Nyie serikali,utoaji wa elimu hii mwisho lini?

ikhlas

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
1,038
1,278
Hii inachosha sasa,ina maana mpaka leo bado tu serikali inapanga kuelimisha wananchi juu ya masuala mbali mbali yanayo tuhusu,na mengie yameshatolewa elimu lakini bado wananchi hawaja elimka,hivyo kuna utoaji mwengine unafanyka miaka nenda miaka rudi tangu enzi za nyerere,
Tumechoka kusikia uelimishwaji juu ya,
1.Faida za kujinga na mifuko ya hifadhi ya jamii..
2.Bima za afya
3.Umuhimu wa kulipa kodi
4.Umuhimu wa EFD machine
5.Elimu ya vitambulisho vya taifa
6.Elimu ya kutii sheria za nchi
7.Polisi jamii
8.Kujiajiri
9.Elimu ya katiba
10.Madereva na swala la mwendo kasi
11.Kutunza mazingira
12.Kutii na kuheshimu sheria za barabarani
13.Haki na nafasi ya mwanamke katika jamii
14.Mila potofu
15.Upandaji miti
16.Utunzaji wa vivutio vya utalii
17.Mapambano dhidi ya ukimwi
18.Ngono zembe
19.Ndoa za utotoni
20.Umuhimu wa kupima afya
Continueeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.......................................................
Hivi masomo haya na eleimu hii tamati ni lini ili tu graduete na kuanza kuyafanyia kazi?
Je somo la muhimu kuliko yote(core subject) ni lipi ili liekewe mkazo wa kipekee?
Kuna utaratibu gani wa utoaji elimu hii serikalini au kila sekta ina mipango yake?
Je kuna haja ya masuala haya yawekwe kwenye mtaala RASMI WA ELIMU YETU?
 
Back
Top Bottom