Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
Hapa unapotosha. Ni madarasa gani hayo "maalum" unayozungumzia? Tupo wengi tuliokuwepo enzi hizo!
Ilikuwa si rahisi kupata kadi za CCM kama mnavyozipata siku hizi kwa kununua tu.
Zamani kulikuwa na mafunzo maalum ambayo kila alietaka kupata kadi hiyo ilikubidi kuhudhulia mafunzo hayo kwa miezi mitatu ambayo yalikuwa yanaratibiwa na CCM yenyewe na kuendeshwa na makada wa CCM wengi wao walikuwa wanatoka Chuo cha Chama kivukoni. Na siku ya kupewa kadi hizo mlikuwa mnakula kiapo maalum kabla kukadhibiwa KADI Hiyo.
Na kwa kukufahamisha haikuwezekana kabisa mtu kuweza kujiunga na Chuo kikuu bila kuwa na Kadi ya Chama CCM na ilikuwa ni moja ya kigezo kuweza kuchaguliwa kujiunga hapo UDSM. Na kukujuza zaidi ulikuwa huwezi pata Passport au hata kazi Serikalini bila kuwa na Kadi za CCM. na kubwa zaidi hata maofisini au katika majeshi na mashirika yote kulikuwa na tawila CCM n viongozi wake walikuwa na nguvu kuliko hata Mkurugenzi mkuu.
Enzi hizo huko Tanzania ilikuwa na Sera kuwa Chama kimeshika hatamu za uongozi.
nafikiri nimekupa mwanga nafikiri waliowahi kupitia JKT nafikiri wanalijua hilo Pale RUVU JKT PEO alikuwa anaitwa WO II Nassari.