Jamhuri ya Zanzibar
Senior Member
- Jul 17, 2012
- 126
- 195
Picha ya Kwanza:
Rais Abeid Amani Karume wa Zanzibar akiwa na Rais Gamal Abdel Nasser wa Misri mara baada ya kiongozi huyo kuwasili Zanzibar kwa ziara rasmi tarehe 24 Septemba, 1966 ndani ya Muungano. Kushoto kwa Mzee Karume anaonekana Brigadier General Yussuf Himid. Leo hii sio tu Rais wa Zanzibar hana hadhi ya kukagua gwaride na kiongozi wa kigeni nchini lakini pia Zanzibar haina hata hadhi ya kufikiwa na mgeni huyo. Hayo ndio yaliyokuwa wakati wa Rais Obama na wakati wa ziara ya Mwai Kibaki ya kuwaaga watanzania. Rais wa Zanzibar alilazimika kwenda kupanga foleni na kushangilia mizinga uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.
Picha ya Pili:
Malkia Elizabeth II wa Uingereza akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar Sheikh Aboud Jumbe mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwa ziara rasmi katika visiwa hivi mwaka 1979.
Hadi wakati huo zilibakia angalau alama kama hizo za Muungano wenye heshima, haki na usawa kati ya Zanzibar na Tanganyika.
Sasa mambo yamegeuka. Badala ya Wakuu wa Madola ya kigeni kutembelea Zanzibar, kupokelewa rasmi kwa gwaride na kupigiwa mizinga 21 huku Wimbo wa Taifa wa Zanzibar na ule wa nchi ya Mkuu anayetutembelea zikipigwa kwa heshima, sasa Rais wa Zanzibar na wasaidizi wake hufunga safari kwenda Tanganyika kuwapokea Wakuu wa Nchi za Nje na kufanya nao mazungumzo yanayoihusu Zanzibar huko huko.
Hatuwezi tena kukubali udhalilishaji huu kuendelea. Hatuwezi tena kuwaachia Tanganyika udhibiti wa Mambo ya Nje yanayoihusu nchi yetu. Tumewaamini kwa miaka 50 sasa lakini wameshindwa kuonesha uaminifu.
Tunataka kuona suala la Mambo ya Nje linaondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano na linasimamiwa na nchi washirika wenyewe kila nchi kati ya Zanzibar na Tanganyika kwa upande wake.
Picha ya Tatu:
Tofauti kati ya Serikali mbili za Karume na zilizopo sasa ambazo zimeipora Zanzibar hadhi yake. Nyerere na Karume walikagua gwaride kwa pamoja wakati wa sherehe za Muungano na sio peke yake. Hivi sasa mwenye hadhi hiyo ya kukagua jeshi wakati wa sherehe za Muungano ni Rais wa Jamhuri ya Muungano pekee.