Nyoka wa ajabu

Suala la mimi kukufanya wewe uamini kama yupo au hayupo sina muda huo...ila endelea kuamini kile unachokiamini...maana kila nafsi itakufa katika yale iliyoyazoea na kuamini.....
Imani kwangu sio mahala pale. Asante
 
Kwa imani yangu ningechukua maji ya baraka na rosari naweka kwenye mto wa kitanda ila sala lazima halafu unalala weee.
Ila mi ndoto ilikuwa kwenye kochi tena mchana kweupeee na ilikuwa ugenini.
Asante sana
 
Ila mi ndoto ilikuwa kwenye kochi tena mchana kweupeee na ilikuwa ugenini.
Asante sana
Don't be superstitious, tulia kunywa maji mengi labda ulikuwa na njaa sana wakati unaota ikawa kama unatafuta chakula? Waza mtu umpendaye, mpigie simu, mwambie unampenda, tembelea bustani za maua, vuta harufu nzuri ya maua kama upo sehemu zenye summer flowers utaona raha tuuuu. Be blessed.
 
Don't be superstitious, tulia kunywa maji mengi labda ulikuwa na njaa sana wakati unaota ikawa kama unatafuta chakula? Waza mtu umpendaye, mpigie simu, mwambie unampenda, tembelea bustani za maua, vuta harufu nzuri ya maua kama upo sehemu zenye summer flowers utaona raha tuuuu. Be blessed.
Wala sina shaka, ndoto ilikuwa jumapili mchana na mpaka sasa niko sawa kabisa... Japo nilikuwa na shauku ya kijijua kuwa mimi ni nani ila niko sawa. Asante kwa ushauri mzuri, nitaenda bustanini... Napenda harufu za maua
Asante sana
 
Daaaaaah mshikaji wangu we noumaaaaaaa watu wanaota wao ni kina bakhresa, mengi, ww unaota uwe nyoka, mamaaye
 
Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?


Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
Pole sana hii inasababishwa na maCCM
 
Sina mashetani mkuu
Sio lazima yapande kichwani kaka! Jinsi tunavyoishi kienyeji mashetani wanafanya wanavyotaka kwenye maisha yetu.Ndoto za ajabu ajabu na za kutisha ni ishara ya kutawaliwa na haya madude.
 
Sio lazima yapande kichwani kaka! Jinsi tunavyoishi kienyeji mashetani wanafanya wanavyotaka kwenye maisha yetu.Ndoto za ajabu ajabu na za kutisha ni ishara ya kutawaliwa na haya madude.
Mi siishi kienyeji na wala sina mashetani,
 
Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?


Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?


Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
13.+Bronze+snake+BV.jpg
 
Juu ya Mpangiko wa Ulimwengu Mpya
30 Septemba 2011 saa 10:01 mchana/ jioni
YAH: Mazungumzo na mabadilishano ya mawazo kati yangu na mjumbe mmoja wa JF kuhusu 'Mpangiko wa ulimwengu Mpya'--ambapo ni muendelezo wa uchanganuzi wa picha ya 'New World order' na mawazo mengine... 27th November 2010

****

Ninajuaje kwamba ninachokijua mimi ndiyo kweli na si mapokeo ya watu fulani...

... Ngoja kidogo; sayansi ni maarifa yapatikanayo kwa kufanya vitendo vya majaribio, kutizama kiuchunguzi na kuzijaribu kweli zinazosemwa.

Yote nitakayosema ninapenda na kutaka yajaribiwe hivyo. Utakuja kuyasikia/kusoma na kuyajua niliyomaanisha kuyasema halafu na wewe utaamua kwa kadri ya ubora wa upeo wako na mawazo. Ni kheri tu.

Ninaonaje ukweli huu haunihusu mimi pia? Babu, unahusu kwa sana tu... Lakini miye pia ni msafiri katika njia, mara kwa mara nachomoa ramani yangu na kucheki ni wapi nilipo na wapi naelekea; pia nasoma na kusikiliza ishara za wengine barabarani--Ukichukulia ukweli kwanza ni starehe sana kutembea katika njia na kuwa mtiifu kwa vipassana.

Ninajuaje kama njia za kupima ni bora(?)

Ulimwengu wote uliodhahiri ni lugha na mawasiliano; kadri unavyopata umahiri kwa kuusoma, kuulewa na kuusikiliza ndiyo unapata ushahidi wa Kweli na Haki. Mara nyingi hata kilichodhahiri si ukweli wenyewe hasa na hivi ni ufundi daima kujaribu kufafanua mashauri na kujitahidi kuwa bayana katika maelezo na mhutasari. Mara nyingine katika kuiingia maana ya jambo ama kweli ya kitu unaweza kugusa ufafanuzi wenye msigano kidhana na mapokeo ya nje... Lakini ukiwa ni mwendesha baskeli katika njia za kweli daima huogopi kupepesuka; kwa bahati njema daima ukidhamiria kwa dhati kufanya hivyo mizania yako ya kuwa katikati hukuteka na kukustahimilisha. Basi ni vema daima kukomaa na kudhamiria kuchungua yote bila kuhofu kuangukia upande... Kuna miujiza mingi katika maisha, ndivyo tuseme wengi wanaweza kudai hivyo, lakini siri yake iliyowazi ni kujitosa kuthubutu mambo fulani pasipo kusita wala kujizuia kwa hofu na mashaka. Hayo mengine ulimwengu utajali, lako la kushika ni Nia njema...

Baraka

By Kiranga

Kuna mambo nakubaliana nayo, wakati mengine napata ugumu kukubali.

Paragraph yako ya tatu imebeba ukweli mkubwa ambao wengi wetu kwa kutokana na egoism au hata kufumbia macho tu, tunaweza kutouona. Na mara nyingine hata watu wanaohubiri ukweli huu kama wewe huwa unawahusu lakini hawalioni hilo. Unajuaje kwamba ukweli huu haukuhusu wewe pia?

Unajuaje kwamba unachojua wewe ndiyo kweli na haki, na si mapokeo ya watu fulani tu ?

Unajuaje kwamba njia zako za kuupima ukweli ndizo sahihi na bora kabisa ?

By Mose

Kuna Mpangiko wa Ulimwengu uliowenyewe hasa; na kuna jitihada famba na kusanifu mifumo na tawala pamoja na udhibiti wake.

Katika nadharia za njama, watu huteta kuhusu uwezekano wa Watawala fulani kuhodhi michakato ya umma katika kuibana hiyo ndani ya muundo fulani wa kufanyikia sura. Hii ni silika yenye kuchimbia hadi ndani sana miongoni mwa watu wachache wenye kupenda utawala. Mara nyingi hata yale mambo mengine yanayohalalishwa kijamii kutokana na dhana, falsafa, itikadi ya ushawishi ya vyombo tuvitambuavyo kama taasisi; huongezea kwenye sura fulani ya mpangilio wenye maslahi zaidi kwa kundi fulani.

Wanadamu katika hali ya utashi wa kawaida, demokrasia yao, mifumo ya kiutawala na utendaji ni nadra kulenga shabaha ya udhahirisho kwa 'HAKI'. Haki ni shauri tata katika ustawi wenyewe hasa wa jamii. Haki ni kama mizania ya mienendo ili kufungamanisha 'kawaida' fulani. Kawaida ni siri ya 'SHERIA' lakini pale ambapo watu hawamaizi kikamilifu 'KWELI' ya sheria wao hufanyiza namna ya mashauri na kuyaita mashauri hayo ni sheria; halafu huyasimamisha kwa mujibu wa Taasisi zenye wajibu wa kutenda 'utekelezaji wa Haki'.

Je, kumepata kuwepo kipindi chochote cha wanadamu ambapo watu walikuwa sawa kifanaka ama tuseme hapakuwa na umaskini? Matumizi ya fedha kama kizio katika kuakisi mikondo ya mabadilishano ni uvumbuzi wenye kufuatisha mabadilishano yaendenayo na faida; je, ziada katika mabadilishano ikiwa huhifadhika na hadhi ya vitu kukua na kujitokeza tena na tena kama ilivyo asili juu ya nchi yote ... Je, hadhi ya uchumi hufungama vipi na mazao ya asili yenye kuchipua, kukua na kutafunwa katika uchumi hai wa watu? Je, katika ulimwengu wenye mapinduzi ya tekinolojia--matumizi ya nishati katika kuleta tija ya uzalishaji mali na pia ongezeko la huduma za bora za malazi kama upatikaji wa maji....nini hatma ya Uchumi wenye kujishikiza katika utaratibu wa mahodhi na ulimbikizaji?

Katika ulimwengu wa ongezeko la maarifa na tekinolojia; uchumi limbikizi ni mfume dume usiohitajika tena kwani kuendelea kwake kuwepo kunaleta athari la migogoro ya kiuchumi na kuporomoka vibaya kwa ustawi wa makundi mengine ya jamii. Manufaiko ya rasilimali na huduma muhimu hujikuta yakijilimbikizia kwa 'wateule' wachache' na huku wengi wakabakia mikono mitupu na tena hata kulazimika kuuza jasho lao kwa ujira mdogo wa kuwatumikia 'wenye nazo' na hali hata hivyo wenye kubania kile walichonacho. Nguvu ya msukumo kwa uzazi nayo hufunua sura adimu ambapo wale walionacho hujidhibiti hata katika uzao na hali wale wasionacho hujisahau na kujiachia na hali haya yakileta ongezeko la makundi ya maskini wanaozaliwa kwa wingi katika makazi yaliyoduni...

Katika kutambua haya na zaidi, nimeandika muktadha mpya wa uchumi mama wenye kuweza kuondoa maradhi ya uchumi wa leo na ustawi wake. Msingi mkuu wa sura ya uchumi huu ni kanuni mama ya uzima wote... Kuwa vitu vyote vimehifadhika katika mwili mama ambao kutunza na kustawisha vile vyote vidogo vifanyikavyo katika milki yake. Ni mawazo mapya juu ya utu na ustawi...

Mambo kama dini na mapokeo yafanyayo ustaarabu wa wengi bado ni mashauri yenye 'kubana' na 'kuthibiti' mawezekano ya mikunjuko ya kiutamaduni ya jamii husika. Sehemu ya watu kuhofia njama ya kundi fulani kuhodhi 'uhuru' wao wa kidini ni muakisiko wa hofu yao wao wenyewe--toka ndani inayowafungamanisha na dini ama imani zao fulani fulani. Wanadamu wamejua muktadha wa dini zenye kuamuru na kuagiza... Wanadamu wengi hata leo hawezi hata kufikiri dini ni Uhuru... Kwa kuwa dini haina chochote cha kuhusiana na mtu mwingine. Kila mtu huzaliwa peke yake kabisa na atakufa peke yake kabisa na hivi ikiwa kuna wajibu kwa kutafuta 'siri' za kuishi na kuwa basi hiyo ni safari binafsi kabisa ya mtu; hakuna hata mwingine mwenye kustahili kuingilia labda ikiwa mtu hujichakachua kufikiri mtu mwingine ndiye anayepaswa kumpangia yeye hili ama lile. Kuogoa na hata kuogopana hakuna uhalisia hasa kwani daima hilo linaishi pamoja na uwezekano wa mtu kuogopa hata kimvuli chake yeye mwenyewe. Mtu anao uhuru wa kuchunguza dini zote, imani zote na kujaribu yeyote kati ya hizo na hata kuachana nazo akiona si zenye kumfaa. Hofu ni fimbo inayotumika pia kuwadhibiti watu na machaguo yao. Na hata pale watu wanapochagua kuona 'tatizo' na hali ni kiwingu feki; hata lile tumaini linalowezekana la uhuru kamili na mwongozo wa kuelekea kwake hufumbwa kuonekana. Ndivyo hivi katika ulimwengu huu, kwa mtu mmoja jambo laweza kuwa ni tatizo na hali kwa mwingine wala si tatizo. Binadamu hujifunga wao wenyewe kwa kwamba za udhanifu usiokuwa na kina; na pia kukosa fikra zenye mizizi katika kweli 'isiyotikisika' na tena huku wao wenye wakaogopa kutikiswa kwani wajua hata imani za wengi ni mapokeo ya juu juu tu na wakati mwingine ni mwendelezo wa ujinga na kasumba.

Mpangiko wa Ulimwengu mpya ni tumaini na jaribio la nyakati zote katika mkunjuko na ustawi wa wanadamu. Kama vile tambi mbili za misokoto ya DNA yapo mambo matatu yanayofanya uwezekano kamili wa kufanyika kwa Mpangiko wa Ulimwengu mpya. (1) Kung'amua sura iliyohifadhika ya kheri ya madhahirisho yote--hapa ndiyo muktadha wa mungu na uhandisi wa ulimwengu mzima unahusu. (2) Kujua kuwa maumbo yote, madhahiriko yote na Uzima wote ni sehemu ya MOJA ilisiritika. (3) Kujua kuwa Utu au tuseme uanadamu ni Mkirimiko wa kuwa na umbo, akili na NIAkatika kudhahirisha KWELI iliyosiritika katika yote na mote. Uanadamu ni kitovu cha utashi katika kuchagua akili kumbukumbu na akili ya king'amuzi.

Mpangiko wa Ulimwengu Mpya ni fahari ya kutaniko la maarifa ya maumbo na siri za uzima... Ni usanisi unaokutanisha 'mambo ya kiroho' na kisomo cha akili kumbukumbu. Pale mtu apotezeapo funguo kwa 'KWELI' za 'kiroho' hawezi ng'amua ile SHERIA na NJIA ya kuleta Mpangiko wa Ulimwengu Mpya kwa kuwa yeye mwenyewe hasa ndiye ni lile jiwe lenye kusimikwa mahala pa mwanzo katika ujenzi.

Japo twazungumza juu ya nyakati katika uhandisi wa 'roho na uzima' hakuna 'wakati' na hivyo siri za Mpangiko wa Ulimwengu Mpya na 'Ufalme Usiohamishika'. Yote yalikatika uwezekano yapo hapa na sasa na ikiwa mtu asikiliza ndani ya kimya na ukimya wa nafsi yake; uwezo wa kupokea picha kwa 'Mpango Mzima' upo na kila mtu. Kutafuta siri za 'Ufalme usiohamishika' ndiyo jambo la msingi kuliko mengine yote ikiwa mtu ni mwenye kutaka kufanyika upya katika KWELI na HAKI. Mapenzi kwa hii KWELI humuinua mtu na kumuongoza katika STAHIKI yake--japo ili kuwa hivi humpasa mtu kuruhusu iwe kwake ndani NIA kama NIA iliyokatika 'Mpango Mzima'.

Mwili wote wa 'Uzima na Wakati' ni chombo chenye kumbeba mtu ili afikie katika ufahamu ulio ni nuru na pumzi kwa yote. Kuna usifa akili katika kila kitu kilichofanyika... Vitu vyote ni viumbe hai katika usirifu wake. Mwanadamu anapoishi kujiandaa kuwa moja na ile hadhi iliyofichika ya usifa-akili hai ubebao na kustawisha yote; yeye huwa ni Boddhisatva kwa mujibu wa dhana, mafundisho na mapokeo ya utamaduni kwa Kibuddha. Ndiyo hivi katika njia ya Buddha, msisitizo katika mapokeo hayo upo katika ufahamu na kuyeyukia katika huo; kwa kuwa huu ndiyo kila kitu. Na hivi katika Ubuddha hakuna msisitizo wa 'mungu' kwa kuwa tayari ulimwengu wote ni mama mzazi na baba mzazi kwa yote yaliyodhahiri na yale yasiyodhahiri.

Katika mapokeo ya dini za magharibi kuna mungu; kwa kuwa mungu ni alama na ishara ya 'ukamilifu', mamlaka na kilele katika sura ya muundiko. Na ni namna ya kiegemeo kwa kudhanifu mpango uliowekwa... Lakini hayo yote yamekuwa na maana katika vizazi na ustawi wa wanadamu. Ndani ya miaka 20 ijayo sehemu kubwa ya udhanifu wa mungu kama mtawala utatoweka katika akili za watu. Si tu tekinolojia na matukio mengine yataleta ufunuo kwa walio wengi, lakini umma wote wa duniani utang'amua ya kwamba japo dunia ni hadaa, Ulimwengu daima ni Shujaa. Ulimwengu una mambo mengi mazuri ambayo hayajawahi hata kufikirika huko nyuma... Na pia ulimwengu una maajabu mengi isivyo idadi na hivi ndani ya 'Mpango Mzima' siye kama viumbe hukirimika kutaamulika ilivyobora kabisa kuwezekana. Na itajulika: UTU ni ua katika mapana ya dahari na si kizio cha safari ya mtu kuzaliwa na kufa. Hatuwezi kujibainisha utu wetu kwa misingi ya kuwa tu hapa ama pale... Mambo yote yamekwishafanyika katika sehemu yenye KWELI--Ilivyo jana, leo na kesho. Mingine yote tunachagua kipi kutukia katika kila nukta ya 'WAKATI'.

Kwa kadri ambavyo watu hawana utahayari wa kutafuta siri na nafsi roho zao, siku zote watatokea vinara watakaopitisha mashauri ili kuwaendesha wengine. Na hata ikiwa wengi watatekwa katika njia ya uharibifu daima wapo ambao 'KWELI' huwa ni dhahiri--wao huponea chupu chupu na kuweza kuvuka hata vigingi vya migogoro na maangamizi. Ni hawa ambao daima katika nyakati zenye uwezekano wa migogoro hutumika kama 'vipitisho' vya siri ya kuponea. NA siku zote hawa hujaribu kufanya usikronizi kati ya kuponea huko na jitihada za kujaribu kuanzisha mfanyiko wa ulimwengu mpya. Kila nyakati za majaribu yenye kuweza kudondokea katika migogoro na uangamizi wa ustawi wa wanadamu kuna funguo kwa mwanzo mpya. Huwa ni vipindi vya hofu na mivutano... Lakini mwisho wa siku wema hutawala. Na wakati mwingine pale ambapo kuna uwezekano wa watu 'kuinuka' hapo hapo pia kuna wezekano la 'anguko'.

Nadharia za njama zilizopohapa kwa sasa si bahati mbaya; hizo kulinganishwa na yale yaliyosemwa na baadhi wa 'maona' wa zamani kuhusu nyakati za mwisho nayo pia si makosa... Lakini siyo yote yaliyosemwa lazima kubakia hivyo hivyo katika 'wavu' wa wakati. Matukio katika nyakati zote mbele na nyuma yanaweza kuhandisiwa. Mtu yeyote awezaye kusoma mambo ya nyakati afanya hivyo kwa 'uhakika' moja tu wenye kufungamana na nukta fulani ya kuona jambo... Ulimwengu daima unawezesha hata yale yanayotarajika kutokea kutotokea... NI siri fulani ambayo ina kina-- labda nacho ni kisichokuwa na mwisho katika mwelekeo huo. Kwa kuwa ulimwengu nao hauna mwanzo wala mwisho--mwisho unaweza kuwa mwanzo na mwanzo kuwa ni mwisho. Ayasemayo mwanadamu si lazima ulimwengu kufuatisha bali mwanadamu anakirimika ANAPOTAKA HASA kujua yote, hata mafumbo ya 'mungu'.

Hebu tuvinjari sura ya leo: tazama video ijayo na kiungo cha hapa chini

Embedded media from this media site is no longer available

Halafu unaweza kutazama 'Zeitgist Film' ilikupata mitizamo zaidi ya binadamu na mikingamo yake dhidi ya kujitambua.

Upendo
 
Kutoka: Mwongozo hai kuelekea Uhuru Halisi seh. IV

Husimulika kwenye simulizi la 'mwanzo' jinsi mwanamke alivyodanganyika na 'nyoka'... Husemwa katika kisa: nyoka alimfuata mwanamke akamwambia: eti, umeambiwa usile matunda ya 'mti wa katikati'? Naye mwanamke kwa haiba yake yake ya kitoto kuhakiki hivyo na kubayanisha zaidi angalizo la ada ya 'mauti' itakayojiri endapo watakula. Lakini nyoka akamwambia kama vile kusema--kula tunda kutawapa ujuzi wa mema na mabaya na wao watakuwa kama mungu na hilo ndiyo wamezugwa... Naye mwanamke akaja kuyaona matunda ya mti wa katikati ni yenye kufurahisha na kupendeza 'machoni' akayachuma na kuyala na kumpa na mwenzie mwanaume wakala wote... Ndipo ghafla wote wakajishtukia wapo uchi... wakaona aibu.

Kisa cha mwanamke ni kielelezo cha ukweli mmoja kuhusu fahamu za mwanadamu. Wanawake wako karibu sana na maumbile yao kuliko jinsi walivyo wanaume. Na hivi wanawake pia wapo karibu na mazingira na kuvutika kupendezwa na faraja zake. Na ndivyo hivyo hivyo wanawake wamefanyika juu ya miili yao; mwanaume ni mtu ambaye jinsi ya kwanza ya 'kumjua' mwanamke ni kwa misukumo ya udadisi. Mfanyiko wa mwanamke kimaumbile huzidi mashauri yake yote yenye jinsi ya 'unyoofu' ulio ni kawaida ya nidhamu yake kiakili. Mwili wa mwanamke hujibainisha na ule wa kiume kwa maumbo yake yenye mviringo, na hali mwanaume ni mwenye maumbo nyoofu. Amkaribiapo mwanamke, mwaume udadisi wake huweza kuchukua sura ya kugusa na kupapasa kwa kuwa jinsi hivyo hutafuta kuaarifika na 'siri' za umbo la mwanamke... Lakini mwanawake wanajinsi tofauti ya akili ifanyavyokazi inayojitofautisha na jinsi ya kiume. Wanawake ni watu saikolojia ya undani kwa kuanzia; na wanaweza kubakia hivyo maisha yao yote. Mwanamke asiyejua mume toka kuzaliwa kwa mfano, ikiwa hataingiliwa na misukumo ya milazimisho toka nje anaweza kubaki ni bikira maisha yake yote na wale yeye asione ajabu. Kwa kuwa wanawake ni wenye kujifurahisha mawazo na ndoto zao za ndani na hata kuzimwagilia na kustahimilisha ndani ya tumbo hilo hilo la ndoto. Ndoto za mwanamke zisipoingiliwa na kukatishwa zinaweza kubakia ni uwezekano tu. Na ndivyo ndoto za mwanamke 'hukamilishwa' na 'nia' kutoka nje ili zijekuzaa matunda. Ni kama vile katika simulizi ya kisa cha Binti mfalme aliyelala usingizi kusubiri busu la mwanamfalme ili aaamke na kufanya harusi yenye mwanzo wa furaha ya milele kufuatia. Na ndivyo wanaume hufanyika kwa saikolojia ya nje ambayo ndiyo hasa hudhahirisha 'nia';-- ya kupanda vilima na kushuka mabonde, kukata vichaka na kutandua bui bui walioizunguka kasri; kuingia ndani na kumkuta binti mfalme mzuri aliyelala usingizi; kumbusu na nakujikuta ndiyo kamwamsha.

Lakini nia bila mwongozo haiwezi kuzaa matunda. Mwanaume ni mpofu kujua ni wapi pa kulenga katika mwili wa mwanamke ili kukamilisha 'maarifa' yake. Kugusa pekee yake hakutoshi na mwanaume kwa jinsi hii kusemwa, huanza udadisi kwa jinsi ya kuhangaika na kuchezea maumbile tu. Lakini kitendo mbadala hufanyika katika mwanamke. Mwili wa mwanamke ni mwili uliojaa na moto wa msisimuko kote katika mwili wake. Mwanamke anao uwezo wa 'kujisikia' kwa kila kitu juu ya mwili wake, na huo hafundishwi kwa maana 'upo damuni'. Na hivi inaweza hata kusemeka mwanamke ndiye mvumbuzi wa msisimuko wa mwili na hata kutambua kitovu cha hisia zote kuwezekana kusisimuka zipo mahala karibu na uvungu wa kiuno chake. Na hili huwa hata bayana wa watoto wadogo... Watoto wa kike huanza kujua nguvu ya viungo vyao uzazi mapema kabla ya wale wakiume. Jamii hukemea tabia za watoto kujigusa gusa sehemu hizo kitendo ambacho 'hushtuwa' watoto na kuanza kuwajengea dhamira ya hatia na aibu. Hii ni kwa kuwa binadamu mwenyewe hana busara ya kushughulika vema na nguvu za maumbile na hata yale ya uzazi.

Basi hii ndiyo kusema ni mwanamke aliyemuongoza mwaume kulijua tendo la kujamiiana na si vinginevyo katika picha ya mienendo. Wote wawili yumkini hawakutambua wanachofanya lakini pale kitendo hicho kilipokamilika ndipo tahamaki ya aibu ikawaingia kwani 'kujua' vilele vya kutaniko la kimwili daima ni mapinduzi makubwa kimwili, kiakili na kiroho kwa mtu mume na mtu mke. Hupelekea kung'amua 'ubinadamu' wao katika muktadha wa vitu vyote vinavyowazunguka; na ndivyo hufuatia kutambua shauri la uzazi, kuwajibika na ustawi kwa 'nguvu' ya jasho lao.

Kisa cha mwanamke aliyedanganyika bustanini ni kisa cha binadamu wote. Ni jinsi ya kike katika 'utofahamu kumbaizi' wa akili za binadamu wote ambao huchochewa ubinadamu ili avuke daraja lake na nia na utashi. Nyoka ambaye ni ishara ya werevu wa ulimwengu wote mzima wa madhahirisho ambao huchochea binadamu kutahamaki maumbile na ufungamano wa utamu wake ama muonekano wake na jinsi zake. Mtoto awapo mdogo yeye yu hajui kuwa ipo siku moja yeye atakuwa ni 'mtu mzima'. Kwa yeye ataudhania utu uzima kwa jinsi yake ya utoto. Katika uzima wote wa maisha yapo mazingira ambayo husukuma watu kuachana na 'utoto' wao lakini hapo hapo huwatupa katika uwanja wa mapambano na maalimwengu. Mazingira hayo ni sehemu ya msingi wa mpango wote mzima wa 'Uzima' kwani pasipo hayo kungesingekuwa na 'kukomaa'. Pia 'wakati' katika ndoto si sawa na wakati katika 'kukomaa' na ndivyo daima katika maisha kuna nyoka mwenye kushawishi mwanadamu ajaribu kuuingia ulimwengu wa 'nyakati thabiti' na aachane na utete wa mawazo. Naye binadamu huuingia ulimwengu wa 'wakati thabiti' kwa aibu ya yale 'mambo ya utoto' na kuzitenda kazi ili kumfaa 'nia' yake thabiti na si ndoto za alinacha. Utoto ni muhimu kwani kwa huo binadamu huweza hudhanifu hata yale 'makuu' yasiyowekana mara moja; lakini ingelikuweje ikiwa binadamu huanza kwa mawazo ya moja kwa moja ya 'vipimo' na 'kiasi'?

Basi si 'Mwanamke' kama ichukulivyo na kusomwa juu juu katika visa kama hivi ndiye 'aliyekosea'; ubinadamu wote unakosea wakati wote pale unapoanguka katika majaribu kwa visa vyote vyenye vya kufungamana na 'wakati' na hata raha zake kwa minajili ya matamanio; na ndivyo Ouroboros huwa ni nyoka mwenye kufukuzia kuung'ata mkia wake yeye mwenyewe. Na kwa muktadha mwingine ndivyo hukutwa picha ya Ouroboros ikizungushia kati picha nyingine za kitoto kichanga kikichezea fuvu la kichwa cha mwanadamu. Ni kielelezo cha uzazi, uchanga na mauti ndani ya milele yote ya ubinadamu.

Kufa na kuzaliwa tena kwa ubinadamu hushikiliwa na mhimili wa mwanamke ama jinsi ya kutunga na kudhahirisha maumbo yote ndani ya nyakati. Na hapo ndiko twajifunzako mambo mawili yahusuyo uhai—ustahimilishaji na uponyaji katika muktadha wa sifakazi itambulikayo kama UPENDO.

Pale ambapo pana 'muundo wa daraja la nia' pana uwezekano wa mkirimiko wa jinsi ya nishati iwezezayo kukirimisha ustahimilishaji na uponyaji wa mienendo ya kiuhai. Nishati hii ni Upendo; na ni yenye jinsi yake maalum yakuonekana kujifungamanishia ndani yake usifa-akili wa mawezekano yote katika ulimwengu. Huu nguvu zake huhuisha tu vile vyenye mpangalio maalum wa ndani yake ili kuwa 'hai'; vile vile hudhahirisha sura za 'mgando' wa maumbile mengine.

Mpangilio wenye mawezekano ya kushikilia maumbo yote katika sura zake 'hai' na zile za 'mgando' ni Upendo ule wenye kufutika maumbo yote yaliyodhahirika. Palipo na usafi wa kuyabayanisha mawili haya--namna ya Pumzi ya Uzima hudhirisha utukufu wake katika mienendo ulio pia ni utukufu wa usifa-akili uliyofanyikia ulimwengu wote kwa nyakati zote. Ndivyo hiyo pia huitwa ni 'Pumzi Takatifu'. Ipo kote na mote lakini utambuzi wa mwanadamu kwa wakati unaweza kutomaizi ukweli wake dhahiri. Pumzi Takatifu ndiyo huleta utangamano wa vitu vyote vya jinsi ya nchi na mbingu kwa mawimbi yake ya Uzima.

DNA ni 'muundo wa daraja la nia' na hivi ndani yake upo uwezo wa kukirimika na mawimbi ya uzima kama ule unaostahimilisha mienendo yote ya Dunia, Mwezi, Jua, Nyota na Mbingu. Habari zijazo na haya mawimbi ndiyo huongoza mienendo yote ya uhai kwa seli husika na kwa jinsi ya mapana ya sura yake; na vile vile panapo dosari yoyote katika maumbile uhai yanayoathiri msimamo wa mustakhabari wa seli, mawimbi ya uzima ni 'Tiba' ya kurekebisha mpotoko wa mienendo. Mienendo yote ya shughuli katika seli za uhai ni jinsi ya mawimbi na hivi ile dhana ya 'urefu wa wimbi' inaingia pia katika mashauri. Penye 'urefu wa wimbi' na hapo hapo jinsi ya kutaka kutanabahi kasi ya mitetemo, panahitaji la kizio cha 'wakati' ili kukadirisha na kutofautisha jinsi ya mawimbi tofauti ikiwa twataka kufanya kisomo cha kuendana na 'vipimo' na 'viasi'. Lakini kwenye seli na hata mkusanyiko wa seli wenye kuja kuunda kiumbe kizima mienendo yake yenye kutokana na jinsi ya mawimbi mengi yafanyayokazi kwa wakati mmoja; hayo hufanya hivyo kwa jinsi tuiitayo ni utangamano. Ikiwa miendendo ya shughuli mbalimbali katika seli yapaswa kuchangamana na kuchanganyika mwongozo maalum wa 'mizunguko' ya vitendo hukidhi kufanya 'vizio' vya nyakati katika viumbe hai. Na hivi miili ya viumbe hai kama mwanadamu kwa mfano; ni jinsi ya mchangamamo na mchanganyiko wa 'mizunguko' ya namna nyingi ya vitendo, mingine ikiwa midogo midogo na mingine mikubwa mikubwa yote hiyo kutosha kumdhahirisha mwanadamu 'mzima'.

Ipo athari moja katika uono wa macho ambayo hutumika katika ubunifu ufundi wa kihandisi kujenga vyombo vya umeme kama luninga na redio. Vyote hivi viwili ni vyenye kutumia kanuni za mawimbi kutenda 'miujiza kamili' ya utumikivu wa ufundi wa mambo. Mawimbi yenye kusaidia mwanadamu kuchakatisha 'habari' akilini ni yenye jinsi ya 'upana' sana kuliko yale yanayoweza kuchakatishwa na umeme kwa tabia zake. Umeme huishia kuweza kupitishwa katika vitu yabisi ama vimiminika lakini huo huo pia unaweza 'kunyongorotwa' na 'kunyooshwa' katika mzunguko wake wa 'kutiririka' kutoa 'mawimbi'. Mawimbi hayo yanaweza kubayanishwa kama 'kiasi' na 'mwelekeo' katika mzunguko wa mtiririko kwa umeme uitwao ni 'sakiti'. Basi katika sakiti, kidude kinachofahamika kama 'koili' ni jinsi ya mnyongoroto wa kipitisho umeme kama waya; na kile kidude kifahamikacho kama 'kapasita' nacho ndiyo hasa kinachofanyakazi kama 'nguvu za radi' zirushavyo 'cheche za moto' kati ya usawa mmoja hadi mwingine. Na kapasita ndicho ambacho ndani yake kimetengenezwa kama 'nyuso' mbili za vibati vyenye kuweza kupitisha umeme vikiwavimetenganishwa na 'utupu' uliojazwa hewa au kijikaratasi kilichotiwa nta au kimiminika chumvi chumvi nk ili mradi hivyo vyote huwa na jinsi tofauti ya uwezo 'kuhifadhi' zile 'cheche za moto'. Kwa kuwa kapasita hutokana neno la kiingereza lenye maana ya 'chenye unafasi wa kuweza kubeba'--capacitor. 'Koili' hutokana na neno la kiingereza lenye maana ya mnyongoroto—coil.

Umeme ni namna ya 'nishati' yenye jinsi mbili kwa wakati mmoja—'jinsi ya maji' na 'jinsi ya moto'. Vidude vya utundu wa kucheza na umeme ndivyo hutumika kulingana na tabia hizi mbili umeme kwa kadri itakiwavyo. Basi 'jinsi ya maji' ndiyo ina ugani wake wa mashauri ya 'Umeme Mtiririko' na jinsi ya moto ina ugani wake wa 'Umeme Simamivu' . Jinsi ya maji hutaja 'elektroni' katika uwianishi wa vipimo na mashauri; na wakati jinsi ya moto hutaja 'chaji' katika uwianishi wa namna ile ile. Si lazima mashauri ya chaji, elektroni na hata umeme wenyewe kuwa sawa kabisa 'kiudhanifu picha' na vile basi inavyosemekana katika taaluma yenyewe ya umeme; lakini ni bora kuyaelewa na kuyatambua mazingira yake ya mpangilio wa vitendo na matokeo.

Utundu na uchunguzi umeleta ujuzi, na hivi katika sayansi; umeme umeleta mapinduzi ya kutoka ule uwanja wa maarifa peke yake hadi kuja kuwa maarifa na ufundi.

Kutoka jinsi ya kidude kimoja kimoja katika kuunda sakiti za umeme ili kutoa matokeo yaliyosanifiwa; ujuzi na ubunifu umeleta mbele usanifu shindilivu kimuundo kutegemeana na ubora na pia uvumbuzi wa namna mbalimbali za vipitisho vya umeme. Mapinduzi makubwa ya usanifu na ufundi yamekuja na maendeleo ya kuvumbuka na kutumika kwa 'vipitisho nusu' vya umeme katika kubuni vyombo ya utumikivu wa kiumeme. Haya mapinduzi ndiyo yamezaa ulimwengu wa 'uelektronishi' kama sayansi ya udhibiti mwendo wa elektroni kwa kutumia vipitisho nusu vya umeme.

Vipitisho nusu vya umeme ni vile vidude vinavyoweza kutengenezwa jinsi yake hata katika nafasi finyu sana na huku vikileta matokeo yanayokidhi utumikivu wa umeme—katika mashauri ya muktadha wa kiingereza hutajwa ni 'semi-conductor' devices. Hivi ni vile vyenye tabia ya kuweza kupisha umeme katika mazingira fulani na hapo hapo kuwa na uwezo wa kutokupitisha umeme katika mazingira tofauti. Mazingira hayo inaweza kuwa halijoto inayokizunguka kidude hicho ama 'mweleko' wa mkondo wa umeme ikiwa vinatumika njiani katika sakiti ya umeme. Mara nyingine 'namna ya miale ya mwangaza' huathiri hadhi ya tabia zake vile pia mfano wa hata miale isiyoonekana kwa macho lakini ya jinsi wa mwangaza wa kawaida kama vile katika kidhibiti kazi za chombo tokea mbali—remote control. Vidude hivi kwa maumbo yenyewe hasa ni vyenye jinsi isiyo ya chuma ila kuwa kama tu mawe yalivyo. Na ndiyo jinsi ya mawe katika sura ya mchanga huwa kuwa ni malighafi katika kuundia sakiti za elektronia kwa hata sura iliyojifinya sana nafasi. Sura hii yenye kujifinya nafasi ndiyo hufahamika kama 'Sakiti Jumuizi'--integrated circuit, IC ambapo usanifu wa muundiko wake hughairisha ulazima wa kutumika kwa jinsi ya moja moja; kwa vidude vingi vya aina ya 'kikinzaji'--resistor, 'dayodi'--Diode, 'Tranzista'--Transistor na jamii zingine zote za jinsi ya dayodi, tranzista ikiwemo na kapasita katika mazingira yasiyo mapana. Sakati Jumuizi ndiyo ile huonekana kama kashata nyeusi za mstatili ama mraba yenye vijimeno vingi katika pande zake mbili ama zote nne. Vijimeno hivi wakati mwingine hukunjwa kuwa 'miguu' na kushikizwa na chuma laini ya risasi katika vimbao vya kiuelektronishi.

Dayodi ni kidude chenye hadhi ya kuweza kuruhusu mwelekeo mmoja wa mtiririko wa umeme na Tranzista ni kidude chenye hadhi ya kukutanisha sakiti mbili za umeme na kuatharisha mitiririko ya umeme kushahibiana kote kote. Kidude hichi basi ndiyo pekee huwa na miguu mitatu lakini kisicho namna ya sakiti jumuizi. Hivi ndiyo jamii ya vidude katika ulimwengu wa elektronia vinavyofanya kuwepo kwa uwezekano wa 'ukuzaji' wa 'viasi vya mawimbi' ili kuwezesha sifa kama vile kutoka kwa sauti iliyokuzwa kupitia spika toka kwenye kipokelewo cha sauti—maikrofoni na amplifaya na halafu basi vile vile kuweza kurekebisha ukubwa wake kwa ufundi mwingine unaohususha labda kuzungusha 'fungulio' la sauti ama kubonyeza mahala.

Ni muhimu kufahamu mashauri ya uelektronishi ili kuielewa fizikia iliyofanyiwa kazi na vile vile kutangamanisha visomo vya maumbo. Na toka kwenye mashauri haya tunasogea mbele na kumbukumbu la 'uwezekano wa ukuzaji wa mawimbi' kifizikia, lilio ni shauri la msingi wa tranzista; na basi kubakiza 'ufanyaji wa mawimbi' katika sakiti na utumikivu wake.

Sakiti inayofanywa kwa vidude viwili vilivyo ni koili na kapasita ikitiwa moto wa umeme 'hutetemesha' kiasi cha umeme na mkondo ndani yake. Kasi ya mtetemo ni mpishano wa 'kiasi' cha nguvu ya umeme utendekao kati ya koili na kapasita. Kadri nguvu iongozekavyo katika kapasita kwa mfano; itakuwa ni kioo cha mteremko wa nguvu katika koili. Kinyume chake pia ni sawa—kuongezeka kwa nguvu katika koili ni kuteremka kwa nguvu katika kapasita. Basi ndivyo hivi viwili hujifanyia ncha mbili za vilele vya nguvu—kimoja kinapokuwa juu sana ndiyo wakati huo ho kingine huwa chini sana. Kwa jinsi hiyo hii nguvu huwa ni pumzi itayodumisha mapokezano ya kuhamishiana nguvu mpaka pale pumzi 'itakapokauka'. Kwa kawaida pumzi ya umeme hukauka ikiwa sakiti ya koili na kapasita haitastahimilishwa kwa mfululizo wa 'moto'. Na ndiyo maana uelektronishi huhitaji umeme endelevu katika sakiti kwa kuwa vidude vinavyoweza kubaki na moto kwa kitambo fulani ni koili na kapasita tu. Na hivi pia siyo kusema 'vinaweza kutoa nguvu' la hasha. Umeme unaweza kusukuma sakiti ya koili na kapasita na jinsi nyingine ya vitu kama vidude mbalimbali vya kiuelektronishi na sakiti jumuizi ambavyo vyote kwa pamoja vinavyoweza kutumia umeme kudhahirisha kazi.

Kasi ya mitetemo ya nguvu za umeme katika sakiti ya koili na kapasita daima huwa ni ile ile na haijalishi ni kiasi gani cha moto wa umeme kimetumika 'kutekenya' mwenendo wake. Hii ni sifa madhubuti inayoleta uhakika wa mawimbi yanayotarajiwa kufanyiwa kazi ili kufanikisha lengo la hata kusafirishwa mbali. Na sakiti ya koili na kapasita pia huitwa ni 'sakiti ya utetemeazi' kwa kuwa huweza kutekenyana na nyingine iliyo nje yake. Utetemeazi ni tabia ya kimaumbo ambapo kitu kimoja chenye kutetema chaweza kuambikiza kingine kutetema ikiwa kuna mshahibiano wa maumbile na vipimo kwa namna maalum. Ni jinsi ambavyo waya mbili zilizokazwa huweza kuambukizana mitetemo ikiwa mmoja utakung'utwa kupigwa. Maana ile ambayo haikukung'utwa ikisogezwa karibu na ile iliyokung'utwa huanza pia kutetema na kutoa sauti kwa jinsi yake. Basi sakiti ya utetemeazi ndiyo ile katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'resonant circuit'.

Mawasiliano ya kimawimbi husaidiwa uwezekano wake kwa sifakazi ya sakiti ya utetemeazi kwa pande zote mbili; ile yenye kurusha mawimbi na ile yenye kupokea mawimbi. Katika mazingira ya uwezekano, sakiti ya utetemezi itafaa 'kurusha mawimbi' pale kasi ya mitetemo yake itakapofikia kiasi fulani ikadirishayo kwa kutajwa ni frikwensi ya kurushika. Maji, hewa na anga vina mpitisho wake wa mawimbi wenye kuanzia na viasi tofauti vya frikwensi. Frikwensi ya mawimbi inayokidhi masafa ya kurushwa hewani ndiyo kuchanganywa na habari ili hiyo ipokelewe inakotegwa kunaswa. Mawimbi yaliyobebeshewa habari yanaponaswa huchujwa kiuelektronishi ili kuibakiza habari inayotakiwa.

Katika kurusha habari ni frikwensi moja tu inayotumika kwa habari na hivyo sakiti ya utetemeazihutumika kupanga masafa ya marusho pasipo haja ya kurekebisha-rekebisha kiasi cha frikwensi. Katika mapokezi ya mawimbi sakiti ya utetemeazi huwa na namna ya kuweza kurekebishika ili kunasa mawimbi mbalimbali wakati hata wakati. Hili huwezekana kwa kurekebisha upana wa zile 'nyuso' zinazotazamana katika kapasita; kwani kadri nyuso mbili za kapasita zinaposanifiwa kusogea kama vile kisu cha kukunja kinavyoweza kukunjua visu vyake mbali mbali na huku havigusani yenyewe kapasita itapelekea utetemeazi tofauti kwa kadri ya ukubwa wa utazamano wa nyuso. Kusanifu hivyo kapasita ni rahisi kuliko 'kuzidisha' ama 'kupunguza' minyongoroto ya koili ambako pia kunapelekea uwezekano ule ule. Lakini tekinolojia ya kisasa huweza kufanikisha kitendo cha kubadili frikwensi katika sakiti ya utetemeazi kwa kutumia aina ya kapasita iliyo ni jinsi ya dayodi kwa hapo hapo; ambayo kwa kadri ya nguvu ya umeme uliounganishiwa moja kwa moja kwa hiyo--hufanya 'namna ya mwanya/pengo' katikati ya namna mbili za vipitisho nusu vya umeme vinavyoifanya hiyo. Basi badala ya kuzungusha ili kurekebisha frikwensi, jinsi ya umeme unaoongezwa ngazi kwa ngazi unaweza kufanikisha kile kile kwani huo umeme husababisha mgandamizo wenye kudhibiti 'upana' wa pengo na hivyo tena--hatautetemeazi waweza kuhama kutoka uwezekano wa frikwensi moja hadi ingine. Hii ndiyo hutumika katika vyombo vya kiuelektronishi vya leo kama redio za simu za mikononi, ama jinsi zote za udhibiti wa kubonyeza... Jinsi hii ya kurekebisha mdako wa mawimbi ndiyo huenda kwa jina la 'mrekebisho uliosanifika unamba' kwa kuwa ufundi huu umetokana na ufundi wa kudhibiti tabia za sakiti kwa 'Uelektronishi wa Jinsi ya Namba'. Basi mrekebisho ulisanifika unamba ndiyo ule katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'Digitally Synthesised Tuner'. Uelektronishi wa Jinsi ya Namba hutajwa ni 'Digital Electronics'.

Na sasa tuukague ulimwengu wa mawimbi na habari.

Sauti au picha haviwezi kutumwa hewani kitekinolojia pasipo utumikivu wa mawimbi. Kwa bahati nzuri sauti nayo ni mitetemo na hivi yaweza kuchanganya na mitetemo ya kiumeme na kurushwa hewani kama kitu kimoja. Hili linafanikiwa kiurahisi kwa kuwa sauti inaweza kufua umeme wenye jinsi ya mawimbi kwa mitetemo yake juu ya chombo maalum kinachofahamika kama maikrofoni. Pia zipo aina za maikrofoni ambazo zitumikapo kama kidude cha ukinzani katika sakiti ya umeme; basi ukinzani waweza kutetema kadri sawa na sauti inayoangukia juu ya kiwambo chake chenye kutetemeshwa na sauti. Hili linafanya mkondo wa umeme katika sakiti kubadilika kushahibiana na mitetemo ya sauti na basi nguvu za umeme zinaweza kugemwa kama mawimbi ya kiumeme.

Mawimbi ya kiumeme huchanganywa na frikwensi toka katika sakiti ya utetemeazi katika sakiti nyingine maalum ya 'umodutulishi'--mchakato wa kuchanganya habari mawimbi na mawimbi ya kurushia hewani. umodutulishi hutoa zao la mawimbi yaliyo tayari kwa marusho; yenye hadhi ya aidha 'umodutulishi kimo' au 'umodutulishi frikwensi'. Katika umodutulishi kimo ndiyo wimbi la marusho hutetema hewani kote na huku 'ukali' wake ukinepa kwa kadri ya mitetemo wa mawimbi ya ile habari hasa. Pale mawimbi haya yapokelewapo ule mnepo huengulia na kuchakatuliwa ili kubaki mawimbi ya kiumeme yenye kukuzwa na kuendesha vyombo vininge vya kielektronishi ili kugezwa habari kamili nje chombo chenyewe na kwa hadhira kupitia spika.

Jinsi hii ndiyo katika redio hukutwa skeli ya mitabendi ya 'AM'--kwani hili huwakilisha 'Amplitude Modulation'. Kwa upande wa umodutulishi frikwensi mnepo hufanyika katika 'kasi' ya mtetemo wa 'frikwensi ya marusho' ambayo yaweza kunepeshwa kwa kiasi chake na hali mawimbi yakapokeleka nasakiti mtetemezi iliyotegeshwa kufaa katika wigo wa masafa ya 'FM'--kwani hii huwakilisha 'Frequency Modulation'. Basi kwa kawaida wigo wa masafa ya umodutulishi frikwensi hufanyika katika mitetemo ya kasi zaidi kuliko ile inayotumika katika umodutulishi wa kimo. Katika nadharia za mawasiliano, kadri mitetemo ya kasi inavyotumika ndivyo 'habari' inavyoweza kubebwa kwa 'ufanisi' zaidi na pia ubora. Umoditshi wa frikwensi si tu unawezesha marusho wa matangazo bora kwa sauti, iwe muziki ama vinginevyo; lakini pia unatija kwa 'weupe' wa dosari. Hiii ni kwa kuwa katika jinsi hii ya mawasiliano mwingiliano wa 'makelele' yenye kuweza kuchafua habari moja kwa moja hakuna. Kwenye umodutulishi wa kimo habari inaweza 'kuchafuliwa' na kelele zitokanazo milipuko ya cheche ama mashine zenye kutumia umeme zinaweza kuwa karibu na chombo pokelevu cha mawimbi. Basi ndivyo wigo wa masafa wa 'FM' ndiyo hutumika zaidi kwenye matangazo ya idhaa za burudani na taarifa kuliko 'AM'. Vile vile jinsi hiyo hiyo ya umodutulishi wa frikwensi ukifanyika kwa jinsi ya 'uelektronishi wa unamba'; huleta 'Mawasiliano ya unamba' yaliyo ni bora kuwezesha hata mawasiliano ya simu za viganjani na pia mikonga ya simu yenye kuenenda kwa mawasiliano ya angani.

Kuwezesha mawasiliano ya picha na sauti mchanganyiko wa jinsi zote mbili za umodutulishi hutumika kwa wakati lakini katika wigo wa masafa ya juu zaidi ya kimawimbi yenye kuja kurushwa hewani ili kuwezesha namna ya habari nyingi kutumwa kwa mfungasho mmoja. Kila uzi wa habari, tuuite 'sigino' hutiwa kwa nafasi ndani ya mtiririko wa mawimbi wenye jinsi ya kiarifu cha 'ufungu' wa habari. Kiarifu hichi ni alama ambayo katika kupokewa kwa mawimbi ya habari, ule uzi wa habari—sigino utakadirisha mafungu yake yenye kujumishia 'habari' ya picha na pia sauti katika kipindi cha muda mfupi mfupi sana. Basi hiyo alama ndiyo huarifu mwanzo na mwisho wa fungu la taarifa; ambao kwa jinsi yake hushaibiana mfumo wa picha katika luninga. Sigino ya habari hutangamanishwa na sigino ya kutengeneza picha katika kioo cha luninga kwa kiarifu cha umuda. Mchakato huu ndiyo jinsi hufahamika ni usikronizi wa mienendo.

Ni katika hadhi ya usikronizi twatanabahi jinsi ya kisomo muhimu sana katika ushahibishaji wa mienendo. Tekinolojia inafanya 'miujiza kamili' ya ajabu sana kwa ufundi wa usikronizi wa mienendo katika minajili ya wakati. Pasipo huu mawasiliano ni muhari. Si tu katika uelektronishi ndipo tunamaizi uwezekano wa hadhi za usikronizi lakini ni ukweli uliobayana kuwa mienendo hata ya shughuli za seli katika mwili huwezekana kwa jinsi ya usikronizi wa michakato yake. Mpokezano wa majira huitwa nirithimu; na mpangilio jinsi ya shughuli zote za uhai wa seli hufuatisha 'rithimu' ambavyo pia ni kusemakujisikronizia na vipindi vya majira. Ili jinsi ya mawimbi na majira katika mwili ndiyo hufahamika kama 'rithimu ya kidaiyurini'--diurnal rhythms. Panapo mzunguko wa vitendo na majira kama vile usiku na mchana pana rithimu ya kidaiyurini.

Basi ndivyo hata uwezekano wa kusafirisha picha kwa ajili ya luninga katika mawimbi ya kiumeme hewani husanifiwa. Ili picha itengenezwe kuonekana katika kioo cha luninga huwa kunamzunguko wa uchororaji wa picha. Kitendo hichi hufanyika haraka sana kuliko macho yanavyoweza kumaizi uchoraji huo ukitendeka hata atazamapo kioo cha luninga. Na ndipo katika shauri hili tunajifunza finomena ya kipekee sana katika mwili wa mwanadamu. Kinyume na inavyoweza kudhanika katika hali ya kawaida na tena ile ya watu wengi; fahamu za kuona kwa macho za mtu si ni endelevu katika utanabahifu. Fahamu kama 'kugusa' ni ya karibia papo kwa hapo; vivyo hivyo kwa harufu puani, na kuonja ulimini--kwa kuwa hizi zote huendana kwa jinsi ya 'mguso' baina ya vipokezi vya taarifa za kimwili na mazingira chochezi yanayouzunguka mwili. Lakini tujapo kwenye kuona na kusikia; kitu tofauti hutendeka katika muktadha wa kuchakatisha 'habari'. Ni kupitia macho na masikio ndipo mtu hupokea 'uzi wa habari' na hivyo ili kumaizi hiyo mchakato hufanyika katika ubongo wake ili kuengua 'habari' kutoka kwenye mwanga ama sauti wenye kubebea ndani yake habari. Kisomo cha uchakatishi wa taarifa na 'uenguaji' wa habari ndani ya viumbe hai ndiyo hufanyika katika ugani wa kisayansi katika mashauri ya 'sibanetia'.

Vipokeo vyote vya taarifa na habari katika mwili wa viumbe hai kama mwanadamu huratibiwa na ubongo katika uchakatishaji bainifu. Habari haiwi habari mpaka kuwepo na rejea ya kumbukumbu ya mashauri sehemu fulani katika uratibu wa ubongo. Kumbukumbu haiwezekaniki ila tu kwa uwepo na uwezekano wa 'nia' kuchukua mkondo ili kurahisisha finomena ya 'kuandika' kinachopokelewa kama habari ili kuwa kumbukumbu yenye kufaa manufaa ya rejea. Basi ndani ya mwanadamu kwa mfano, ipo nia inayomwezesha yeye kukusudia 'kunakili' habari na pia ipo 'nia' ndani yake inayohifadhi kila kitu kinachoendelea hata kama mtu mwenyewe hakusudii hivyo moja kwa moja. Ufahamu jua nafahamu mbalali ndiyo uwanja wa mchezo wa nia za jinsi zote mbili. Ndivyo hivi ufahamu jua unaweza kufananishwa na sehemu ya bonge la barafu iliyo upande wa juu wa bahari na wakati huo huo fahamu mbalali ndiyo ule upande uliozama ndani ya bahari—bahari ya utofahamu kumbaizi. Juu ya uso bahari ndiyo hufanya ufahamu jua kumbaizi. Barafu ndiyo basi ugani wa upeo maizifu wa mtu kwa wakati katika madhahirisho. Na hapa ndipo pana dalili ya kuwa ipo sehemu katika utambuzi wa binadamu na viumbe vyote ulioungana; huo si mwingine ila muktadha wa utofahamu kumbaizi ndani ya 'wakati' na hapo hapo 'ufahamu jua kumbaizi' nje ya wakati.

Basi na huo ubongo kwa ile jinsi ya upande wa kushoto na na ile ya kulia ndivyo kupitia usikronizi wa 'habari' hutafsiriwa ama kutiwa alama za uhifadhiko wa kimakusudi katika akili ya mtu; kwa jinsi isiyofahamika sana katika mashauri ya saikolojia ya juu juu ya miongoni mwa wanataaluma wa leo, kila kitu katika maisha yote ya mtu hunakilika mahala palipofichika nje na 'nia' yake ya kawaida. Lakini je, taarifa huingiaje katika ubongo wa mwanadamu?

Sauti hushabihishwa na kumbukumbu za sauti ili kumaizi habari na hili huwezekana kwa kusoma 'sahihi' ya mawimbi ya sauti yenye mfananio wa kumbukumbu fulani. Kila kinachosikika nje husikishwa tena kwa jinsi ya ndani ya ubongo ili kuleta 'utambuzi'. Ni kitendo kinachohusisha usikronizi wa habari yenyewe na kwa upande mwingine hapo hapo 'usimyulizi' wa mfananiko wa taswira sauti katika ule mchakato wa 'kuita' kumbukumbu. Usimyulizi ni kuibua taswira ya mfano itakayozimua mwangaza wa kuteka jinsi kama hiyo hiyo ya picha kama ipo katika wigo wa kumbukumbu za fahamu jua ya mtu mwenyewe. Huko ndiko huleta 'kujua' katika akili na utambuzi wa jambo. Basi ndivyo hivyo mtu akumbushwaye kitu kilichosahaulikia mbali hutajiwa visifa-sifa vya jambo ili 'aunde picha' na ikiwa hivyo visifa vinakidhi haja atagutuka na vile kana kusema anhaaa! Kumbe ni ~... Usimyulizi ni kuunda kadiri ya mfananio wowote wa kitendo ama picha kwa makusudio maalum ya kubashiri uwezekano wa uhalisia wa jambo usio wa hapo hapo. Ndiyo katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni muktadha wa 'Simulation'.

Jinsi hiyo hiyo ya uitaji wa kumbukumbu hutendeka ili kutafsiri picha itokanayo na macho ya mtu. Lakini katika macho uono huja kwa kukusanya taarifa za jinsi ya seli moja moja nyingi zipatikanazo ndani ya goroli la jicho, juu ya ngozi ya uso wa ndani kwa kila jicho na tena kutazamana kimwelekeo na mwingio wa nuru machoni—paitwapo retina. Ubongo ndio huunganisha taarifa moja moja ya kila seli ili kudhanisha taswira ya kile kilichoinngia katika uono wa macho. Lakini hapa ndipo hasa pakugusia tena hadhi ya usikronizi. Seli za uono katika macho, huwahazisomomi picha endelevu kama ambavyo ni rahisi kudhania; seli za uono huona picha kwa 'kubakia' na taarifa kwa kitambo fulani. Kitambo hichi ni kifupi mno ijapohali kipo katika uhalisia wa mchakato wa kuona. Macho 'huona upya' kadri ya kila baada ya '1/25 ya sekunde'. Na ukweli huu ndiyo hutumika kuendesha sifakazi ya kuchora picha katika vioo vya luninga ama vile vya kompyuta. Picha katika vioo huchorwa kwa mpangilio wa mafungu yaitwayo fremu na hizo hurushwa kwa kasi ya fremu 25 kwa sekunde ama zaidi kufaa uonaji wa watu. Kwenye vyombo kama kompyuta, kulingana na matumizi ya kinachotazamwa na ubora unaotakiwa; kasi ya kuchora picha inaweza kuongezwa kwa kuchagua frikwensi ya kuanza upya kwa picha ambayo huja na jina la 'Refresh Rate' katika mpangilio wa mchakato wa kuonekanishia picha.

Basi ndiyo mawimbi ya kiumeme hewani hubeba 'uzi wa habari' na kiarifu cha mwanzo wa mafungu ya picha ili kufanikisha usikronizi wa fremu ya kwanza hadi ya mwisho kwa kila sekunde inayokatiza katika kupokea 'taarifa' katika luninga. Katika 'mawasiliano ya unamba' taarifa zaidi zinaweza kufungamanishiwa na mtiririko wa habari juu ya idadi ya fremu kwa sekunde, mwanzo na mwisho wa mafungu yake, sauti na hata zingine zenye kuweza kutafsiriwa katika king'amuzi cha mawimbi na habari kilicho mahususi.

Katika ufundi wa kutetemesha uzi wa mawimbi ya habari kwa matangazo ya kiluninga tunajambo moja muhimu la kufahamu pia. Pamoja na rangi zote zionekazo katika luninga, ukweli ni kwamba ni rangi tatu tu--nyekundu, kijani na bluu; ndizo zenye kuakisika katika sigino--uzi wa mawimbi, na mitetemo yake ya marusho ya mawimbi ya kiumeme. Na halafu 'fremu za picha' ndani ya sigino si chochote ila mzunguko kamili wa mistari inayochorwa kutoka kona moja ya fremu kwa juu kushoto, mwendo wa kutoka kushoto hadi kulia katika ulalo wa mapana ya mstatili; halafu kurukia chini mstari unaofuata kwa jinsi hiyo hiyo na tena na tena hadi mstari wa mwisho wenye kukamilisha fremu moja. Fremu inayofuatia ni mzunguko huo huo wa kuanza juu kabisa kushoto na kuishia chini kabisa kulia. Hii hufanyika hivyo hivyo kwa jinsi ya zile rangi tatu kwa jinsi inayoendana nukta kwa nukta na huku kila ya hiyo moja ina taarifa yake yenyewe. Kwa ajili ya manufaa ya ufundi wa usikronizi, fremu zote zinaviwango sawa vya idadi ya mistari na uwiano wa mapana na marefu ya mstatili yanayotambulika kusanifiwa utendaji wa vyombo vya kiuelektronishi; pia kwa viwango vya taifa moja hadi lingine kwa minajili ya kuchagua. Luninga za kisasa hata hivyo zinauwezo wa kutambua jinsi sigino ilivyo na kujibadilisha ufanyaji kazi wake ili ziweze kuchora picha katika vioo vyake ikiwa uwiano wa mstatili si sawa na uwiano unaokuja na fremu za picha katika sigino. Ndivyo hivyo huweza 'kukata' sehemu ya juu na ya chini ili picha ienee katika mstatili wake mpana; ama kufanya mstatili mdogo ndani ya kioo chake ikiwa uwiano wa fremu toka kwenye sigino ni wa mstatili mpana vile basi kufanya picha iliyoendelea katikati ya utepe mweusi wa juu na chini.

Ni muhimu kujua jambo kuhusu rangi hizi tatu yaani nyekundu, kijani na bluu. Hizi ndizo zile zenyekutajwa ni rangi za msingi. Kutokana na hizi; rangi zote zenye kudhihirika machoni zaweza kufanyika. Hizi ndizo zile rangi tatu ambazo zikiwakilishwa kwa miduara mitatu inayoingiliana utaniko wake basi huleta rangi zile rangi Saba za upinde wa mvua--katika zile sehemu za maingiliano ya nafasi. Picha nzima ya rangi katika kioo cha luninga inaweza kufanyika kutokana na kuchanganya mmuliko wa chembe tatu tatu katika utenganisho wa vijinukta vingi vilivyopangiliwa katika kiwambo cha picha. Kila chembe ikiwakilisha mwanga aidha wa nyekundu, kijani na bluu. Katika luninga za kizamani, zile zenye jinsi ya chogo, uelektronishi wake unategemea ufundi wa kumulika chembe hizo tatu tatu kwa jinsi ya 'bunduki' inayolenga 'risasi' chembe moja kati ya tatu kulingana na nguvu ya habari ijayokudhahirisha sehemu ya picha kamili; jinsi kama ni aidha, nyekundu, kijani ama bluu. Bunduki zote tatu hulenga hizo chenye kwa mwendo uliosikronizishwa na hivyo ndiyo vile kuchora ile mistari ya kutokea upande wa juu kushoto hadi upande wa chini kulia. Bunduki ni jinsi ya kurunzi inayomulika jinsi ya miale nyoofu kuelekea kwenye kila chembe yenye kuwakilisha moja ya rangi tatu. Hizo chembe huwa ni aina ya madini ambayo yakimulikwa na miale ya namna hiyo yenyewe huwaka mwanga aidha wa nyekundu, kijani ama bluu kulingana na yalivyofanyika—madhini ya fosfa nyekundu, fosfa ya kijani na ile ya kibluu. Miale hiyo kuitwa ni miale ya 'elektroni' lakini hivyo ni kwa kuwa ufundi wake wa kuisababisha kutokea huwa unahusu kuunguza waya katika kila bunduki iliyoko nyuma kabisa ya lile chupa kubwa-- ambalo ndiyo hasa limtungi linaloleta chogo la kioo cha luninga; na halafu ikiwa jinsi ya umeme mkali sana unaokuzwa na kidude kiitacho 'busta' utapandikizwa kati ya ncha mbili moja ni yenye kugusana na waya wenyewe unaoungua na ncha nyingine kuwa ni ule uso wote unaoshikilia chembe za rangi, basi ndiyo miale hiyo huonekana kana 'kusafiri' kutoka kwenye bunduki hadi kwenye hizo chembe za rangi. Nazo hizo chembe za rangi zina sifa moja mahsusi, mara tu zilengwapo na miale ya hiyo miale zenyewe huwaka mwanga hapo hapo. Ni ajabu lakini kweli kwamba kuwaka na kuzima huko kuendenako na miale inayolenga na huku ikisogea kutoka upande wa juu kushoto hadi upande wa chini kulia kuikamilisha fremu moja ya picha—katika kiono cha mtu anayetazama luninga hutafsiri kama ni picha halisi na wala si vipande vipande vya 'vimulimuli'. Haya ni matunda ya usikronizi na kasi ya kitendo chenyewe katika mizunguko yake ya vitendo na tena kwa muda mfupi kwa macho kutotambua.

Katika luninga za kisasa—luninga bapa, kiwambo cha mchoreko wa picha kinachofanya kioo cha luninga huwa na jinsi ile ile ya chembe tatu tatu lakini zenyewe si chembe yabisi mfano wa madini ya fosfa katika kupangiliwa kwake ndani ya mistari inayokamilisha mfanyiko wa fremu. Badala yake huwa ni vidimbwi vilivyo katwa vizuri katika miraba miraba halafu ndani yake kukawekwa 'vimiminika kriyisto'—chembe-mawe maji. Kriyisto ni jinsi ya muundiko wa kimaada wenye sura ya mgando kama wa jiwe na tabia zake zote uang'avu na 'ukioo' wa jinsi ya kupitisha mwanga na vile basi uakisivu. Chumvi--dawa ya jiko ni kriyisto; huwa na ung'aavu lakini ukioo wa wake haupitishi mwanga. Chumvi huweza kuyeyuka katika vimiminika kama maji. Vimimibiko tofauti huleta hadhi na kadiri tofauti ya 'uyeyuko' na ndiyo hufanya upana wake mahsusi wa mashauri ya kisomo cha chumvi katika kemia na fizikia. Ni katika utaaluma wa uelektronishi ndimo mashauri ya kifizikia ya chumvi na hasa kuhusishwa na mwanga hutumika kiufundi wa kusanifu matumiko ya kikazi.

Ni tabia ya baadhi ya vimiminika kriyisto kupitisha mwanga ama kutopitisha mwanga pale viunganishwapo kiumeme na umeme katika hali ya mkondo geu wa kasi fulani. Kasi hiyo ya ugeugeu wa mwelekeo wa mkondo wa umeme kati ya ncha mbili; nayo pia huwa na kizio cha ufrikwensi. Hii ni kama ilivyokatika zile saa za mkononi ambazo huchora maandishi ya majira ya wakati kwa 'wino mweusi'. Ule 'wino mweusi' ni kimiminika kriyisto ambacho kikiunganishwa na frikwensi kadhaa ya kiumeme basi hugeuka kukinga mwanga usipite kabisa. Kiwambo chenye kubeba vimifereji vyenye kuunda picha ya maandishi kikiwekwa juu ya uso wa jinsi ya kioo akisivu kufaa, pale vimifereji hivyo vikingapo mwanga kutokufika katika kioo kutafanya mtazamaji aone kama 'wino mweusi' wa maandishi. Basi ndivyo hivyo hivyo katika viwambo vya picha katika luninga bapa huwa na jinsi ya 'chujio' kwa mwanga wenye kutoka ili kuonekana katika kioo cha luninga; kufanywa hivyo kwa matumiko ya vimiminika kriyisto. Chembe zote katika hali ya moja moja, hufanyika kwa chujio yake inayoruhusu mwanga kutoka ama kutokutoka kwa muktadha wa rangi zote tatu katika kila kimraba. Kuwashwa na kuzimwa ni zao la usikronizi unaoendesha mpangilio wa hivyo hivyo kwa kioo chote katika kukamilisha kila fremu ya picha. Mwanga wa vinukta vyekundu, kijani ama bluu waweza kutokea kwa kichujio na kurunzi kwa rangi hizo kutokana na mwanga mweupe uwakao wakati wote nyuma kabisa ya kiwambo cha picha kwa jinsi ya muakisiko wa taa za pembeni kioo chenyewe—isivyodhahiri lakini katika picha ya nje ya kioo cha luninga. Vinukta vinavyofanikisha utokeo wa rangi huboreshwa ufanisi kwa kuwa ni sehemu ya 'Filimu-Tranzista Nyembamba' na pia 'Dayodi Itoayo Mwanga' ambavyo ndiyo hufanikisha kitendo cha kuwasha ama kuzima kwa mwanga na muktadha wote mzima wa usikronizi unaoendana na uelektronishi wa unamba.

Basi ndiyo hivi kwa sanaa na tekinolojia, leo hii kuna hata vyombo vya kiuelektronishi vinavyobebeka na kuhamishika kiurahisi vyenye 'kioo cha picha za rangi' kuanzia simu za viganjani, saa za mkononi, gemu za kiuelektronishi, vidude kama IPOD nk. Hivi yote hufanyika kwa kujumuishia ndani yake tekinolojia za vioo-picha jinsi ya 'vimiminika kriyisto'-- kutajwa kama 'Liquid Crystal Display' kwenye maelezo juu ya makasha, muktadha wa lugha ya kigeni. Katika kiingereza, mashauri ya uelektronishi miongoni mwa wazungumzaji wa lugha hiyo hutaja kwa ufupi 'TFT LCD' kuwakilisha 'Thin Film Transistor Liquid Crystal Display' ilivyo tuseme ni Kioo picha cha vimiminika kriyisto katika muktadha wa 'Filimu-Tranzista Nyembamba'. Pale ufundi unapohusisha Dayodi Itoayo Mwanga ni ndiyo mashauri ya kiingereza hutaja na pia 'LED'--Light Emitting Diode.

Kama ilivyokatika kuonesha picha, mchakato kama huo huo hudhahirika katika 'uchukuaji wa picha' toka kwenye jicho la kamera. Picha inayopita kwenye lensi ili kurekebisha umbali na mapana ya picha kuchujwa mara tatu kwa wakati mmoja ili kupata jinsi tatu za fremu zenye kunakili rangi nyekundu, kijani na kibluu. Fremu hizi hundwa kwa chembe ndogo ndogo ya 'Kidude cha ncha za kuunganishwa kwa chaji' ambavyo hufanywa kwa uelektronishi wenye kuhusisha tabia za kapasita na papo hapo jinsi moja ya rajisi rahisi ya mtungiko wa chaji ndani ya upahala panapoweza 'kusomwa' hivyo kiuelektronishi. Chaji ambayo huweza 'kuyeyuka' pale mahala itungikapo kwa kusababisha mkondo wa umeme ndani ya sakiti; hiyo yafanyika mahala palipo ni kama ule 'uwazi' kati ya nyuso mbili za kapasita ama kiwambo kisichopitisha umeme kati hizo--kisipitisho. Ndivyo hivyo kapasita pia ni kidude kinachoweza 'kuhifadhi' nguvu za umeme; maana ikiwa chaji imejazwa katika hiyo hubaki humo mpaka sakiti iiunduliwe kukamilisha njia ya mzunguko wa umeme, na hapo ndipo umeme utatiririka mpaka chaji iishe. Katika vile kidude cha ncha za kuunganishwa na chaji, namna ya kitako cha madini ya silikoni iliyotoneshewa kidogo elementi za boroni, huwambwa juu yake kwa utando wa kampaundi ya silikoni daioksaidi (SiO2, kimfanyiko wa molekyuli). Juu ya utando huo ndio kushikamanishwa na vipitisho vitatu vya umeme vyenye kutumika na zoezi la kuchakatisha 'uzi wa habari' kwa kadri ya ukali wa umeme unaojitokeza kutokana na chaji zinazojitengeneza katika kitako cha Silikoni iliyotoneshewa boroni kulingana na mwanga unaoangukia kila chembe moja ya kidude cha ncha za kuunganishwa kwa chaji na hasa kitakoni pake. Katika mashauri ya kiingereza kidude cha ncha za kuunganishwa kwa chaji ndicho hutajwa kwa jina la 'Charge-coupled Device'--CCD na kile kiwambo kilicho ni 'kisipitisho' cha kiumeme hutajwa ni 'dielectric'.

Mpangilio wa 'CCD' ndiyo huchakatishwa kwa jinsi ya usikronizi ili kuutengeza 'uzi wa habari' utakaotiririshwa kama mawimbi ya kiumeme hadi kungine mbali ama kuhifadhiwa kiuelektronishi. Kwa kuwa usikronizi kama kitendo cha kujitengemea huendana na uchakatuzi wa muda na vipande vya taarifa, ni muhimu pia kufahamu 'ukamilifu' wa 'mapatio kamili' ya 'kung'amulia' taarifa toka kwenye taarifa inayopokelewa. Kwanza kabisa ni kusema kipo kiwango maalum kwa vizio vya wakati baina ya urushaji na upokeaji. Vizio hivi huandamishwa kwa frikwensi za 'kung'amulia' taarifa ambavyo ndiyo hasa majira ya uwakati; pia huitwa ni kasi ya saa. Ikiwa kwa mfano sampuli ya uzi wa habari imesikronizika kasi ya saa kadri ya 'kilohetzi moja' basi wakati wa kupokea habari itang'amuliwa toka kwenye taarifa ikiwa kasi ya saa kuchakatisha kukomboa habari nayo ni 'kilohetzi moja' kamili. Kinachobakia ni ile tu ishara ya kutambua mwazo na mwisho wa kila sampuli ya uzi wa habari utiririkao. Ndivyo hivi mawasiliano yote huchukua sura yake okiondoa pekee yake matangazo ya radio ambayo huwa si yale yenye jinsi ya usampuli wa uzi wa habari. Matangazo ya redio huwa na usampuli wa uzi wa habari ikiwa mawimbi yake ya kiumeme yameambatanishiwa 'taarifa za ziada' kama ilivyo siku hizi katika matangazo ya wigo wa masafa ya mitabendi za 'FM' huweza kufungamanishiwa na taarifa za jina la kituo na taarifa nyingine fupi fupi kwa wakati. Katika matangazo ya Redio ama Luninga ya jinsi ya mawasiliano ya unamba haya huendana na usampuli wa uzi wa habari wakati wote.

Kiuelektronishi, 'mapatio kamili' ya kasi ya usampuli kwa uzi wa habari hutokana na maboresho yasakiti ya utetemeazi kwa kufungamanishwa na tabia ya mitetemo ya kriyisto yabisi maalum. Madini kama ya 'Kwatzi', ni kriyisto yenye tabia ya 'kutetemesha' mkondo wa umeme(pasipo kujali ukubwa wa mgandamizo wa kiumeme) kwa kasi ya frikwesi iliyo ni moja daima. Sifa hii ndiyo inayofanya madini haya kutumika kote penye umuhimu wa ukadirisho wa kasi ya saa katika kuchakatisha ung'amuzi wa habari. Hivyo daima kriyisto ya kwatzi itakutwa kwenye vyombo vya kurusha, vyombo vya kupokea na vyombo vyote vyenye kuendana na uchakatuzi wa sampuli za uzi wa habari. Pia kwenye vyombo vyote vya kiuelektronishi vinavyohusisha saa na namna ya uratibu kwa rajisi ya wakati. Kriyisto ya Kwatzi hutumika hata kwa ukubwa wa chembe ndogo sana kwa muonekano lakini kukidhi mahitaji. Sakiti ya utetemezi yenye ile kasi yake ya 'mtetemo asilia' iliyo ni sawa na ule mtetemo asilia wa kwatzi kuchakatishwa pamoja kiufundi ili kuhakikisha kugemeka kwa kasi ya mitetemo isiyoyumba kabisa na hivyo kufaa sana kwa shughuli mbalimbali za kiuelektronishi. Mitetemo asilia ya sakiti ya utetemezi haitoshi kukidhi uthabiti wa kasi ya saa ifaayo shughuli mbalimbali.

Mawasiliano angani ni jiwe la msingi katika hatua za ustawi na maendeleo ya mwanadamu. Ni ishara ya mengine mengi yatakayofuatia na hata kubadilisha sura ya jamii yote na mustakhabari wake. Si tu kimawasiliano na uchukuzi peke yake bali pia katika muktadha wa unyambuliko wa kiutu.

Maendeleo makubwa ya ulimwengu wa leo wa habari ni matunda ya 'uelektronishi wa kimawasiliano'; na katika huu tunashuhudia mwanzo wa mwanadamu 'kuvuna' mawezekano yaliyo katika uwazi wa nafasi na mbingu. Kutuma ujumbe/habari hata mahala pa mbali na hivi pia kuletewa 'habari' yoyote yenye mapenzi mema ndiyo mwanadamu--hata kabla ya huu uwezekano alipatwa na njozi na maono ya mfano wa 'malaika'. Yeye aliliona hili kwa jinsi ya mtu mwenye mbawa, arukaye hata mbawa na hivi mwenye kuzidi kadiri za umbali na kasi ilikutokea. Na yeye alilichukulia hili kama mfadhiliko kwa ujumbe kati ya mtu na Mungu na kwa nia njema. Lakini hii pia ni akitipu muhimu kuelewa jinsi ilivyojichimbia ndani sana ya fahamu mbalali iliyozama kwa kiasi chake ndani ya utofahamu kumbaizi. Kutoka katika utofahamu kumbaizi, fahamu mbalali ya mwanadamu ilipitisha 'ujumbe' kwa 'fahamu jua' ya mtu iliyowakilishwa kwa sura ya 'mtokezo wa malaika'. Malaika ni daraja ambalo binadamu vile vile amepata ufunuo wa hata yale yasiyokuwepo katika jamii yake kufahamika.

Binadamu hana uwezo wa kumaizi ukweli ulio ni dhahania mno; na hivi ufunguko wake hufanyika kuja kwa muktadha wa namna ya kipekee. Wakati mwingine huo huhitaji daraja lenye kumaizika sura ya upokezi wa 'taarifa/ujumbe/maaria' kuufaa 'ufahamu jua' wake. Ni kama vile kusema binadamu hawezi kuielewa lugha ngeni mpaka pale yale maneno ya lugha ngeni yamekuwa ndani ya fahamu yake kawaida ambayo ndiyo ufahamu jua. Ili kung'amua habari/ujumbe wowote kwa wakati binadamu hushughulika na upande wake wa ufahamu ulio ni ufahamu jua.

Uwezo wowote ambao unaweza kupitiliza ufahamu jua ili kung'amua habari; huo unaleta mashauri ya 'Paranomo' ya utambuzi kwa mwanadamu; huu pia ni uwezekano lakini usio wa kawaida sana miongoni mwa watu wengi; mara nyingine kujitokeza katika kulingana na mazingira fulani. Paranomo ndiyo yaweza kuhusisha hisia za kiakili zijitokezazo zaidi ya zile za milango ya kawaida ya fahamu kwa mtu na tena zenye kiasi chake cha usahihi kiutambuzi. Ufahamu jua katika hali ya kawaida hukamilisha kitendo cha utambuzi kwa kukutanisha hisia pokezi za kimwili, kumbukumbu na fikra/mashauri ya akilini. Paranomo hutanua hisia pokezi kutoka zile zilizomwilini mwa mtu na hata zaidi ya hizo—hali pia isivyo ni moja kwa moja.

Muktadha mintarafu paranomo unapohusisha ile jinsi ambavyo 'vifungu' ama 'uzi wa habari' ama pia namna ya ushawishi wenye kuweza kutoka kwenye wigo wa akili ya mtu mmoja hadi mazingira yake ya nje na kinyume chake pasipo zile jitihada za kimwili, kama vile kutamka na kutenda, ila tu kwa nguvu ya nia na akili tupu ndiyo ugani hasa wa chenye kuweza kutajwa ni 'Saikia'. Na vile vile yaweza kusemwa mambo ya Paranomo ni vipawa vya Saikia. Mawezekano ndani ya Saikia ya mwanadamu ni pamoja na kitendo chenyewe cha ufikirivu na utambuzi uendenao na kumbukumbu ama kuzidi mipaka ya kawaida na hivi kuhusisha ukionambali, usikiambali, uelewambali na uisharifu. Haya ndiyo katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'clairvoyance', 'clairaudience', 'clairsentience' na 'intuition'. Saikiakwa minajili ya vipawa vya akili ndiyo hutajwa katika mashauri ya kiingereza ni 'Psychic'. Msimamo mzima wa mtu kiakili kwa wakati ni Saikia ya mtu; 'Psyche' katika mashauri ya kiingereza.

Nuru ya Ufahamu, utambuzi na kumbukumbu ndiyo husokota nyuzi zote za msuko wa UTU na 'ujifahamuko'; ndani ya wigo wa Ufahamu Jua wa mtu. Utambuzi ni mfungamano wa Fikra na Hisia kwa kila urajisi wa neno ama tendo ndani ya Saikia ya mtu na kumbukumbu lake lote katika ufahamu jua—kwa nukta ya wakati wowote. Kwa kuwa hisia zote ni jinsi ya kimiminika kama ilivyo kwa 'maji'; fikra ni kama 'barafu' katika bahari ya ufahamu kamili. Kwa jinsi ya mchanganyo wa 'joto' na 'baridi' binadamu anaweza kufanya matone ya 'barafu' za mafikara. Nayo matone ya barafu yaweza kuja kufanya mabonge juu ya uso wa 'ujifahamu' wa mtu na pia chini; katika kuelea kwenye mapana ya bahari inayowezekanisha mabonge yote. Basi kwa mfano huu, ni miale ya Nuru ya Ufahamu yenye kumjalia mwanadamu uwezo wa 'kusababisha' hali ya joto ama baridi ili kurajisi jinsi ya mafikara yote katika madhahirisho katika utumikivu wa kumbukumbu lake na 'kujiona' katika kioo chake cha utu.

Kwa kadri mtu anavyojifahamu na kwa minajili ya kumbukumbu yeye atazidi kujisokotesha nyuzi za maisha yake kwa msingi wa mafikara yake. Maisha kwa jinsi yake; huakisi kile mtu akitendacho kwa matokeo yajayo kwa mujibu wa kanuni za maumbile. Kwa jinsi ya mizunguko na majira kila fikara ama neno ambalo mwanadamu hukirimu haja ili kudhahirika--kwa kukusudia ama kutokukusudia; hilo huja kuchukua sura kwa nguvu za kimaumbile. Kuna vile vitu ambavyo mwanadamu hupanda kwa nje kwenye mazingira yake na basi pale majira sahihi yanapowadia yeye huvuna kutokana na kile alichokipanda. Kuna vile ambavyo hata pasipo kutambua jinsi atendavyo nje ndivyo vile apandapo ndani katika ufahamu mbalali; hivi navyo hubaki kuwa ni ushawishi wa kichinichini utakaokuja kumtia mtu kwenye uwanja wa mavuno ya jinsi yake. Mawazo yote na mafikara ya mtu ni mbegu katika gurudumu la wakati. Majira sahihi yafikapo binadamu huvuna matokeo ya faida ama hasara kwa mawazo yake yote. Kwa kuwa mawazo ni vizio vya nia-utu kulingana na fikra na hisia za mtu mwenyewe; hivi ni kama vipande vya sumaku inayovuta ama kuvutika katika mazingira ya jinsi yake ili kufiti sura na maumbo.

Haba na haba hujaza kibaba ndiyo kanuni inayotawala misukumo ya mikondo midogo midogo kuweza kuunganika na kufanya msuko mmoja mkubwa na wenye nguvu ya jumla ya yote na mwelekeo mmoja uliodhahiri. Kila msukumo wa wazo ndani ya mwanadamu ni wenye kupanda hatia ama uhuru katika muktadha wa haki wa kanuni za maumbile. Wakati ndiyo huhukumu yote kwa nguvu zilizofanyikia katika maumbile yake na madhahirisho. Mkusanyiko wa mawazo ya jinsi ya uharibifu ama uharibiko yatamvuta mtu katika mazingira ya uharibifu na matunda yake. Mkusanyiko wa mawazo yenye ujenzi yatamsukuma mtu katika kiu ya kuunda na kutanua ustawi wake. Panapostahili stahili ujenzi binadamu akiwa na nia-utu iliyo ni mbegu ya mafikara mema atajaliwa kheri na maumbile na azma yake kutimizwa. Kulazimisha kujenga pale ambapo mazingira na wakati si sahihi binadamu atavuna taabu na kujihangaisha. Ujenzi hutaka werevu wa akili na utangamano wa maumbile na nyakati—siri yenyewe hasa majira na mizunguko iletwayo na 'Pumzi ya Uzima'. Binadamu akoseapo kanuni anaweza kusahihisha adha yoyote imsibuyo kwa kuendana na njia ya usikronizi wa mwendo wake na kanuni za kheri ya maumbile yote. Dosari ya makosa ya mwanadamu husahihishwa kwa nia safi na uongofu katika njia ya katikati yenye kheri kwa yote. Mwendo huu ndiyo utangamano wa nia-utu katika mtu na nia-uzima wa vyote. Dosari ya makosa kwa mwanadamu si hesabu kwa matendo yake bali ni upotofu wa nia yake kwa wakati na pia mshahara wa ubovu katika nia-utu wake kwenye mfichamo wa ufahamu mbalali wake.

Maumbile yote yamefanyika kwa hekima ya namna yake ambapo hakuna chochote kinachoweza kukimbia athari za matendo yake. Kadri mtu asababishavyo jitahada zozote matokeo humrudia kwa kadri ya stahiki za nguvu zake katika kitendo cha mgongano wa madhahirisho yote. Kuna yatendayo na matokeo yake huonekana kuja upesi ama kadri ya kusemama hapo hapo; na yale ambayo huleta athari za matokeo katika kusonga kwa vipindi. Hii yote ni kwa kuwa ulimwengu wote tuuona kwa macho ni tumbo la uzazi kwa hata yale yasiyodhahiri kwa ufahamu jua wetu kung'amua mara moja na hali pia tumbo hili hukirimu hata uwezekano wa mdhahiriko wa maumbo kwa mafikara yetu mabovu ndani yaufahamu mbalali. Yapo mambo yatokeayo katika jamii ambayo ni mavuno ya mtu mmoja mmoja na yapo ambayo ni mavuno ya kiukundi—ukijiji, ukimtaa, ukimji, uki-Jiji, utaifa. Pia yapo mambo ambayo ni mavuno kwa uanadamu wote duniani.

Hakuna mwanadamu asiye na kadri ya dosari inayomkutanisha yeye na wengine walioko katika mazingira yake ila ikiwa tu ameyatambua madeni yake katika makundi ya watu na kuweka nia ya kuyalipa na kuacha kulisha ubatili na upotofu wa kanuni zenye kheri ziongozazo madhahirisho yote.

Ndivyo 'Karma' imekuwa ikifundishwa katika mashauri ya dini nyingi kutoka mashariki. Kinachokwenda katika mzunguko hurudi; kinachopandwa huvunwa. Pia kuwa binadamu yuko kokote pale anapojikuta kuwapo kwa kuwa ana karma katika muktadha wa deni na hapo alipo. Na pia mtu huzaliwa pale ambapo msimu ni sahihi ili karma yake kuvunwa na majira na mazingira ya yale anayoyakuta mahali. Mtu huzaliwa mahala kwa kheri ama ubaya kwa kadri ya mbegu yake iliyofichamia katika ufahamu mbalali; ndani ya ufahamu mbalali pia kuna kumbukumbu hata kwa yale asiyomaizi kupata kuyatenda katika muktadha wa ufahamu jua wake. Na hivi kila nukta ya mwanadamu ni hukumu yake ikiwa hamaizi mbegu za nia-utu wake zichipukiazo kutokana na matendo aliyotenda kungine katika muktadha wa ufahamu mbalali. Mengi ya mawazo na fikra na usadikifu wa watu si 'mawazo mapya' kama wanavyoishi kujifahamu; bali ni fikra na mawazo waliyodumisha toka kungine hata nje ya wigo wa maisha yao wanaoujua. Na basi ni mpaka pale mwanadamu anavyokirimika kujua hata yale yaliyofichika ndani ya ufahamu mbalali wake ili aweze kubatilisha ushawishi wa uchafu wa mawazo yake hawezi kumaizi yeye 'Haki' iliyofanyikia ulimwengu wote. Haki hii ni hai na endelevu; si kama vile hasa ilivyopatwa kuzungumzwa kwamba husubiri siku fulani. Kwa kuwa watu wa zamani walifaa kwa mambo ya zamani na mashauri kuwafaa visomo vyao na mapana yao. Leo hii kisomo hiki hiki kinafunua mambo makuu zaidi na binadamu hana budi kutahayari upokeo wake kwa hekima kuu kuliko kumbukumbu lolote la maneno na masimulizi.

UHURU wa mtu ni kujinasua na kamba zote zinazomfunga mtu na mtu, pia mtu na mazingira hata katika muktadha wa ufahamu mbalali na mbegu zake za fikra-hisia kikumbukumbu. Lengo la mirengo ya kiroho kwa imani za kimashariki toka zamani ilikuwa ni kuupata huu Uhuru—Kisaikia, kimwili na kihisia; na ndivyo ilivyo hata kwa siku zote. Daima uhuru kamili huhusisha muktadha wa hata yale yaliyofichika toka kwenye upande wa nje wa ustawi wa wanadamu wote na tena jinsi ya mtu mmoja mmoja.

Ikiwa kwa muktadha wa mawazo na matamanio yake yeye mwenyewe mwanadamu hukirimika kuzaliwa mahala hata pasipo kumaizi kanuni zilizopelekea yeye kuzaliwa hapo; ni ishara ya kwamba yeye mtu si huru. Kila mwanadamu anawajibu wa kutafuta muktadha wa sababu za yeye kuzaliwa mahala; la sivyo yeye si mwenye kuwajibika na kweli ya ukirimiko wa uzima wake na ustawi wake pale alipo. Pia yeye hawezi kuwa huru na yale ambayo hajayashtukia kutawala majaliwa yake na hivi anakuwa 'mteja' wa usadikifu wowote usio ni hekima madhubuti ila mashauri ya mpito na ahueni. Kwa kadri anavyokirimika kutambua toka ndani, muktadha wa majaliwa yake kutokana na matendo yake yeye mwenyewe ndani ya nyakati za ndani na nje; kwa uzuri na pia ubaya yeye anao 'utashi' ambao ndiyo basi ngazi ya msingi kwa ukombozi wa mtu mwenyewe. Kwa kuwa kheri humshika mkono kumwongoza yule aliye na nia thabiti na uwajibikaji kwa jumla yote ya matokeo ya kazi zake. Mwanadamu ana kheri anapokiri makosa yake na kuyakubali kwa moyo wake wote na huku akiomba ndani ya 'roho' mwangaza wa wongofu kwa njia yake. Kwa saburi, maovu yote ya mtu husafishwa kwa moto wake wa nia safi na marekebisho ya dhamira katika mwendo wa safari yake yote mpaka pale atakapotakasika kabisa. Na hata atakasikapo mwanadamu anaweza kwa kupitia 'nia moja na Roho wa Uzima wote' kuchagua majaliwa yake kungine kokote katika msongo wa wakati na mahala—naam, hata kwa maisha mengine mbali na wigo wa maisha yake kipindi cha sasa.

Namna ya kumbukumbu inautumikivu kwa 'ukuwa' wa mtu katika muktadha wa nia na dhamira. Kumbukumbu ni kimvuli cha maarifa ya yote katika wakati wote na mawezekano yote. Ipo namna inayoweza kuleta shauri kuwa kila litendekalo katika majaliwa ya vitu vyote ndani ya nyakati ni sehemu ya uwezekano wenye kutathminika wa madhahirisho na maumbo yote hata kama ndani ya madhahirisho hayo kuna mkondo wa kuweza kuchagua baadhi ya maamuzi ndani ya viumbe vyenyewe. Kuna muktadha wa vitu kuwa kwamba vimepangwa na hali havijapangika kwa wakati huo huo -- kusema basi jumla ya yote huwa na sura dhahiri pale upana wa matukio unapotathminiwa. Hili katika ulimwengu wa fizikia ni huleta mashauri yenye nadharia za dhana ya kwamba 'haiwezekani kukadirisha mwendokasi na unafasi wa chembe zifanyazo tonadari ya maada' na hali tonadari yenyewe yaweza kutathminiwa hayo mawili katika uhalisia wake. Hili ni shauri la mfizikia Heisenberg--kwa mfano; na huitwa 'Kanuni ya Utohakika ya Heisenberg'.

Jinsi ya tabia na hadhi ya tonadari ni yenye kufanana kabisa na chembe msingi kwa utu na roho katika kufanyika kwa mwanadamu. Hivi ni vema kuyapitia mashauri yahusiyo muundiko wa chembe na chembe katika kuyafanya maumbo. Minajili ya utohakika wa kung'amua unafasi na kadiri ya mwendo kwa chembe zidhaniwazo kufanya tonadari ndiyo hiyo hiyo huweka ombwe katika utambuzi wa mwanadamu katika kudadavua 'kiini' cha uzima wake. Kwa mfano mtu aweza kusema kuwa kwake mtu ni 'hakika'; lakini je' iweje kuwa yeye ni mwenye kujimaizi ujitambuko wake na wakati mwingine asiwe hivyo? Nukta moja ya wakati mtu ni mzima na bukheri wa afya, wakati mwingine yeye yu mgonjwa na hajiwezi na tena zaidi wakti mwingine yeye ni mwenye kulala katika mauti na tena asije kumka tena... Kiini cha ujitambuo wa unafsi katika mwanadamu kitovu chake ni wapi hasa? Kwa maana ni hicho tu labda ndiyo 'hakika' yenyewe—hivyo basi mwili wenyewe usiwe ni hivyo. Ikiwa mtu huwa na 'utambuko' kwa kujimaizi nafsi yake ni nini sehemu ya kumbukumbu katika kujibainisha kwake hakika ya kuwa ni nafsi moja?

Kumbukumbu ya mambo na unafsi wake mtu japo yaweza kuwa ni 'kioo cha ujitambuo' yenyewe hiyo yaweza kabisa isiwe 'kweli' na wala 'hakika' yenyewe... Sasa kipi basi ni hakika? NI kawaida ya kuwa binadamu anayosilika ya kujibainisha 'ukuwa' wake kwa kumbukumbu la matendo yake lakini je, hili ni shauri la kweli ya utu wake kabisa kabisa? Yumkini kumbukumbu ina utumikivu wa kadri ya umuhimu kabisa katika ulimwengu wa madhahirisho lakini kumbukumbu yote ni 'usikweli'. Kadri ambavyo kumbukumbu ni usikweli lakini kubidi kukidhi haja ya 'ujitambuo wa mpito' basi hilo litakuwa wazi kuwa ni ile hali yenye kuwezeshwa na akili ya mtu mwenyewe yenye kufikiri na kuendesha mashauri ya wakati hadi wakati-- na pia iko sehemu ya akili ya mtu isiyo na sililka ya namna hiyo. Sehemu ya akili isiyo ni chombo cha mafikara ila tu sitaajabu ya 'mgundisho' wa tafsiri ya uwezekano wa mtu kujitambua; kwa minajili ya kumbukumbu lake na kwa jinsi ya 'kioo cha kujiona' tuuite ni 'akili ya juu' nayo hutenda kazi kwa mtindo tunaoweza kuuita ni 'dhahania'. Wazo tupu lililo ni mfano wa mbegu ni dhahania. Jinsi ya dhahania katika muktadha huu ni ile sura isiyo bayana ya jambo pana na hali yenyewe ni kama ule muhtasari mzima unaohifadhi ukweli wa lenye kujakufahamika vema baada ya vitendo vya kawaida vya matendo ya akili ya chini ya mtu kuchukua mkondo wa mizunguko wake wa mafikara na udadavuaji. Akili ya chini na ya juu ya mtu vyote kwa pamoja hufanya saikia ya mtu; nayo humuandama yeye kwa mapana yote ya kujitambua uzima wake.

Saikia ya mtu yeyote ni siri ya mafumbo kwa uelewa wa mtu nayo mazingira yake na hiyo huja kuzaa tathmini ya nidhamu ya mtu mwenyewe na nia yake. Upo uwezekano wa kutosheleza kusema kwamba-- Saikia ya watu wote, vitu vyote na uzima wote huwa na mahala ambapo hukutana ki 'maana na kheri' ya mienendo yote. Lakini katika muktadha wa dhahania binadamu kwa jinsi ya mtu mmoja mmoja, hukinga 'maji' kwa wakati mawezekano ya kujifafanua yeye wenyewe katika minajili ya majaliwa na mustakabari wake na hivi kuazimia mielekeo ya nia yake tokea kwenye mawezekano mapana zaidi ya dhahania ya utu na uzima wote.

Ili kutia hamasa ya 'ujitambuo' wa mtu, kumbukumbu la mtu humchochea yeye katika kuyabayanisha mapana ya kuchagua na kuamua mashauri ya 'utu' wake kulingana na mfululizo wa matendo yake na uhifadhiko wake katika maisha na mazingira aishiyo na kutokea kule atokeako. Nidhamu ya 'utu' ni kutaniko la mtu, mazingira yake na ung'amuzi wa mema ama mabaya katika kutanabahi ustawi wake yeye mwenyewe. Na hivi katika wanadamu wote kumbukumbu yaweza kuwa ni kimvuli cha kuegama na kinga kwa yale yasiyofahamika. Hapo hapo mwanadamu akusudiapo kutanua zaidi wigo wake ndivyo hata wigo wake wa kimvuli huongezeka. Mwanadamu daima yuko katika mapambano ya mazoea na yale mageni kwake. Mageni huweza kumletea hofu yeye lakini ikiwa mtu ni mwenye kushirikisha akili yake ya juu yeye aweza kushinda adha ya kumbukumbu na mashauri yenye kasumba na hivi huweza kuongozwa na dhahania katika kukabili mawazo mapya na wigo mpana zaidi wa maisha.

Akili ya chini ya mtu ni yenye kusumbuka na kumbukumbu na vina vya tafsiri dhidi ya utu wa mtu mwenyewe. Lipo daraja linalounganisha akili chini na ile ya juu ya mtu mhusika mmoja; wateosofia huita hili 'antakarana'. Uwezo wa mwanadamu kuzidi akili ya kawaida-- iliyo ni ile ya chini ni hafifu; na hivi ni katika mazingira maalum hutokea kwa mwanadamu kutumia mawezekano yaliyo katika akili ya juu. Na hivi wanadamu katika wingi wa idadi na silika ni wenye 'utambuo' mdogo wa yale yanayofanya saikia yao. Basi ndivyo hivi watu waweza kuwa watumwa wa mazoea yao duni na hafifu na hali wao wasione lolote lililopungua katika ustawi wao. Wale wote wanaoanza kuvuka daraja la antakarana daima wataonekana ni watu wa 'mashauri ya ajabu ajabu' na ufikirivu usio wa kawaida. Hawa ndiyo wale watu ambao huleta mabadiliko makubwa katika jamii zao hata kama jamii inayowazunguka haijaweza kwa wakati wake kuwatambua kwa matunda ya michanyato yao.

Moses Simon | Facebook
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom