Nyie kwenyu ni cityhall

Nyie kwenyu ni cityhall

Sijawahi kughadhibika kama siku ile nilipopata hii taarifa ya habari kupitia radio mbao ya pale kijijini kwetu... Maneno hayo ya kusema kwetu ni cityhall (babu yangu hawezagi kusema C.. Kwake yeye C ni shi) yalitamkwa na mtemi mmoja wa mji mkubwa wa mbali vijiji kadha kutoka cha kwetu...
.. Nikaona mtihani ndio huu yani nina hasira halafu nikatafsiri tena nisitumie tafsida yoyote.... Nikamkumbuka jamaa yangu mmoja ambaye tuna mazoea ya kukutana barazani kwetu na kubadilishana mawazo.... Kuna siku alinipigia simu kwenye kilongalonga cha zawadi.... Kwa sauti ya kilevi akasema Oyaa niko kwa mama muuza hapa kilabuni nina togwa kombe la tatu, kaingia jamaa anauza majambia je nitoe ofa ya kuyanunua nakugawa kwa walevi ooh sorry wanywaji wengine!? [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]... Nikajua kweli togwa sio mbege.. Nusu kilevi nusu lishe[emoji23] [emoji23] [emoji23] .. Wanyaki wanajua vema...

Hatimaye nikakubali kukalimani kwa jinsi nilivyoona itapendeza zaidi na sitaishia kuchezea kichapo kwa wazee korofi wa kijijini kwetu... Ila sikutamka kama babu anavyotamka [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Mwenyekiti wa kijiji hakuwepo
Katibu tarafa pia hakuwepo
Mgambo na sungusungu wote walikuwa na udhuru.. Ilikuwa ni siku ya gulio kijiji cha jirani
Balozi alikuwa kwa mganga anatibiwa mshipa... Nikajiona mwenye nafasi ya kujiachia nitakavyo na wazee wangu.. Unajua ofisi ya kijiji ndio hapo hapo kuna selo?
..... Wazee wangu city hall kwa kinyaki ni ukumbi wa kijini.. Hapo hukutana watu wote kujadiliana mambo yote mazuri na mabaya... Lakini city hall kama tukiamua kufuata lafudhi ya babu yangu aliyepigana vita Burma ni hivi
. Tuna akili lakini hatuzitumii
. Tuna ardhi lakini kila siku tunalia njaa
. Tuna malighafi zetu za kijiji lakini kila siku kigulu na njia kwenda kuhemea kwa wengine
. Nyumba zetu ni vibanda, barabara zetu ni vichochoro, zahanati yetu iko hoi bin taaban, mazao shambani yanakufa kwa kukosa mbolea...
. mabwana afya, afisa mifugo na wataalam wetu wote wamekimbia fani wote wamejiunga kwenye kile kilinge cha kupiga soga na kuhemea...
Mwenyekiti wetu wa kijiji yote haya hayaoni kila siku ni yeye na mgambo na sungusungu wake... Si mmeona hata leo hawapo hapa? Wako wapi? Wazee wanatikisa vichwa kwa huzuni....
Hebu oneni kule kwa wenzetu... Angalieni ustawi wa jamii zao.. Bwana shamba ni bwana shamba.... Tabibu ni tabibu,... Kila mtu na ujuzi wake....
Wenzetu wana vikao vya kila siku kila wiki na hata mwezi.. Wnajadiliana na kukubaliana kwa pamoja.. Wanaaminiana katika utendaji... Hawaviziani wala kuleteana majungu makopo na masufulia
Kwenye korokoroni zao wamejaa wahalifu wanaofundishwa utu wema wabadilike na kuwa wa faida kwenye kaya na vijiji vyao.. Wazee wangu hebu oneni hapa kijijini kwetu.... Selo yetu imejaa watu wa namna gani.. Mmeziona zile hukumu za yule hakimu? Mmewaona mgambo na sungusungu wetu wanakamata kina nani? Wazee wangu kijiji chetu kimeitwa city hall kutokana na mambo kama haya...
Ambiere unawapa tabu akina DAB hawataweza kuambulia kitu hapa. Ni kama umpe fulani kitabu cha Things Fall Apart atatoka kapa
 
teheeee hizi algebra sio mchezo ..""
naona bashite anaweza kurudia rudia kuusoma huu Uzi kutwa nzima na bado akakosa majibu stahiki ""

.kwahiyo inamaana wanaotuambia kuwa Tanzania itakuwa ya viwanda ilhali mvua ikinyesha tu umeme unakatika kama tumewasha kibatali huwa wanatuongopea ...
 
M/kiti wetu hataki kujifunza kwa vijiji jirani...ajiona yeye anapewa maono na muumba wake!
mgambo & sungusungu hawahusiki kwenye usalama wa wanavijiji tena bali kutwa kukamata wasiopaswa kamatwa!
jela zetu zimejengwa ili kumkomoa mtu na sio kumrekebisha tabia ili akirudi mtaani awe mwanakijiji bora!


hii 'shittyhall' hii😡😡😡..
 
teheeee hizi algebra sio mchezo ..""
naona bashite anaweza kurudia rudia kuusoma huu Uzi kutwa nzima na bado akakosa majibu stahiki ""

.kwahiyo inamaana wanaotuambia kuwa Tanzania itakuwa ya viwanda ilhali mvua ikinyesha tu umeme unakatika kama tumewasha kibatali huwa wanatuongopea ...
Moja jumlisha moja wanasema eti ni kumi na moja... Kuna wakati kidogo nikubaliane na hii aljebra ya kizio cha tatu bila baki.. Lakini nikasema hapana ngoja nijaribu na magazijuto nione yatanipa jibu gani.. Dah kumbe niko city hall sikutaka kuendelea zaidi
 
M/kiti wetu hataki kujifunza kwa vijiji jirani...ajiona yeye anapewa maono na muumba wake!
mgambo & sungusungu hawahusiki kwenye usalama wa wanavijiji tena bali kutwa kukamata wasiopaswa kamatwa!
jela zetu zimejengwa ili kumkomoa mtu na sio kumrekebisha tabia ili akirudi mtaani awe mwanakijiji bora!


hii 'shittyhall' hii😡😡😡..
Thinking a great way... Save the day
 
Nikamkumbuka jamaa yangu mmoja ambaye tuna mazoea ya kukutana barazani kwetu na kubadilishana mawazo.... Kuna siku alinipigia simu kwenye kilongalonga cha zawadi.... Kwa sauti ya kilevi akasema Oyaa niko kwa mama muuza hapa kilabuni nina togwa kombe la tatu, kaingia jamaa anauza majambia je nitoe ofa ya kuyanunua nakugawa kwa walevi ooh sorry wanywaji wengine!? [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]... Nikajua kweli togwa sio mbege.. Nusu kilevi nusu lishe[emoji23] [emoji23] [emoji23] .. Wanyaki wanajua vema...
Hivi Unajua niliyanunua halafu nikayagawa kweli lakini nikawahi ondoka kilabuni[emoji23][emoji23].
 
Hivi Unajua niliyanunua halafu nikayagawa kweli lakini nikawahi ondoka kilabuni[emoji23][emoji23].
Hahahaaa... Sorry nilisahau kukudipu kwenye hii mada...
 
.
IMG-20180309-WA0105.jpg
 
Ni kweli nchi yetu ni city hall hata watoto wanajua kaka mshana hide my ID
 
Back
Top Bottom