black abdu
Senior Member
- Dec 2, 2022
- 157
- 214
Kusema ukweli huwa nakereka sana kusikia nyimbo za dini, zinapigwa kwenye sehemu za starehe, hasa Bar. Sehemu hizi ni sehemu Shetani na jeshi lake wanafanya kazi zao kwa ufanisi, na anaona ni kama kuikosea heshima dhana ya kuwa nyimbo za dini ni sehemu ya kuabudu.
Kwenye hizi Bar, zinapopigwa nyimbo hizi wakati watu wamelewa, naona ni kama kumkebehi Mungu.
Na pia ni kuzikosesha heshima nyimbo hizi, ambazo zilipaswa kuzikumbusha nyoyo Utukufu wa Mungu.
Kwenye hizi Bar, zinapopigwa nyimbo hizi wakati watu wamelewa, naona ni kama kumkebehi Mungu.
Na pia ni kuzikosesha heshima nyimbo hizi, ambazo zilipaswa kuzikumbusha nyoyo Utukufu wa Mungu.