Nyoka/mdudu mwenye vichwa viwili

Nyoka/mdudu mwenye vichwa viwili

Nkwesa Makambo

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2011
Posts
4,763
Reaction score
1,320
Ndugu wana jamvi, jioni ya Leo nilishtushwa na kelele za watoto wakisema wameona nyoka mwenye vichwa viwili pasipo mkia.

Kwanza nilifikiri ni utani wa watoto, lakini baadae nikaamua kwenda kuangalia.
Japo nilikuta watoto wanamuua lakini nilithibitisha ni kweli pande mbili ni vichwa hana upande wenye mkia.

Kwa kweli Mimi ni mara ya kwanza kuona kitu cha aina hiyo.
Je ? Ni jambo la kawaida.

Wataalam wa Elimu ya viumbe mnaweza kutusaidia hii inakuwaje ?
Je ? Kwa kadri ya picha huyo ni nyoka kweli kama sio nyoka ni mdudu gani ?
 
Attachments

  • 1427041006829.jpg
    1427041006829.jpg
    70.3 KB · Views: 2,053
  • Thanks
Reactions: amu
Hao ndio wanaitwa ndumila-kuwili, na ndio kisa ata cha mtu mwenye nia mbilimbli kuitwa ilo jina Ndumilakuwili
 
Hahaa! Huyo ni mdudu jamii ya nyoka ila hana madhara. Sijui kwa kiswahili anaitwaje ila bukoba tunamuhita "kitabona izoba" kwa maana kwamba haoni.
 
Hao ndio wanaitwa ndumila-kuwili, na ndio kisa ata cha mtu mwenye nia mbilimbli kuitwa ilo jina Ndumilakuwili

Nilikuwa nafahamu uwepo wa neno ndumilakuwili lakini sikujua kama ni nyoka kweli. Asanteni wadau japo bado kiu ya kufahamu zaidi ninayo ili kujua kwamba ni aina kwa maana ya kundi maalumu la wadudu/nyoka au ni ulemavu katika wadudu / nyoka.
 
hahaa! Huyo ni mdudu jamii ya nyoka ila hana madhara. Sijui kwa kiswahili anaitwaje ila bukoba tunamuhita "kitabona izoba" kwa maana kwamba haoni.

Ni "mdudu jamii ya nyoka", kwa maana kwamba ni aina maalumu ya wadudu na vichwa viwili ndiyo sifa zao au sijakuelewa vema Mkuu ?
 
Kwa nini wanakua na vichwa viwili sijui

Ila wapo sana

Ukweli Leo ndiyo Mara yangu ya kwanza kuona wadudu wa aina hii, nimewahi sikia story za nyoka wa vichwa viwili lakini; wakiwa na mkia huku vichwa vikigawanyika Mara mbili...
 
Huyo sidhani kama ni nyoka ila itakuwa ni jamii fulani ya mdudu ambayo sisi hatuifahamu. Kwasababu tunajua nyoka ndiomaana naye tumemuinclude aj kumwita nyoka.
 
Hata mimi nilizani hivyo..
 
Hao wapo sana,ila wenyewe ni kama vile hawaoni na sidhani kama wanang'ata!
 
Ndugu wana jamvi, jioni ya Leo nilishtushwa na kelele za watoto wakisema wameona nyoka mwenye vichwa viwili pasipo mkia.
Kwanza nilifikiri ni utani wa watoto, lakini baadae nikaamua kwenda kuangalia.
Japo nilikuta watoto wanamuua lakini nilithibitisha ni kweli pande mbili ni vichwa hana upande wenye mkia.
Kwa kweli Mimi ni mara ya kwanza kuona kitu cha aina hiyo.
Je ? Ni jambo la kawaida
Wataalam wa Elimu ya viumbe mnaweza kutusaidia hii inakuwaje ?
Je ? Kwa kadri ya picha huyo ni nyoka kweli kama sio nyoka ni mdudu gani ?

Wapo mkuu na tabia zao kigeu geu kama dr.slaa
 
ni mdudu gani ?[/QUOTE]

WAKUU!!!
HUYO NI NYOKA,YUPO KWENYE KUNDI LA:BLIND SNAKES-(FAMILY TYHLOPIDAE)NA HANA VICHWA VIWILI KAMA TUNAVYODHANI!NYOKA HUYU NI KIPOFU NA SEHEMU YAKE YA MBELE INAFANANA SANA NA MKIANI SO HII IKAPELEKEA KUDHANI KWAMBA ANAVICHWA VIWILI.KUNA AINA ZAIDI YA 240 ZA NYOKA HUYU NA KWA E.AFRICA TUNA AINA23 IKIWA NI PAMOJA NA HUYU TUNAYEMJADILI HAPA.

NYOKA HUYU UISHI KWENYE MASHIMO YENYE UNDONGO LAINI NA KIPINDI CHA MVUA KAMA HIKI NDIO HUTOKA KWENYE MASHIMO MAANA MASHIMO HUJAA MAJI.
CHAKULA CHAKE NI WADUDU WARUKAO NA MCHWA PAMOJA NA LAVA(LARVAE).UNAWEZA NIULIZA CHOCHOTE KUHUSU NYOKA MAANA NDIYO FANI YANGU HASWAAAAA!!!
AHSANTENI KWA USHIRIKIANO!!!!
Kwa nini wanakua na vichwa viwili sijui

Ila wapo sana

Wapo huitwa ndumilakuwili.

hahaa! Huyo ni mdudu jamii ya nyoka ila hana madhara. Sijui kwa kiswahili anaitwaje ila bukoba tunamuhita "kitabona izoba" kwa maana kwamba haoni.

Huyo sidhani kama ni nyoka ila itakuwa ni jamii fulani ya mdudu ambayo sisi hatuifahamu. Kwasababu tunajua nyoka ndiomaana naye tumemuinclude aj kumwita nyoka.

Hao wapo sana,ila wenyewe ni kama vile hawaoni na sidhani kama wanang'ata!

Ndugu wana jamvi, jioni ya Leo nilishtushwa na kelele za watoto wakisema wameona nyoka mwenye vichwa viwili pasipo mkia.
Kwanza nilifikiri ni utani wa watoto, lakini baadae nikaamua kwenda kuangalia.
Japo nilikuta watoto wanamuua lakini nilithibitisha ni kweli pande mbili ni vichwa hana upande wenye mkia.
Kwa kweli Mimi ni mara ya kwanza kuona kitu cha aina hiyo.
Je ? Ni jambo la kawaida
Wataalam wa Elimu ya viumbe mnaweza kutusaidia hii inakuwaje ?
Je ? Kwa kadri ya picha huyo ni nyoka kweli kama sio nyoka ni mdudu gani ?
 
Hao wapo sana nilisha mkuta kwenye kundi la siafu. sijajua anauhusiano gani na siafu
 
ni mdudu gani ?

WAKUU!!!
HUYO NI NYOKA,YUPO KWENYE KUNDI LA:BLIND SNAKES-(FAMILY TYHLOPIDAE)NA HANA VICHWA VIWILI KAMA TUNAVYODHANI!NYOKA HUYU NI KIPOFU NA SEHEMU YAKE YA MBELE INAFANANA SANA NA MKIANI SO HII IKAPELEKEA KUDHANI KWAMBA ANAVICHWA VIWILI.KUNA AINA ZAIDI YA 240 ZA NYOKA HUYU NA KWA E.AFRICA TUNA AINA23 IKIWA NI PAMOJA NA HUYU TUNAYEMJADILI HAPA.

NYOKA HUYU UISHI KWENYE MASHIMO YENYE UNDONGO LAINI NA KIPINDI CHA MVUA KAMA HIKI NDIO HUTOKA KWENYE MASHIMO MAANA MASHIMO HUJAA MAJI.

CHAKULA CHAKE NI WADUDU WARUKAO NA MCHWA PAMOJA NA LAVA(LARVAE).UNAWEZA NIULIZA CHOCHOTE KUHUSU NYOKA MAANA NDIYO FANI YANGU HASWAAAAA!!!
AHSANTENI KWA USHIRIKIANO!!!![/QUOTE]

Nimefurahi sana kujua ndumilakuwili ni nyoka........nilidhani ni jina la kwenye Sani tu.......
sasa huyo mdau hapo juu kasema alimkuta kwenye siafu........ana uhusiano wowote na hao jamaa...........?.........
 
ni mdudu gani ?

WAKUU!!!
HUYO NI NYOKA,YUPO KWENYE KUNDI LA:BLIND SNAKES-(FAMILY TYHLOPIDAE)NA HANA VICHWA VIWILI KAMA TUNAVYODHANI!NYOKA HUYU NI KIPOFU NA SEHEMU YAKE YA MBELE INAFANANA SANA NA MKIANI SO HII IKAPELEKEA KUDHANI KWAMBA ANAVICHWA VIWILI.KUNA AINA ZAIDI YA 240 ZA NYOKA HUYU NA KWA E.AFRICA TUNA AINA23 IKIWA NI PAMOJA NA HUYU TUNAYEMJADILI HAPA.
NYOKA HUYU UISHI KWENYE MASHIMO YENYE UNDONGO LAINI NA KIPINDI CHA MVUA KAMA HIKI NDIO HUTOKA KWENYE MASHIMO MAANA MASHIMO HUJAA MAJI.
CHAKULA CHAKE NI WADUDU WARUKAO NA MCHWA PAMOJA NA LAVA(LARVAE).UNAWEZA NIULIZA CHOCHOTE KUHUSU NYOKA MAANA NDIYO FANI YANGU HASWAAAAA!!!
AHSANTENI KWA USHIRIKIANO!!!![/QUOTE]
Mkuu Mimi naishi mazingira yenye nyoka sana....sasa nasikia kna mmea ukipanda kunguka uzio nyoka akanyagi kabisa...je huo ni mmea gain!? je kuna ukweli wwte kuhusu jiwe LA kunyonya sumu nyoka au PESA aina ya sarafu!?
 
Nikiwa mdogo kule kijijini, huyu nyoka akionekana tulikuwa tukiambiwa jambo baya litatokea kwenye familia kama msiba
 
Du! Huyu atakuwa ndumilakuwili kama nanihii wa ACT tanzania
 
Back
Top Bottom