Nyerere mzee wa mikakati gwiji na mahiri wa siasa Afrika

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,168
33,439
Alikua ni dokta,injinia,askari,muumini,mwanafalsafa, mwanasiasa,mwanausalama,mwanamichezo na mwanaharakati nk.

Wakati wa utawala wake tuliona nchi zikikombolewa toka wakoloni kulikuwa na makambi ya wapigania uhuru na haki wa ANC, PAC, FRELIMO ,SWAPO ,SAHARA Magharibi,(PLO) nk.

Michezo, Tz iliwika ktk soka t Stars ilicheza kombe kubwa la Afrika,mkumbuke Filbert Bayi ktk riadha,kumbuka ndondi,kumbuka wanamuziki kama Mbaraka.

K
umbuka wanasiasa mahili kama Sokoine,Salim ,Malechela wakati huo.

Kumbuka wababe wa vita kama Mayunga, Msuguri ,Maafudhi,Kimario, Warden, Kiwelu nk,pia kumbu majasusi wa tz walivyoweza kuwabana majasusi wa makaburu Amini Banda nk.

Kumbuka elimu yetu wanadiplomasia wetu UN, NAM, OAU.

Kumbuka utaifa wetu kupitia Halaiki, Mgambo,JKT.

Kumbuka nchi hatukubaguana kikabila wala kidini,Mzee yule alikuwa binadamu alikuwa ana maadui zake lakini ali deal nao peaceful.

Alivuna maliasili chache za nchi kwa manufaa ya nchi.Hakujilimbikizia mali binfsi wala ya taifa.je huyu sio mahili?

Ninaposema alikua dokta maana yangu huduma za afya zilikua bure na bora,alikuwa injinia wote mnajua juu ya viwanda vya siri na nyeti,askari maana yake usalama wa nchi ndani na nje ulikuwa imara nk.hayo ni machache tu unaweza ongeza unayokumbuka lakini unaweza pinga.

Ni mtazamo wangu tu,nawasilisha.
 
Alikuwa kiongozi aliyewapenda watu na watu walimpenda, mjenzi mahili wa hoja asiyeogopa majadiliano hata kwenye hoja nzito ambazo viongozi wa sasa wamekuwa waoga kuijadili kama ya udini, ukabila nk. Hakuwa mbaguzi wa kujali kwake kama hawa tulionao kama angekuwa hivyo kwa miaka zaidi ya 20 kama kiongozi wa juu kabisa nchini Butiama kungekuwa bora sana kulinganisha na ilivyo sasa au na wilaya nyingine.

Nyerere, mkulima wa kawaida aliyezungukwa na utajiri wa nchi ambao aliamini mali za nchi sio zake binafsi ni za wote na yeye amepewa dhamana tu ya kuzilinda kwa faida ya sasa na ya baadae, mwanauchumi aliyeanzisha viwanda vilivyoajiri maelfu ya watanzania na kufanya ajira lisiwe tatizo zito kama ilivyo sasa. Baba wa wengi na babu kwa vijana wa sasa ambaye alitamani kuona wajukuu zake wakiinuka kiasi akajinyima starehe kwa faida ya kizazi cha mbele asichokiona..

Niseme nini? Binadamu tumetofautiana, japo kila mmoja ana udhaifu lakini bado viwango vya udhaifu wetu havipo sawa, ukweli ni kwamba aina yake ni ya kipekee
 
Nyerere baaba mlezioo Nyerere baabaa mwanamapinduzioo Mengi mmesema bado huyu hana mfanowe...
 
Alinifurahisha jinsi alivyojitolea kulijenga kanisa Katoliki kwa uwezo wake wote.Pumzika Baba Mwanaheri
 
Mada hii imenikumbusha mengisana juu ya mwalimu Nyerere. Kuna wakati Kalinali Lugambwa alitaka kugombea Upapa, lakini alipoenda kumwambia mwalimu, alimshauri kuachana na habari hiyo kwani wazungu wasingekubali kuongozwa na mtu mweusi! Hivyo alimwambia "watakuua hachana na kinyanganyiro hicho" . Hii inaonesha kwamba mbali na uwezo wake wa kufikiri haraka Nyerere alikuwa na maono.
 
alinifurahisha jinsi alivyotaifisha shule za dini ili watanzania wote kwa pamoja waweze kusoma bila kujali dini zao.nyingi ya shule hizo zilikua za makanisa ila nyingi zaidi zilikua za wakatoliki.bila hivyo sijui leo ingekuaje.
 
Tatizo la mada kama hizi, mtatutaka sote tukubaliane kwa 100% na mawazo yenu, yaani wote tuimbe NDIYO! NDIYO! NDIYO!tukisema kinyume na imani yenu; utasikia UNA CHUKI BINAFSI!!
 
Mkimsoma na kumchambua Nyerere mtasikitika!,maovu yake ambayo siku hizo yalifanywa kwa siri na kufichwa na utawala wake wa kidikteta!, kwa kuwa Mwalimu alidhibiti vyombo vya habari vyote, hakuna aliyethubutu kuhoji, wala kujuwa undani wa maovu ya rushwa, ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanana na tawala nyingi za kidikteta za kiafrika wakati huo.

Udikteta wa Nyerere wa kudhibiti wapinzani wa serikali na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kwa ukatili wa namna kama hizo yaliyowakuta akina Ludovik Mwijage na wenzakeMkuu hii ukiisoma humtamani Nyerere, jamaa kaelezea karibu mambo yote maovu ya Mwalimu ambayo siku hizo yalifanywa kwa siri na kufichwa na utawala wa kidikteta wa Mwalimu, kwa kuwa Mwalimu alidhibiti vyombo vya habari vyote, hakuna aliyethubutu kuhoji, wala kujuwa undani wa maovu ya rushwa, ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanana na tawala nyingi za kidikteta za kiafrika wakati huo.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...mwijage-the-dark-side-of-nyereres-legacy.html
 
Acheni porojo. Yawekeni na vilelezo vyake hapa. Kudhibiti wachafuzi wa hali ya amani na mshikamano ni udikteta wa kulinganisha na madoikteta kama kina Amin?

Wekeni ushahidi hapa.
 
Alinifurahisha jinsi alivyojitolea kulijenga kanisa Katoliki kwa uwezo wake wote.Pumzika Baba Mwanaheri
Alinifurahisha na namna alivyogawa elimu kwa watu wote waislam kwa wakristo bure, matibabu, uhuru wa kuabudu nk. Lakini alinifurahisha zaidi alipokuwa akiwapa Bakwata viwanja na majengo sehemu mbalimbali katika nchi hii kama vile markaz pale chango'ombe, jamiat kule bukoba, pale biafra nk ili wajenge shule na vyuo na pia kujiendeleza na huku akiwanyima wakristo na kuwaacha wajinunulie wenyewe kwa kuwa aliamini wao tayari wanazo hata kama hawakupewa na serikali, huzuni yangu ni kwamba waliopewa badala ya kujiendeleza wao wanatifuana ngumi na wengine wako ndani
 
Nje ya Tanzania anajulikana kama msaliti tu...aliitelekeza Pan Africanism na kuuweka mfumo wa Kikatoliki nchini mwake.

Wanaijeria hawamsahau jinsi alivyoshiriki kuigawanya nchi yao kule Biafra.

Nkrumah na wafuasi wake wanamuona ni kibaraka wa Wazungu tu.
 
Alikua ni dokta,injinia,askari,muumini,mwanafalsafa, mwanasiasa,mwanausalama,mwanamichezo na mwanaharakati nk.

Wakati wa utawala wake tuliona nchi zikikombolewa toka wakoloni kulikuwa na makambi ya wapigania uhuru na haki wa ANC, PAC, FRELIMO ,SWAPO ,SAHARA Magharibi,(PLO) nk.

Michezo, Tz iliwika ktk soka t Stars ilicheza kombe kubwa la Afrika,mkumbuke Filbert Bayi ktk riadha,kumbuka ndondi,kumbuka wanamuziki kama Mbaraka.

K
umbuka wanasiasa mahili kama Sokoine,Salim ,Malechela wakati huo.

Kumbuka wababe wa vita kama Mayunga, Msuguri ,Maafudhi,Kimario, Warden, Kiwelu nk,pia kumbu majasusi wa tz walivyoweza kuwabana majasusi wa makaburu Amini Banda nk.

Kumbuka elimu yetu wanadiplomasia wetu UN, NAM, OAU.

Kumbuka utaifa wetu kupitia Halaiki, Mgambo,JKT.

Kumbuka nchi hatukubaguana kikabila wala kidini,Mzee yule alikuwa binadamu alikuwa ana maadui zake lakini ali deal nao peaceful.

Alivuna maliasili chache za nchi kwa manufaa ya nchi.Hakujilimbikizia mali binfsi wala ya taifa.je huyu sio mahili?

Ninaposema alikua dokta maana yangu huduma za afya zilikua bure na bora,alikuwa injinia wote mnajua juu ya viwanda vya siri na nyeti,askari maana yake usalama wa nchi ndani na nje ulikuwa imara nk.hayo ni machache tu unaweza ongeza unayokumbuka lakini unaweza pinga.

Ni mtazamo wangu tu,nawasilisha.

Mambo ya Mlm Nyerere nchini kwetu ni kama dini, kuna watu wanaamini Mungu yupo na kuna watu wanaoamini hakuna Mungu, hawa watu wawili huwezi kuwafanya au kuwashawishi wakakubaliana hata siku moja, kila mmoja ana sababu zake nyingi tu za kwa nini anaamini hivyo, vivyo hivyo mambo ya Bw. Nyerere, kwa baadhi alikuwa mkombozi wa kweli mwenye hizo sifa ulizo orodhesha, na kwa wengine alikuwa Dikteta, Mbinafsi, na mwenye Chuki, mpenda Vita, aliyetuachia madeni, Muongo alitudangaya mengi, n.k

Acha kabisa mkuu....mwal. nyerere alikuwa Nabii alijenga hoja kwa kunukuu misahafu ya dini na alibashiri mengi yanayotokea(ukabila ,udini na anguko la CCM) pia alikuwa msanifu majengo(kaone mji wa sumbawanga na vijiji vya ujamaa mkoa wa Rukwa ...mpaka gazeti mwanahalisi wamewahi kuripoti kuwa wamemwona nyerere sumbawanga wakiwa na maana ya mpangilio wa mji na vijiji vya ujamaa), pia alikuwa kauli ya turufu kwa mataifa ya maghalibi kumbuka msimamo wake kuhusu benki ya dunia na IMF......mungu mrehemu....
 
Ntafurahi sana nikipata ukweli kuhusu Kambona....tukiachana napropaganda ambazo pia zilichangia kuitwa mhaini
nadhani matatizo haya yakuiona serikali ya sasa ya ccm inawanyanyasa wapinzani chanzo ni baba yetu wa kwanza..!!!

Mkimsoma na kumchambua Nyerere mtasikitika!,maovu yake ambayo siku hizo yalifanywa kwa siri na kufichwa na utawala wake wa kidikteta!, kwa kuwa Mwalimu alidhibiti vyombo vya habari vyote, hakuna aliyethubutu kuhoji, wala kujuwa undani wa maovu ya rushwa, ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanana na tawala nyingi za kidikteta za kiafrika wakati huo.

Udikteta wa Nyerere wa kudhibiti wapinzani wa serikali na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kwa ukatili wa namna kama hizo yaliyowakuta akina Ludovik Mwijage na wenzakeMkuu hii ukiisoma humtamani Nyerere, jamaa kaelezea karibu mambo yote maovu ya Mwalimu ambayo siku hizo yalifanywa kwa siri na kufichwa na utawala wa kidikteta wa Mwalimu, kwa kuwa Mwalimu alidhibiti vyombo vya habari vyote, hakuna aliyethubutu kuhoji, wala kujuwa undani wa maovu ya rushwa, ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanana na tawala nyingi za kidikteta za kiafrika wakati huo.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...mwijage-the-dark-side-of-nyereres-legacy.html
 
Mambo ya Mlm Nyerere nchini kwetu ni kama dini, kuna watu wanaamini Mungu yupo na kuna watu wanaoamini hakuna Mungu, hawa watu wawili huwezi kuwafanya au kuwashawishi wakakubaliana hata siku moja, kila mmoja ana sababu zake nyingi tu za kwa nini anaamini hivyo, vivyo hivyo mambo ya Bw. Nyerere, kwa baadhi alikuwa mkombozi wa kweli mwenye hizo sifa ulizo orodhesha, na kwa wengine alikuwa Dikteta, Mbinafsi, na mwenye Chuki, mpenda Vita, aliyetuachia madeni, Muongo alitudangaya mengi, n.k

Huwezi wafanya wote wakawa na msimamo sawa ndio maana kuna timamau na wehu......Mi kwangu Mwal. Nyerere ni kama lulu,dhahabu,ID,Utaifa,Fahari,mwenye heri, mkombozi.....dah! sio hawa wezi wa sasa
 
Nje ya Tanzania anajulikana kama msaliti tu...aliitelekeza Pan Africanism na kuuweka mfumo wa Kikatoliki nchini mwake.

Wanaijeria hawamsahau jinsi alivyoshiriki kuigawanya nchi yao kule Biafra.

Nkrumah na wafuasi wake wanamuona ni kibaraka wa Wazungu tu.

Ni ushetani kuifananisha Nigeria na TZ .....unajua historia ya mapinduzi waliyopitia nigeria na Amani tuliyopitia.....watu wengine kila jambo kuhusisha na udini.......ni laana kufundisha ngumi na kunfuu kwenye nyumba za ibada unajua hilo.....
 
Huwezi wafanya wote wakawa na msimamo sawa ndio maana kuna timamau na wehu......Mi kwangu Mwal. Nyerere ni kama lulu,dhahabu,ID,Utaifa,Fahari,mwenye heri, mkombozi.....dah! sio hawa wezi wa sasa

Mfano wako sio sawa, huwezi kulinganisha mtu aliye na akili timamu na ambaye hana akili timamu, hawa ni watu wawili tofauti!

Mimi nimetolea mfano wa watu wawili wenye akili timamu kabisa, ambao huwezi kuwafanya wakaamini sawa, sasa wewe umetokea kuwa upande mmoja ambao unaamini yote hayo ulioyasema kuhusu Bw. Nyerere na una sababu zako si ajabu unaweza kujaza kitabu kuziandika, kuna mwingine pia atakuwa na mawazo tofauti atakuwa upande mwingine na yeye anaweza akakujazia kitabu kuhusu kwa nini kwake yeye Bw. Nyerere alikuwa ni mhalifu aliyestahili kuhumiwa kabla ya kufariki, na hapo hakuna jinsi, unaweza kumshawishi vinginevyo, ni mpaka pale tu Bw. Nyerere mwenyewe angekuwepo ndio angeweza kuyamaliza haya, maadamu hayupo n huu mjadala unabaki kuwa hauna maana!

Back
Top Bottom