Nyoka amtoa baru mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyoka amtoa baru mbunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mrdash1, Feb 11, 2012.

 1. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Nyoka amtoa baru mbunge[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]
  [​IMG]
  [/TD]
  [TD]
  NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, alitimua mbio kunusuru maisha yake na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mwanri alikuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kuendesha harambee ya kujenga Kanisa la Kilingi, akiwa na mkewe meza kuu, aliwashangaza waumini alipokimbia akiwa amenyanyua mikono juu huku akitamka maneno ya “shindwa kwa Jina la Yesu wewe shetani, shetani shindwa kwa Jina la Yesu,” na wageni wengine waalikwa wakianguka chini wakijiokoa. Hali hiyo ilitokea baada ya nyoka kutoka kusikojulikana kuingia kanisani huku Naibu Waziri akijiandaa kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa. Waumini walikimbizana na kiumbe huyo kwa mawe na viti bila kujali kama walikuwa ibadani, huku Askofu na wachungaji wengine wakiendelea kusali na waumini kutakiwa kurejesha utulivu katika ibada.
  Tukio hilo lilitokea katika ibada ya saa nne iliyokuwa ikiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, ambayo pia ilikuwa ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo.


  Hata hivyo, jitihada za waumini za kumkimbiza nyoka huyo kutaka kumwua hazikufanikiwa, baada ya kutoweka asionekane tena, jambo lililoacha simulizi la ni kwa jinsi gani alifika mahali hapo.

  “Inashangaza sana kwani lazima ujiulize alifikafikaje hapo mbele, wakati nyuma yangu kulikuwa na watu wengi...alikuwa na hasira sana, kwani alikuwa tayari kung'ata, kwa kweli hadi sasa mimi sielewi ni mambo gani haya,” alisema Mwanri. Hata hivyo hakuna madhara makubwa yaliyotokea mbali na mhamaniko uliowapata waumini hao. Nyoka huyo hakuweza kutambuliwa aina yake kutokana na mtafaruku huo.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,763
  Trophy Points: 280
  Huu utaratibu mpya wa wanasiasa ya kutafuta publicity kwenye majukwaa ya ibada yatakuwa na mambo mengi sana zaidi ya nyoka huyu.
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hii ilishatoka mara kibao hapa jukwaani wajamini au mtoa mada hujaiona??
  tafuta mada za j3 au j4.
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sasa hapo wanamanisha nini?
   
Loading...