Nyie Manara TV acheni kutuongopea

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,138
7,909
Kuna huyu mtangazaji wa Manara TV anayehoji watu kwa kifaransa, leo alimuhoji mchezaji wa ASEC Mimosas. Watu wamekuwa wanamsifia sana huyu dogo kisa ufahamu wake wa lugha ila ukiangalia inaonyesha hajawahi kupitia mafunzo yoyote ya uandishi wa habari kwa sababu kuna vitu vingi anavikosea ikiwemo kutotoa tafsiri ya kile ambacho anayemuhoji anasema. Yaani anaweza kumuhoji mtu kwa kifaransa akamaliza akafunga mahojiano mchezo umeishia hapo. Hili nimeliona mara nyingi linatokea.

Katika video waliyopost Manara TV baada ya mechi ya leo ya Simba wameipa kichwa "MCHEZAJI WA ASEC MIMOSAS AIKATAA SIMBA AFUNGUKA MECHI HII HAWAKUWA NA MIPANGO NAYO". Ngoja nimwambie huyu dogo na hao Manara TV wasidhani wanaojua kifaransa nchi hii ni yeye tu kwa hiyo waache kutupiga fix.

Huyo dogo alimuuliza swali "Labda unataka uje kucheza hapa Tanzania?", yeye akajibu, "Hili ni swali la mbali sana kujibu. Mimi, kwanza, Asec. Nina raha, Ni klabu bora katika nchi yangu. Nafurahi kusema Simba, Tanzania, lakini kwa sasa Asec, nina furaha." kwa kifupi alisema ukiacha Asec ambapo ana furaha, akija Tanzania angependa kuchezea Simba.


View: https://www.youtube.com/watch?v=nKt7xoNuTw0
 
Mi media ya kimchongo,ya kinafiki na kilimbukeni...yenye wivu na kisukununu kwa Simba...
 
Back
Top Bottom