Nyie wanawake nani kawaroga?

Maisha pesa

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
687
1,000
Nyie wanawake nani kawaroga?

Siku ya mechi ya nusu fainali Euro France vs Germany nilikuwa nimekaa baa moja maridadi pembeni ya jiji nikibarizi na glasi yangu ya wine huku macho yangu yakiwa makini kwenye tv kubwa ya inch kama 70 hivi.

Wakati mechi ikielekea ukingoni huku France wakiwa mbele 1-0 ghafla Antoine Griezmann akapachika bao la pili na kuwa 2-0. Kijana mmoja aliyekuwa mbele yangu aliruka kwa furaha huku akishangalia kuwa ameshinda milion 5 baada ya kubet. Sielewi ni wapi kilipotoka kikundi cha wanawake watatu waliovalia nguo fupi na laini zenye kuonyesha maungo yao wakaanza kumpepea kijana wa watu aliyeshinda milioni 5 huku wakimbusu na kumkumbatia na kumuinua kitini wacheze naye mziki.

Hakika niliyaona mapenzi ya ghafla kwa kijana huyo wakimmiminia kinywaji kwenye glasi picha kibao za mashauzi zikapigwa yaani ilikuwa ni vituko lakini baadae kijana alishtuka akaamua kuwakimbia make anaonekana hakuwa mkware.

Jamani nauliza tena wanawake nani kawaroga? Yaani hadi kwenye hela za betting? Pengine kijana alishajiwekea nia akishinda anunue kiwanja au afungue biashara ya saloon.
 
love you

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
728
1,000
Usi generalize jmn hatukuwepo wote..ulivyo ongea Ni as if wanawake wote tulikuwepo kupapatikia pesa ambayo hata kuiona hawajaiona
 
Maisha pesa

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
687
1,000
Usi generalize jmn hatukuwepo wote..ulivyo ongea Ni as if wanawake wote tulikuwepo kupapatikia pesa ambayo hata kuiona hawajaiona

Sorry lakini nia yangu haikuwa kugeneralize ila nimechukua ka sample kadogo ka baadhi ya wanawake.
 
MO11

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
18,057
2,000
Usi generalize jmn hatukuwepo wote..ulivyo ongea Ni as if wanawake wote tulikuwepo kupapatikia pesa ambayo hata kuiona hawajaiona
yaani wanawake na pesa ni mgonjwa na dawa
kama sio style hii basi style nyingine ila lengo ni moja
 
mzurimie

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,144
2,000
Si umgesemea uliowaona tu sababu sio wanawake wote wapo hivyo.

Na pia wanaume nao wakijua mwanamke ana pesa nao ujigonga hivyon hivyo kwa njia mbalimbali.

Ndio maisha walitaka kubahatisha kupata waliyotaka..
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,604
2,000
Nyie wanawake nani kawaroga?

Siku ya mechi ya nusu fainali Euro France vs Germany nilikuwa nimekaa baa moja maridadi pembeni ya jiji nikibarizi na glasi yangu ya wine huku macho yangu yakiwa makini kwenye tv kubwa ya inch kama 70 hivi.

Wakati mechi ikielekea ukingoni huku France wakiwa mbele 1-0 ghafla Antoine Griezmann akapachika bao la pili na kuwa 2-0. Kijana mmoja aliyekuwa mbele yangu aliruka kwa furaha huku akishangalia kuwa ameshinda milion 5 baada ya kubet. Sielewi ni wapi kilipotoka kikundi cha wanawake watatu waliovalia nguo fupi na laini zenye kuonyesha maungo yao wakaanza kumpepea kijana wa watu aliyeshinda milioni 5 huku wakimbusu na kumkumbatia na kumuinua kitini wacheze naye mziki.

Hakika niliyaona mapenzi ya ghafla kwa kijana huyo wakimmiminia kinywaji kwenye glasi picha kibao za mashauzi zikapigwa yaani ilikuwa ni vituko lakini baadae kijana alishtuka akaamua kuwakimbia make anaonekana hakuwa mkware.

Jamani nauliza tena wanawake nani kawaroga? Yaani hadi kwenye hela za betting? Pengine kijana alishajiwekea nia akishinda anunue kiwanja au afungue biashara ya saloon.
Yawezekana pia alipanga awagonge wote kwa KUWADANGANYA kashinda betting baada ya kusoma ramani, sisi wanaume achana nasi kabisa!
 
Maisha pesa

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
687
1,000
Si umgesemea uliowaona tu sababu sio wanawake wote wapo hivyo.

Na pia wanaume nao wakijua mwanamke ana pesa nao ujigonga hivyon hivyo kwa njia mbalimbali.

Ndio maisha walitaka kubahatisha kupata waliyotaka..

Ni mwendo wa kuangalia fursa tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom