Nyoka (The Divine Serpent)

Mycle255

New Member
Sep 15, 2021
2
2
NANI ATASIMULIA HADITHI YA SHETANI BAADA YA KUSIKIA UPANDE WA MUNGU?

SEHEMU YA PILI:

Screenshot_20220414-094847.png
Katika sehemu ya kaskazini ya Babilonia, HAWA alijulikana kuwa “Mungu wa Eden” (The Divine Lady of Eden) au “Mungu (wa Kike) wa Mti wa Uzima" (Goddess of the Tree of Life), wakikumbuka ibada ya Kiebrania ya Mungu (wa kike) wa mti, Asherah.

Moja ya vyeo vya HAWA kwenye Biblia ni “Mama wa Walio Hai Wote” (Mother of All Living) soma Mwanzo 3:20, hilo lilikuwa jina la kawaida la Mashariki ya Kati la Mungu wa Kike Mkuu aliyeumba vitu vyote kwa damu yake mwenyewe, katika karne nyingi kabla Miungu ya kiume haijafikiriwa. Waandishi wa Biblia huenda walisikia kuhusu Bustani ya Paradiso ya Mungu mwanamke, inayoitwa Heden katika fasihi Takatifu ya Uajemi. Bila shaka walimjua "Nin-Eveh", “The Holy Lady” ambaye Waashuru (Assyrians) walilitumia jina lake kuliita jiji lao kuu. Maandiko ya Waashuru (Assyrians) pia yalimwita “Mother-womb” wakimaanisha Muumbaji aliyeumba wanadamu wa kwanza kwa udongo, mwanamume na mwanamke pamoja, kama katika toleo la kwanza la hadithi ya Mwanzo (Genesis)

Kuna maandiko katika fasihi ya kale yanayodokeza kwamba HAWA ndiye aliyekuwa muumbaji na si Yahweh. Maandiko ya Kikristo ya ki-Gnostic yanaeleza kwamba Adamu aliumbwa kwa nguvu ya neno la HAWA, si la Mungu. Akasema, “Adamu, ishi! Inuka juu ya uso wa nchi!” akainuka na kufumbua macho. “Alipomwona HAWA alisema, ‘Utaitwa Mama wa walio hai, kwa sababu wewe ndiwe uliyenipa uhai.’”
Maandiko ya ki-Gnostic yalisema pia kwamba Yehova mwenyewe alikuwa mtoto wa HAWA, kwa kuwa HAWA aliishi kabla ya Miungu na ndiye aliyewazaa wote. HAWA alimpa Yehova baadhi ya nguvu zake za uumbaji, lakini Yehova akawa na kiburi na kusahau kwamba HAWA ndiye Mkuu kwake: “Yehova alikuwa na kiburi hata kwa Mama yake mwenyewe. Ilikuwa ni kwa sababu ya upumbavu na mjinga kwa Mama yake ndio maana alisema, "Mimi ni Mungu; hakuna mwingine ila mimi." (I am God; there is none beside me).
Maandishi ya ki-Gnostic mara zote huonyesha Mungu (muumbaji) kama mwanzilishi mwenye kiburi aliyekemewa na kuadhibiwa na mamlaka ya kike ambayo ni Kuu kuliko yeye.

Hadi leo bado kuna Sanamu ya Wakanaani inaonyesha Mungu wa kike wa kwanza akiumba binadamu wa kwanza (mwanaume), huku nyoka wake wawili wawili wakiwa kwenye mti wake Mtakatifu wa matunda na mmoja nyuma yake. Kutokana na utafsiri mbaya wa makusudi wa sanamu hizo, hadithi ya Mwanzo iliunganishwa pamoja. Biblia haisemi tunda la HAWA lilikuwa nini; lakini wachambuzi wa baadaye wa Ulaya walipendekeza kuwa lilikuwa Apple kwa sababu hadithi za Ulaya (za kale) zilimsifu Mungu wa Kike (wa kwanza) kwa kusitawisha ma-apple ya Ujuzi na Uzima katika bustani yake Takatifu.

Nyoka wa Hawa alikuwa kiumbe wa kwanza wa karibu wa Hawa na mfano halisi wa hekima yake, tangu watu walipoanza kuamini kuwa nyoka hawawezi kufa, kwa sababu anaweza kujitoa ngozi zao na "kuzaliwa upya."

Watu kipindi cha Neolithic (Final period of Stone Age)
10,000–4,500 BC huko Northern Europe waliamini kwamba nyoka na wanawake walikuwa na maajabu ya uhai yanayoohusiana na kuzaliwa upya. Hata katika nyakati za kihistoria, Wayahudi wa Gnostic waliabudu Mungu wao wa kale Nyoka chini ya jina la Nehushtan ambaye sanamu yake ya shaba ilitengenezwa na Musa, kulingana na (2 Wafalme 18:4), na kutumika kama chanzo cha uponyaji wa kiMungu. Hapo awali makabila ya Waebrania yalimheshimu nyoka, nahash, hadi wakati wa utawala wa Hezekia, ‘alipotupwa chini’ na ukuhani mpya.

Hadithi hiyo hiyo baadae ilichangia Wakristo wa zamani kumtaja Ibilisi kuwa “yule nyoka mkuu”. Kwa maoni ya waandishi kwamba Shetani alichukua mwili wa nyoka aliyezungumza na Hawa; lakini awali nyoka alikuwa ishara ya maisha (uhai).

Madhehebu ya Kikristo ya Ophite yaliabudu nyoka, baada ya kujifunza kwa Wagnostiki wa Kiyahudi ambao walitangaza kwamba Yehova wa baada ya kipindi cha mwisho wa uhamisho wa Babeli mwaka wa 538 K.K (Before Christ) hakuwa mungu bali ibilisi, ambaye alinyakua Ufalme wa awali wa Nyoka Mwenye Hekima. Nyoka aliabudiwa huko Palestina muda mrefu kabla ya Yahweh. Waebrania wa kwanza walichukua idea ya Mungu-nyoka aliyeheshimiwa na watu wa siku zao, na ukoo wao wa kikuhani wa Kiyahudi ukajulikana kuwa Levites (Walawi) yaani, Wana wa Lawi au "Leviathan", jina la Nyoka Mkuu.

Biblia inaonyesha kwamba Yehova alikuwa mpinzani na adui wa Mungu-nyoka, kwa kuwa walipigana wao kwa wao (soma Zaburi 74:14, 89:10, Isaya 51:9) na wangepigana pambano la mwisho siku ya Hukumu (maangamizi) kama Isaya 27:1 na Ufunuo 12 zinavyosema.

Hata hivyo mapokeo mengi ikiwa ni pamoja na yale ya kibiblia yanaonyesha nyoka kama mvumbuzi wa Maarifa ya mema na mabaya katika hadithi ya Mwanzo. Adamu na Hawa wangebaki wajinga bila habari za nyoka kuhusu Mti wa Maarifa. Masimulizi ya Kinostiki ya hadithi ya Edeni yalitumia maneno ya Kiaramu (Aramaic) yanayomtambulisha Hawa, Mwalimu na Nyoka (the Teacher and the Serpent); Hawah, “Mama wa Wote Walio Hai” (Mother of All Living); hawa, “kuelezeka” (to instruct); na hewya, “nyoka.”
Kwa Kiarabu, jina la Hawa la "Maisha," (Life) ni hayyat, sawa na jina la nyoka ni Hayyat pia.

Jina la Kiakadi (the Akkadian name) la Kuhani lilikuwa "snake handler” (mshika nyoka) au “snake charmer" (mvuta nyoka) na Mungu wao wa kike wa kwanza aliitwa "Mistress of Serpents" na vilevile "She Who Gives Life to the Dead" (Avipaye uhai vilivyokufa).

Mfumo wa kuabudu nyoka ilikuwa imeenea kote katika Eurasia wakati wa milenia mbili za kwanza kabla ya Kristo, ikiwezekana kuanzia India kwa mama nyoka (the great serpent-mother) aliyeitwa Ananta au huko Misri kwa Mungu Nyoka mwenye ujuzi wote aliyeitwa Mehen, kwa ishara ya hekima isiyo na kikomo ambaye ujuzi wake wa mambo yote ulionyeshwa na "Uraeus" takatifu iliyovaliwa kwenye paji la Isis. (Uraeus ni ishara ya kale ya Misri ya nyoka aliyefugwa (cobra). Uraeus huunganishwa mbele kabisa ya taji za Farao).

Ilikuwa inafaa, kwa nyoka kuwekwa kwenye Mti wa Maarifa wa kibiblia. Maandiko ya Kinostiki yaliwasifia Hawa na Nyoka kwa kuwapa wanadamu zawadi ya ujuzi, kinyume na mapenzi ya Mungu mkatili ambaye alitaka kuwafanya wasijue lolote. Wazo hili lilitokana na vyanzo vya kipagani kama vile Babylonian Epic of Gilgamesh, ambamo Miungu ilitaka kuwafanya watumwa wao (binadamu) wasijue kitu (ignorant) na kuwazuia wasipate uzima wa milele, wasije wakawa na furaha na kuharibiwa kwa ajili ya kazi ambayo Miungu ilitaka waifanye, ili kusaidia Miungu katika uvivu wao wa mbinguni.

Hisia za namna hiyo hiyo zinahusishwa na Mungu wa Biblia katika Mwanzo 22: “Bwana Mungu akasema, Tazama, mtu amekuwa kama mmoja WETU, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake, akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, na kuishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni. Neno la wingi “WETU” halikuchapishwa kimakosa. Wakati fulani ilirejelea wingi wa Miungu ya kike na ya kiume.
Ubinadamu wa Miungu wazee ilikuwa njia moja ya kudhoofisha ushawishi wao.

Huko Ugiriki mojawapo ya majina ya awali ya Mama wa kwanza wa "Wote Walio Hai" (Mother of All Living) lilikuwa Pandora, kwa Kigiriki "Mpaji wa Yote." (All-giver). Baadae waandishi wa waligeuza jina hili kuwa jina la mwanamke mfu ambaye ndiye aliyesababisha shida zote za ulimwengu, kama matokeo ya udadisi wake.

exemple-dessin-pour-tatouage-femme-infini-serpent-ananta.jpg
 
Back
Top Bottom