Nyimbo za Bongo Fleva zenye stori za kweli

Kuna bwana mmoja alitoa diss track enzi hizo aliwadiss wasanii wote wa bongo fleva
Kuna mstari anasema hivi " Prof Jay umeungua umepewa miwaya na dada wa tanga"

Hyuyo bwana anatoka kikosi Cha mizinga Sasa
 
Kuna bwana mmoja alitoa diss track enzi hizo aliwadiss wasanii wote wa bongo fleva
Kuna mstari anasema hivi " Prof Jay umeungua umepewa miwaya na dada wa tanga"

Hyuyo bwana anatoka kikosi Cha mizinga Sasa
Tupe jina la wimbo tutafute kwenye makabrasha
 
1. Sitaki Demu - Juma Nature
Nature alitoa kibao hiki mara baada ya kugombana na mpenzi wake Sinta

2. Inaniuma Sana - Juma Nature
Chanzo cha wimbo huu ni kama ilivyokuwa hapo juu, Nature aliachana na Sinta msichana aliyempenda sana kabla ya kuzinguana.

3. Msela - Bushoke
Huu wimbo Bushoke aliuimba kwa heshima ya mshikaji wake wa siku nyingi, Papii Kocha ambapo kipindi hiko alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Ukonga.

4. Tutakukumbuka - Crazy GK
Mwaka 2001 wakati GK alipomshirikisha TID katika wimbo huu, hawakujua kama utabaki classic daima, wimbo huu ulikuwa ni kwa heshima ya legend wa Bongo Fleva, D-Rob.

5. Kijana Mteja - Feruz
Feruz aliamua kutunga kibao hiko kumuelezea msela wake Daz Baba ambaye alikuwa ameanza kutumia unga, bahati mbaya miaka michache baadae Feruz naye akaingia katika uraibu huo wa matumizi ya unga.

6. Niaje - Man Dojo & Domo Kaya
Katika wimbo huu, kuna mstari unasema "Imepigwa simu twende Alhamisi, tukafanye vocal tukafanye beat, nachukua ndinga mpaka Bongo City, Vingunguti alikoolewa aunt, Wameiba fedha, Buti, Wameiba Jeans"

Domo Kaya anasema walikuja Dar kutoka Arusha kurekodi Bongo Record, wakafikia Vingunguti, wakaibiwa kila kitu, ilibidi kesho yake waende studio na ndala na nguo za kuazima!

7. Leah - Dully Sykes
Endelea kupumzika kwa amani Leah, Dully aliimba historia ya kweli ya binti huyo.

8. Msinitenge - Prof Jay

9. Amekoma - Mh. Temba
Alitoa kibao hiko ikiwa ni stori ya kweli ya mshikaji mmoja hivi wakuitwa Steve mitaa ya Temeke Unubini, aliyependa sana mademu na kujikuta akimbeba shoga bila kujua, ila Temba akabadili jina katika wimbo na kumuita mhusika Side Mnyamwezi

10. Ametoroshwa - Biz Man
Kama alichoimba na ndio kilichomkuta, hata msahau Sauda kwa kumuacha chooni walipoenda kuoga na kukimbia na mwanaume mwingine

Unaweza ukaongeza na wewe...

Tamara - Hard Mard
Huu wimbo ulichuana sana na wimbo wa Enomaiki wa Ziggy Dee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom