NYERERE ni 'MSANII' kwanza mzalendo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,106
2,000
Kila nikitafakari kilichofanyika kwenye muungano bado nakosa jibu. Nilijiunga CCM mwaka 1980 nikiwa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Wakati huo,CCM ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Baba wa Taifa,Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mambo ya Nyerere bado siyaelewielewi.

Mwaka 1964,nikiwa na umri wa kutosha lakini wa ujana,nilishuhudia Muungano huu wa sasa. Nilishuhudia kuchanganywa udongo wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Udongo huo ukaua nchi husika. Ukazaa nchi moja: Tanzania. Ilikuwa ni tarehe 26/4/1964,miezi mitatu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.

Usanii

Nyerere aliiua kabisa Tanganyika na kuiacha Zanzibar ndani ya Tanzania. Tanganyika ikabatizwa jina la Tanzania Bara. Kemia aliyotumia Nyerere ndiyo inayonichanganya. Muungano huu ulikuwa wa namna gani ikiwa nchi sasa zimekuwa tatu huku moja ikiwa imekufa? Yaani, Tanganyika+Zanzibar=Tanzania + Tanzania Bara+Zanzibar.Ukitaka kuziona nchi hizi tatu ni rahisi. Fuatailia Challenge kule Uganda halafu subiria michuano ya kombe la dunia au mataifa ya Afrika. Utaziona timu za Tanzania Bara,Zanzibar na Tanzania.Pia,angalia Serikali zilizopo.Kuna Wizara za Tanzania,zipo za Zanzibar na pia za Tanzania Bara. Kwa mfano,kuna Wizara ya Miundombinu ya Tanzania Bara na ile ya Zanzibar.Hakuana ya Tanzania.

Kemia gani hii jamani? Huu si usanii uliotukuka uliofanywa na mzalendo wetu Nyerere? Nini kilitokea hapa? Huwa kichwa kinaniuma
 
msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,828
2,000
We kijana maswali magumu namna hiyo humu huwa hayaulizwi,,,,,,we waulize wazanzibar watakujibu lakini hawa vijana wagonjwa wa chademaliasis wanaugonnjwa wa kupenda chongo huita kengeza
 
LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,171
2,000
Mzee Tupatupa

Umesema huwa unawaza mpaka kichwa kinakuuma?

Kwa kweli fikira zako ndio mwisho wake hapo!
 
Last edited by a moderator:

Nyakwec's Bro

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
820
250
Na hapa ndiyo huwa ninampenda baba wa taifa huwa hajikwezi huwa anakubali kwamba kuna makosa na inabidi sasa yasahihishwa kwamba unawezekana wao hawakuweza kuyafanya kwa kutojua au sababu nyingine tu hivi.
tulifanya mambo mengi sana,.mengine mazuri mengine ya kijinga,tatizo lenu mnaacha mazuri mnachukua ya kijinga-jk nyerere
 
Mbowewe

New Member
Dec 2, 2012
1
0
Mimi nadhani muandishi yupo sawa, tuache ushabiki wa kisiasa TANGANYIKA yetu haipo na umeuliwa na Nyerere kwa matashi ya kisiasa, cha kufanya kwasasa ni kuachana na habari za kujivunia utanzania badala yake ni vyema tujivunie utanganyika wetu. wazanzibari wana Nchi yao wala hawako tayari kupoteza taifa lao kwa namna yoyote ile. tuamke watanganyika.
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,200
2,000
tulifanya mambo mengi sana,.mengine mazuri mengine ya kijinga,tatizo lenu mnaacha mazuri mnachukua ya kijinga-jk nyerere

Kweli binadamu kuwaridhisha kazi sana! Pamoja na uzalendo aliouonesha Nyerere, umoja alioujenga, ambao hata wao wameshindwa hata kujenga ndoa zao ziwe na umoja, watu wanatafuta mabaya tuuuu! Kaazi kweli kweli!
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,778
2,000
kila nikitafakari kilichofanyika kwenye muungano bado nakosa jibu. Nilijiunga ccm mwaka 1980 nikiwa mwaka wa mwisho chuo kikuu cha dar es salaam.wakati huo,ccm ilikuwa chini ya uenyekiti wa baba wa taifa,mwl. Julius kambarage nyerere. Mambo ya nyerere bado siyaelewielewi.

Mwaka 1964,nikiwa na umri wa kutosha lakini wa ujana,nilishuhudia muungano huu wa sasa. Nilishuhudia kuchanganywa udongo wa jamhuri ya tanganyika na jamhuri ya watu wa zanzibar. Udongo huo ukaua nchi husika. Ukazaa nchi moja: Tanzania. Ilikuwa ni tarehe 26/4/1964,miezi mitatu baada ya mapinduzi ya zanzibar.

usanii

nyerere aliiua kabisa tanganyika na kuiacha zanzibar ndani ya tanzania. Tanganyika ikabatizwa jina la tanzania bara. Kemia aliyotumia nyerere ndiyo inayonichanganya. Muungano huu ulikuwa wa namna gani ikiwa nchi sasa zimekuwa tatu huku moja ikiwa imekufa? Yaani, tanganyika+zanzibar=tanzania + tanzania bara+zanzibar.ukitaka kuziona nchi hizi tatu ni rahisi. Fuatailia challenge kule uganda halafu subiria michuano ya kombe la dunia au mataifa ya afrika. Utaziona timu za tanzania bara,zanzibar na tanzania.pia,angalia serikali zilizopo.kuna wizara za tanzania,zipo za zanzibar na pia za tanzania bara. Kwa mfano,kuna wizara ya miundombinu ya tanzania bara na ile ya zanzibar.hakuana ya tanzania.

Kemia gani hii jamani? Huu si usanii uliotukuka uliofanywa na mzalendo wetu nyerere? Nini kilitokea hapa? Huwa kichwa kinaniumaheshima yako tupa tupa,,umongea vyema sana,,

nakubaliana naww kwa usanii wa hali ya juu wa ndugu juluis,,

ila nionavyo mimi,,tanganyika + zanzibar = tanzania bara + tanzania visiwani(zanzibar i.e unguja + pemba)
hiyo haswa ndiyo tafsiri yake
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,263
2,000
We kijana maswali magumu namna hiyo humu huwa hayaulizwi,,,,,,we waulize wazanzibar watakujibu lakini hawa vijana wagonjwa wa chademaliasis wanaugonnjwa wa kupenda chongo huita kengeza

Haha, wazaibar mnapotea huku mkiwa na matumaini.Na nyie pia mnaihofia CDM huku haijaweka mguu rasmi huko?AU ndio kwa vile CUF imekandamizwa.
 
Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
2,000
Watu wengi wamepotosha nakupindisha ukweli, dhumuni la mwalimu na waambata wake lilikuwa kuwa na NCHI moja tu ambayo ni Tanzania,

Zanzibar ulisimama kama mkoa tu baada ya Muungano.

Wapinga muungano wametufikisha hapa tulipo na mwisho watauvunja kabisa.
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
2,000
Kila nikitafakari kilichofanyika kwenye muungano bado nakosa jibu. Nilijiunga CCM mwaka 1980 nikiwa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Wakati huo,CCM ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Baba wa Taifa,Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mambo ya Nyerere bado siyaelewielewi.

Mwaka 1964,nikiwa na umri wa kutosha lakini wa ujana,nilishuhudia Muungano huu wa sasa. Nilishuhudia kuchanganywa udongo wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Udongo huo ukaua nchi husika. Ukazaa nchi moja: Tanzania. Ilikuwa ni tarehe 26/4/1964,miezi mitatu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.

Usanii

Nyerere aliiua kabisa Tanganyika na kuiacha Zanzibar ndani ya Tanzania. Tanganyika ikabatizwa jina la Tanzania Bara. Kemia aliyotumia Nyerere ndiyo inayonichanganya. Muungano huu ulikuwa wa namna gani ikiwa nchi sasa zimekuwa tatu huku moja ikiwa imekufa? Yaani, Tanganyika+Zanzibar=Tanzania + Tanzania Bara+Zanzibar.Ukitaka kuziona nchi hizi tatu ni rahisi. Fuatailia Challenge kule Uganda halafu subiria michuano ya kombe la dunia au mataifa ya Afrika. Utaziona timu za Tanzania Bara,Zanzibar na Tanzania.Pia,angalia Serikali zilizopo.Kuna Wizara za Tanzania,zipo za Zanzibar na pia za Tanzania Bara. Kwa mfano,kuna Wizara ya Miundombinu ya Tanzania Bara na ile ya Zanzibar.Hakuana ya Tanzania.

Kemia gani hii jamani? Huu si usanii uliotukuka uliofanywa na mzalendo wetu Nyerere? Nini kilitokea hapa? Huwa kichwa kinaniuma
Samaani lakini Mzeeee !!!!!!!!! [natumia usemi wa kijana mwenzangu elmaalufu kama Mzee wa gossip Soud Cop] kwa ulivyojieleza wewe una umri wa kunizaa.Hivyo kwa heshima hiyo nastahiki kutumia lugha ya staha japo swali lako na kwa umri wako naona da wakati mwingine ndio maana tupo hapa tulipofika kwa kuwa mimi leo namwelewa Mwalimu japo pia kuna yale nayoyakubali na kunaninayayo pishana nayo toka kwake, lakini nakubaliana nae kwa mengi japo mimi ni muumini wa bidii binafsi ila zisizoegmea dhuluma.

Daima watu wote wanao think outside the box wanajua hili:
THERE ARE THREE KIND OF PEOPLE IN THE WORLD
1: Those who make things happen [Like Mwalimu Nyerere]
2: Those who wonder what happen - kupitia kauri yako hii "kwenye muungano bado nakosa jibu."
3: Those who don't know what happen.
Mwalimu alikuwa na upeo wa kujenga kitu ambacho kinafanana na mazingira yetu kulingana na nyakati za zama husika.Na sisi wa sasa hivi tumekuwa waumini wa kucopy mambo ya wengi kwa kuwa tumesoma darasani hivyo kutufanya kuendesha mambo ya Taifa letu kwa kusoma vitabu vilivyo andikwa na watu kama theories na kuzigeuza kuwa ndio jibu kumbe tulipaswa kujifunza idea kisha nasi kuibuka na chetu kokote duniani hakipo na kipo kwetu na kimefanikiwa na kinafanya kazi, kisha wengine toka kwingine waje kujifunza ni vipi chetu kimefanya kazi.

Kawaulize Kenya walituliaje pale walipomaliza uchaguzi ulioisha na kusababisha mauji ya raia wa kenya wapatao 1000.Nini JK aliwaambia wafanye na wakafanikiwa na kumaliza tofauti zao na leo hii wanaenda uchaguzi mwingine.Sio lazima tuwe kama wao [hao wengine unaowatafuta kuona muungano wao] bali sisi na Zanzibar tunaweza kuwa sisi na wengine huko wakatushangaa kuwa imewezekanaje kwenu!!!!Nasaba za wanzaibar na watanzania bara zinajulikana,kuwa kuna wasukuma, wanyamwezi, waha, wanyakusa na wanyasa.
 
Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
0
Kila nikitafakari kilichofanyika kwenye muungano bado nakosa jibu. Nilijiunga CCM mwaka 1980 nikiwa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Wakati huo,CCM ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Baba wa Taifa,Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mambo ya Nyerere bado siyaelewielewi.

Nilipo RED.

Hapo ahali yangu ukusema Kweli.

Kwani miaka hiyo sote tulikuwa hapo UDSM. Haikuwezekana mwanafuzni yoyote kuruhusiwa UDSM bila kuwa mwanachama wa CCM. Na kwa wakti huo ulitakiwa kuhudhuria madarasa maalum ya kufundiswa Katiba ya chama kwa miezi Mitatu kabla kupewa kadi. Wengi tuliofanikiwa kujiunga UDSM tuliotokea maskulini moja kwa moja au katika vyuo mbalimbali tulipata mafunzo hayo tukiwa JKT kwani huko kulikuwa na PEO (Political Education Officers) ambao walitufunza na mwisho tulipewa Kadi za CCM.

Moja ya kigezo cha kujiunga na Chuo kikuu ilikuwa ni kuonyesha Kadi ya CCM. na hilo lilikuwa moja ya kigezo vile vile cha kupata Passport n.k.

Kuwa mkweli hali yangu kwani kuna wengi wanaosoma hapa.
 
sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
2,000
Samaani lakini Mzeeee !!!!!!!!! [natumia usemi wa kijana mwenzangu elmaalufu kama Mzee wa gossip Soud Cop] kwa ulivyojieleza wewe una umri wa kunizaa.Hivyo kwa heshima hiyo nastahiki kutumia lugha ya staha japo swali lako na kwa umri wako naona da wakati mwingine ndio maana tupo hapa tulipofika kwa kuwa mimi leo namwelewa Mwalimu japo pia kuna yale nayoyakubali na kunaninayayo pishana nayo toka kwake, lakini nakubaliana nae kwa mengi japo mimi ni muumini wa bidii binafsi ila zisizoegmea dhuluma.

Daima watu wote wanao think outside the box wanajua hili:
THERE ARE THREE KIND OF PEOPLE IN THE WORLD
1: Those who make things happen [Like Mwalimu Nyerere]
2: Those who wonder what happen - kupitia kauri yako hii "kwenye muungano bado nakosa jibu."
3: Those who don't know what happen.
Mwalimu alikuwa na upeo wa kujenga kitu ambacho kinafanana na mazingira yetu kulingana na nyakati za zama husika.Na sisi wa sasa hivi tumekuwa waumini wa kucopy mambo ya wengi kwa kuwa tumesoma darasani hivyo kutufanya kuendesha mambo ya Taifa letu kwa kusoma vitabu vilivyo andikwa na watu kama theories na kuzigeuza kuwa ndio jibu kumbe tulipaswa kujifunza idea kisha nasi kuibuka na chetu kokote duniani hakipo na kipo kwetu na kimefanikiwa na kinafanya kazi, kisha wengine toka kwingine waje kujifunza ni vipi chetu kimefanya kazi.

Kawaulize Kenya walituliaje pale walipomaliza uchaguzi ulioisha na kusababisha mauji ya raia wa kenya wapatao 1000.Nini JK aliwaambia wafanye na wakafanikiwa na kumaliza tofauti zao na leo hii wanaenda uchaguzi mwingine.Sio lazima tuwe kama wao [hao wengine unaowatafuta kuona muungano wao] bali sisi na Zanzibar tunaweza kuwa sisi na wengine huko wakatushangaa kuwa imewezekanaje kwenu!!!!Nasaba za wanzaibar na watanzania bara zinajulikana,kuwa kuna wasukuma, wanyamwezi, waha, wanyakusa na wanyasa.

Wewe kwa jinsi ulivyoanza mwanzoni nashawishika kuamini wewe ni kijana mdogo na Mungu amekufungulia kuyaona yale ambayo wamefichwa wazazi na mababu zako..Mungu akujalie ukue katika kimo na busara.. Japo kuna mapungufu madogo madogo katika huu muungano but its framework it is amazing,haipo kokote na hapo ndo nakomwona nyerere alikua extraordinary person! Wapiinga muungano muelewe kwamba hakuna popote palipowahi kuwa na utengano watu wakaendelea!
 
  • Thanks
Reactions: DSN

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
0
Watu wengi wamepotosha nakupindisha ukweli, dhumuni la mwalimu na waambata wake lilikuwa kuwa na NCHI moja tu ambayo ni Tanzania,

Zanzibar ulisimama kama mkoa tu baada ya Muungano.

Wapinga muungano wametufikisha hapa tulipo na mwisho watauvunja kabisa.

Si kweli kabisa. Kwani Znz ilikuwa nchi toka enzi za Nyerere na ndio maana kukawa na Serikali ya mapinzuzi Ya Znz ambayo rais wake alikuwa KARUME ambaye pia alikuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Muungano wa Tanzania.

Tuwe wakweli na sio kusema usichokijua.

Pole sana

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,601
2,000
...Na kwa wakti huo ulitakiwa kuhudhuria madarasa maalum ya kufundiswa Katiba ya chama kwa miezi Mitatu kabla kupewa kadi...
Hapa unapotosha. Ni madarasa gani hayo "maalum" unayozungumzia? Tupo wengi tuliokuwepo enzi hizo!
 
Oct 18, 2012
87
70
Watu wengi wamepotosha nakupindisha ukweli, dhumuni la mwalimu na waambata wake lilikuwa kuwa na NCHI moja tu ambayo ni Tanzania,

Zanzibar ulisimama kama mkoa tu baada ya Muungano.

Wapinga muungano wametufikisha hapa tulipo na mwisho watauvunja kabisa.

MUUNGANO WA WATU WA ZANZIBAR NA BARA NI VIGUMU KUVUNJIKA ...Umekuwepo miaka mingi kabla ya wakoloni...na ukastawishwa na biashara zilizokuwepo miaka hiyo .ndio maana tuna watu wa kusini( mikoa ya ruvuma,mbeya,mtwara,lindi) wengi kule unguja mpaka Pemba.
MUUNGANO unaoweza kurekebishwa au kuvunjika ni huo wa kisiasa

Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,146
2,000
Nilipo RED.

Hapo ahali yangu ukusema Kweli.

Kwani miaka hiyo sote tulikuwa hapo UDSM. Haikuwezekana mwanafuzni yoyote kuruhusiwa UDSM bila kuwa mwanachama wa CCM. Na kwa wakti huo ulitakiwa kuhudhuria madarasa maalum ya kufundiswa Katiba ya chama kwa miezi Mitatu kabla kupewa kadi. Wengi tuliofanikiwa kujiunga UDSM tuliotokea maskulini moja kwa moja au katika vyuo mbalimbali tulipata mafunzo hayo tukiwa JKT kwani huko kulikuwa na PEO (Political Education Officers) ambao walitufunza na mwisho tulipewa Kadi za CCM.

Moja ya kigezo cha kujiunga na Chuo kikuu ilikuwa ni kuonyesha Kadi ya CCM. na hilo lilikuwa moja ya kigezo vile vile cha kupata Passport n.k.

Kuwa mkweli hali yangu kwani kuna wengi wanaosoma hapa.
Uko sahihi mkuu,bila shaka nawe ulikuwa unachukua shahada ya kwanza?
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
2,000
Hivi aliyeunganisha nchi mbili ni Mwl. Julius Nyerere peke yake?. Mbona watu hawamtendei haki Sheik Abeid Karume. Kitu ninachoshindwa kuelewa ni pale linapokuja swala la muungano na anayeongelewa ni Mwl. Julius Nyerere peke yake. Hivi huu muungano ungekuwepo kama Sheik Abeid Karume asingehusishwa na kukubaliana katika mapendekezo.

Hebu kwanza tuwe fair kabla ya kuanza kuongelea muungano kwa undani.

Mada yako ingekuwa imebeba maana kamili kama ungesema NYERERE NA KARUME ni "WASANII" badala ya hiyo heading yako. Au ndiyo yale ya catchphrase kwanza maelezo baadaye.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom