mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,775
- 2,198
Ninakubalina na wewe korosho ni zao kuu la biashara barabara ya lami ilipaswa kuwa kusiniKiuchumi, ukiweka lami eneo ambalo lina mazao ya uchumi, uwekezaji huo unaweza kuongeza uchumi na mapato, kiasi cha kukuwezesha kuendelea kuongeza miundombinu mpaka sehemu ambazo hazina mazao ya uchumi.
Kwa hiyo, ingawa sehemu zote zinaweza kuwa zinatakiwa kuletewa maendeleo kama barabara ya lami, lakini sehemu zinazozalisha sana zikipewa kipaumbele, kwa kuwa kipaumbele hicho kitaongeza uzalishaji, utakuwa unarahisisha na unaharakisha maendeleo ya sehemu zote kwa kuanza na sehemu hizi.
Kiswahili tunasema "Kupanga ni kuchagua". Ukianza kuweka barabara ya lami sehemu wanayolima mihogo, badala ya sehemu wanayochimba dhahabu, utashindwa kurahisisha uchimbaji wa dhahabu, ambao utasaidia sana hata kukuwezesha kuweka lami sehemu kumi zinazolima mihogo kwa haraka Zaidi.
Nafikiri ndicho alichokataa Nyerere hicho. Si kwamba alikataa Butiama kusiwe na maendeleo.
Ila, kwa nchi yenye sehemu nyingi zenye uwezekano wa kuwa na mazao yenye kuongeza uchumi sana Zaidi ya Butiama, kwa nini aanze kuweka lami Butiama, lami ambayo haitakuwa na uzalishaji wowote, wakati anaweza kuweka lami sehemu nyingine, ikawa na uzalishaji mzuri utakaosaidia kuweka lami sehemu kumi kama Butiama?
Ukisoma kitabu cha Maisha ya awali ya Nyerere "Nyerere: The Early Years" cha Dr. Thomas Molony wa Edinburgh aliposomea Nyerere, utasoma mpaka Nyerere alivyokuwa Edinburgh alisoma nini, papers alizoandika zilihusu nini. Mmmoja kati ya wanafalsafa ambao Nyerere alimsoma sana na kuandika sana insha juu yake ni John Stuart Mill.
John Stuart Mill alikuwa ni Utilitarianist. Utilitarians wanaamini katika kanuni ya "The greater good for the greater number of people". Yani, ufanye jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi.
Kwa kanuni hizi za kufanya jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi, kuanza kuleta maendeleo sehemu zenye kuweza kujenga uchumi Zaidi kunafaa watu wengi Zaidi ya kujenga sehemu ambazo zina watu wachache na kuzijenga hakuwezi kufaidisha watu wengi Zaidi.
Ndiyo maana Nyerere akauliza, ajenge lami Butiama kuna zao gani?
Ahsante sana kwa uchambuzi mzuri.Kiuchumi, ukiweka lami eneo ambalo lina mazao ya uchumi, uwekezaji huo unaweza kuongeza uchumi na mapato, kiasi cha kukuwezesha kuendelea kuongeza miundombinu mpaka sehemu ambazo hazina mazao ya uchumi.
Kwa hiyo, ingawa sehemu zote zinaweza kuwa zinatakiwa kuletewa maendeleo kama barabara ya lami, lakini sehemu zinazozalisha sana zikipewa kipaumbele, kwa kuwa kipaumbele hicho kitaongeza uzalishaji, utakuwa unarahisisha na unaharakisha maendeleo ya sehemu zote kwa kuanza na sehemu hizi.
Kiswahili tunasema "Kupanga ni kuchagua". Ukianza kuweka barabara ya lami sehemu wanayolima mihogo, badala ya sehemu wanayochimba dhahabu, utashindwa kurahisisha uchimbaji wa dhahabu, ambao utasaidia sana hata kukuwezesha kuweka lami sehemu kumi zinazolima mihogo kwa haraka Zaidi.
Nafikiri ndicho alichokataa Nyerere hicho. Si kwamba alikataa Butiama kusiwe na maendeleo.
Ila, kwa nchi yenye sehemu nyingi zenye uwezekano wa kuwa na mazao yenye kuongeza uchumi sana Zaidi ya Butiama, kwa nini aanze kuweka lami Butiama, lami ambayo haitakuwa na uzalishaji wowote, wakati anaweza kuweka lami sehemu nyingine, ikawa na uzalishaji mzuri utakaosaidia kuweka lami sehemu kumi kama Butiama?
Ukisoma kitabu cha Maisha ya awali ya Nyerere "Nyerere: The Early Years" cha Dr. Thomas Molony wa Edinburgh aliposomea Nyerere, utasoma mpaka Nyerere alivyokuwa Edinburgh alisoma nini, papers alizoandika zilihusu nini. Mmmoja kati ya wanafalsafa ambao Nyerere alimsoma sana na kuandika sana insha juu yake ni John Stuart Mill.
John Stuart Mill alikuwa ni Utilitarianist. Utilitarians wanaamini katika kanuni ya "The greater good for the greater number of people". Yani, ufanye jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi.
Kwa kanuni hizi za kufanya jambo litakaloleta manufaa kwa watu wengi Zaidi, kuanza kuleta maendeleo sehemu zenye kuweza kujenga uchumi Zaidi kunafaa watu wengi Zaidi ya kujenga sehemu ambazo zina watu wachache na kuzijenga hakuwezi kufaidisha watu wengi Zaidi.
Ndiyo maana Nyerere akauliza, ajenge lami Butiama kuna zao gani?
Ahsante sana kwa uchambuzi mzuri.
Our times are different from Nyerere's time. Whether we like or not, we need to connect the whole country in such a way that we can have better options, when it comes to tapping the resources and other opportunities.
Nyerere aliisahau kabisa Lindi na Mtwara sababu ya security wakati ule. Leo ni tofauti.
Kama means za kusukuma maendeleo zikisambazwa Tanzania nzima, umaskini utapungua na fursa zitakuwa rahisi kwa kila mwananchi.
Tusifikirie kama tupo kwenye box. Tanzania is evolving like any other country