Nyerere's legacy failed 100% (economically)

Nyerere's legacy failed 100% (economically)

Tukiorodhesha nchi zilinonufaika na ujamaa basi orofha ni China, Urusi na nyingine chache zizofika 10. Lakini tukiorodhesha nchi zilizonufaika na mifumo ya kipebari orodha ni ndefu sana. Huoni kua ni poor choice kuchagua njia ambayo ni wachache tu walifanikiwa kwa kuipitia??
Urusi sio nchi ya kijamaa na China utawala ni wa kikomonisti lakini ni mix ya ujamaa na ubepari
 
mkuu mm sijamtaja magufuli, namzungumzia Mwl. je lipi la kucelebrate
Mkuu unapaswa kuelewa kuwa maisha ni mchako, environnement y'a wakati ilikuwa ni tofauti na leo, hata envronment ya leo haitakuwa sawa na ya kesho.
Kuhusu ukombozi ilikuwa ni uamuzi wa OAU, na tanzania kuchaguliwa kuwa makao makuu y'a ukombozi barani Africa.
Mfumo wa siasa wakati wa mwalimu uligawanyika kwenye katika kambi mbili,uwe magharibi uwe bebari au uwe mashariki uwe mjamaa .
Kundi lingine lilikuwa lisilofungamana na upande wo wote.
Kuhusu watu kuhamishiwa katika vijiji vya ujamaa unaangalia dhamiri ya hiyo ilikuwa sahihi ? Changa moto zake zilikuwa zipi zilitatuliwaje ?
Kuhusu kutaifisha shule hospital, viwanda, nina imani kama sio ujasiri wa mwalimu kutaifisha shule asilimia 90 ya wasomi tulionao leo wangekuwa either wakulima au wafungaji.
 
Kwenye sera za uchumi alifeli tena sana tu na hata yeye mwishowe aligundua makosa yake, serikali haipaswi kufanya biashara inapaswa ku-regulate na ku support ukuaji wa biashara kisha ikusanye sehemu ya faida kama kodi.

Pia serikali haiwezi kutoa huduma zote za kijamii kwa ubora ni lazima i support na kuruhusu sekta binafsi zinazotoa huduma kama afya, elimu na fedha (benki). Yeye alitaka vyote viendeshwe na serikali mwishowe viliishia kufa tu.

Huyu wa sasa nae ameanza kuingia kwenye ka mtego ka kutamani serikali i control kila kitu, sera za namna hiyo mwisho wake ni unajulikana kabla hata haujafika.
Mbona huyu nae ni walewale,eti mashirika na taasisi za serikali mfano nssf and the likes kujenga viwanda
 
Serikali ya marekani huwa inatoa kandarasi kwa makampuni binafsi kutengeneza vifaa na mifumo ya ulinzi. Kwenye mikataba serikali inakuwa na hakimiliki ya teknolojia kwasababu za kiusalama. Pale marekani inapoamua kuiuzia nchi nyingine vifaa au mifumo ya kijeshi serikali ndio inatoa ridhaa kwa sababu ya kuwa na hakimiliki. Mara nyingi nchi moja inapoiuzia silaha nchi nyingie ni lazima silaha hizo zitakuwa zimepitwa na wakati au kuna slight modification. Mfano mzuri ni ndege f22 amabazo Australia, Israel, UK wameuziwa na marekani. Kila nchi imefanya modification kwenye avionics na mifumo mingine ya mawasiliano. Ukweli ni kwamba makampuni binafsi yanatengeneza vifaa vya kijeshi kwenye nchi za magharibi, nchi za mashariki kampuni nyingi zinamilikiwa na serikali.
Hiyo haimaanishi kuwa serikali haifanyi biashara kwa sababu haimiliki karakana. Apple ni shirika kubwa duniani na hawana karakana, huwa wana-design na kuwa na hatimiliki na kutoa kandarasi kwenye karakana China.
Maana yake, ni kuwa Apple ndiyo kampuni yenye umiliki, iayouza na kula faida ya vifaa vinavyotengenezwa China. Ile ni kama kandarasi tu.
US Army, Navy, Air force wana-design na kumiliki technology nyingi tu. Wanatoa kandarasi kwa viwanda na products zinakuwa zao na wakiuza, hela zinaenda serikalini. Of course watauza silaha zisizo mpya but not obsolete.
All in all, serikali za mataifa makubwa zina makampuni, zina mabenki n.k na mara nyingi zina monopoly kubwa kwenye biashara na siyo lazima ziwe na ushirikiano na watu binafsi.
Serikli nyingi duniani zina viwanda hasa kwenye sekta ya nishati, usafiri, mawasiliano etc.
 
Ni UPUMBAVU uliotukuka kumlaumu hayati JK Nyerere (R.I.P) kwa uchumi mbovu tulionao!

Narudia tena ni UPUMBAVU ULIOTUKUKA!

That old man raised this fuckin country from the scratch. He simply created something from nothing!

Nyerere was long sited, alijua Tanzania ya kesho itakua ya namna gani, na inahitaji nini.

It's just ridiculous to criticize his UJAMAA policy without pointing out the serious problems that we're going through because of CAPITALISM!

Mwalimu alijua Tanzania ina rasilimali ambazo ni lazima zilindwe kwa manufaa ya vizazi vinavyo kuja!

Mwalimu alitambua umuhimu wa ujamaa katika kuliunganisha taifa lenye makabila zaidi ya mia moja.

Mwalimu alijua umuhimu wa ujamaa katika kidhibiti nidhamu na maadili kwa watumishi wa uma!

Wewe unaemlaumu mwalimu, hebu nipe majibu kwa hoja zifuatazo;

- Tanzania imepoteza rasilimali kiasi gani wakati wa ujamaa chini ya Nyerere?

- Je, baada ya kuadopt capitalism, tumepoteza rasilimali kiasi gani chini ya mwamvuli wa mikataba mibovu na rushwa?

- Miaka zaidi ya 30 sasa tangu Nyerere aachie madaraka kwa hiyari, je mmeipata ile demokrasia mnayoitaka? Imewafikisha wapi?

- Mnalaumu mfumo wa chama kimoja eti ulibana demokrasia, je sasa hivi mna vyama vya siasa zaidi ya nane, mbona mnapigwa risasi? Mbona hata mikutano ya hadhara hamfanyi?

Ni mtu mwenye fikra fupi pekee ndie anaeweza kumlaumu baba wa taifa.

Ukweli ni kwamba Mwalimu alichukua nchi akiwa na wasomi wachache wanaoweza kumsaidia kutatua changamoto.

Nchi ilikua changa na hatukua hata na sehemu ya kuigia namna ya kuiendesha.

Ulisikia ufisadi kama wa sasa enzi za mwalimu? That guy was a saint!

Nyerere alikua na mapungufu machache ya kibinadamu kabisa, ila kwa makubwa aliyotutendea tutakufuru kama tutaanza kuzungumzia mapungufu yake ya kibinadamu!

Capitalism mnayoitukuza ndio iliyochukua almasi ya mwadui, dhahabu ya geita, tanzanite ya mererani hadi twiga wa Serengeti waliopandishwa ndege!

Mwalimu alijua athari zake, ndio maana alichagua ujamaa!

Mungu amlaze pema!
 
Back
Top Bottom