Nyie kwenyu ni cityhall

Nyie kwenyu ni cityhall

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,850
Reaction score
831,121
Sijawahi kughadhibika kama siku ile nilipopata hii taarifa ya habari kupitia radio mbao ya pale kijijini kwetu... Maneno hayo ya kusema kwetu ni cityhall (babu yangu hawezagi kusema C.. Kwake yeye C ni shi) yalitamkwa na mtemi mmoja wa mji mkubwa wa mbali vijiji kadha kutoka cha kwetu...
.. Nikaona mtihani ndio huu yani nina hasira halafu nikatafsiri tena nisitumie tafsida yoyote.... Nikamkumbuka jamaa yangu mmoja ambaye tuna mazoea ya kukutana barazani kwetu na kubadilishana mawazo.... Kuna siku alinipigia simu kwenye kilongalonga cha zawadi.... Kwa sauti ya kilevi akasema Oyaa niko kwa mama muuza hapa kilabuni nina togwa kombe la tatu, kaingia jamaa anauza majambia je nitoe ofa ya kuyanunua nakugawa kwa walevi ooh sorry wanywaji wengine!? ... Nikajua kweli togwa sio mbege.. Nusu kilevi nusu lishe .. Wanyaki wanajua vema...

Hatimaye nikakubali kukalimani kwa jinsi nilivyoona itapendeza zaidi na sitaishia kuchezea kichapo kwa wazee korofi wa kijijini kwetu... Ila sikutamka kama babu anavyotamka
Mwenyekiti wa kijiji hakuwepo
Katibu tarafa pia hakuwepo
Mgambo na sungusungu wote walikuwa na udhuru.. Ilikuwa ni siku ya gulio kijiji cha jirani
Balozi alikuwa kwa mganga anatibiwa mshipa... Nikajiona mwenye nafasi ya kujiachia nitakavyo na wazee wangu.. Unajua ofisi ya kijiji ndio hapo hapo kuna selo?
..... Wazee wangu city hall kwa kinyaki ni ukumbi wa kijini.. Hapo hukutana watu wote kujadiliana mambo yote mazuri na mabaya... Lakini city hall kama tukiamua kufuata lafudhi ya babu yangu aliyepigana vita Burma ni hivi
. Tuna akili lakini hatuzitumii
. Tuna ardhi lakini kila siku tunalia njaa
. Tuna malighafi zetu za kijiji lakini kila siku kigulu na njia kwenda kuhemea kwa wengine
. Nyumba zetu ni vibanda, barabara zetu ni vichochoro, zahanati yetu iko hoi bin taaban, mazao shambani yanakufa kwa kukosa mbolea...
. mabwana afya, afisa mifugo na wataalam wetu wote wamekimbia fani wote wamejiunga kwenye kile kilinge cha kupiga soga na kuhemea...
Mwenyekiti wetu wa kijiji yote haya hayaoni kila siku ni yeye na mgambo na sungusungu wake... Si mmeona hata leo hawapo hapa? Wako wapi? Wazee wanatikisa vichwa kwa huzuni....
Hebu oneni kule kwa wenzetu... Angalieni ustawi wa jamii zao.. Bwana shamba ni bwana shamba.... Tabibu ni tabibu,... Kila mtu na ujuzi wake....
Wenzetu wana vikao vya kila siku kila wiki na hata mwezi.. Wnajadiliana na kukubaliana kwa pamoja.. Wanaaminiana katika utendaji... Hawaviziani wala kuleteana majungu makopo na masufulia
Kwenye korokoroni zao wamejaa wahalifu wanaofundishwa utu wema wabadilike na kuwa wa faida kwenye kaya na vijiji vyao.. Wazee wangu hebu oneni hapa kijijini kwetu.... Selo yetu imejaa watu wa namna gani.. Mmeziona zile hukumu za yule hakimu? Mmewaona mgambo na sungusungu wetu wanakamata kina nani? Wazee wangu kijiji chetu kimeitwa city hall kutokana na mambo kama haya...
 
Hahahaaa....mgambo wapo busy...wanaruka na kukanyagana.
.
IMG-20180308-WA0135.jpg
fujo22.jpg
photo-741931.jpg
 
Hiyo picha ya mwisho naomba ufafanuzi sijaielewa ni choo au kitu gani?

Napenda staili yako ya uandishi, yaani unatumia Fasihi kama Roma alipoaga kwenda Zimbabwe. (Huu wimbo kama una akili fupi huatweza kuuelewa alimaanisha nini) ila kadri siku zinavyokwenda ndivyo hali inavyojidhihirisha jamaa alimaanisha nini

[HASHTAG]#hidemyid[/HASHTAG]
 
Hiyo picha ya mwisho naomba ufafanuzi sijaielewa ni choo au kitu gani?

Napenda staili yako ya uandishi, yaani unatumia Fasihi kama Roma alipoaga kwenda Zimbabwe. (Huu wimbo kama una akili fupi huatweza kuuelewa alimaanisha nini) ila kadri siku zinavyokwenda ndivyo hali inavyojidhihirisha jamaa alimaanisha nini

[HASHTAG]#hidemyid[/HASHTAG]
.
IMG-20180308-WA0244.jpg
 
Back
Top Bottom