia makubaliano na kusaini mkataba wa kandarasi mlioyoipata Siku ya leo ni nzuri kwa kumaliza tofauti zenu za muda mrefu.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Mambo yako yameingia ugumu kila kitu kimekwama hii inatokana na kuwa na maadui wengi Umekuwa mtu wa kutokujali na kudharau baadhi ya mambo chukua tahadhari kabla hujaharibikiwa Utalazimika kutumia nguvu katika baadhi ya mambo ili walau upate nafuu.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Unahitajika kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako acha kuishi kwa mazoea Ile safari na mpango wako wa kuhama endelea nao una maslahi kwa upande wako Utapokea mgeni au kupata habari mpya zinazohusu mtoto.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Uko kwenye kipindi kizuri cha kupata mafanikio masuala ya kazi na pesa hayata kupa usumbufu tegemea leo kupata pesa kutoka kwa mtu uliye ongea nae kuhusu kukupa kazi Utafanikiwa kupata cheo kazini na kujikuta unaheshimika na biashara zitakuendea vizuri.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Unatakiwa kuwa karibu na rafiki yako ni kipindi ambacho utajikuta hakuna jambo unaloweza kulifanya bila yeye Mshirikishe na muweke karibu kila mtakachofanya kitawanyookea Siku nzuri kwa kufanya matembezi ya hapa na pale na kuwasiliana na ndugu.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom