Nyerere ana kashfa nzito hapo kwenye link chini, especially posts tatu za mwisho.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...oka-monduli-chuo-cha-jeshi-kwa-msukosuko.html
Mbona hatuzioni hizo kashfa!? nimeangalia hiyo thread ila sikuona kitu kama hiyo hebu tujuze! Au kutoa ile barua ya kumgrass Seyore??
Hususan rejea posts 118, 119,120 na kuendelea
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uo-cha-jeshi-kwa-msukosuko-6.html#post1671213
Hivi mnayajuwa ya Nyerere au mnasikiliza porojo zake za kwenye vibaraza vya kuchezea bao?
Hana jema aliloifanyia hii nchi. Lipi moja?
Hajaacha misingi imara ya kuendesha hii nchi kama aliacha ni ipi?
Hata katiba alizokuwa akiandika Ikulu na mawakili wake wabovu leo kila mTanzania hazitaki.
Hebu mmoja tu, anambie kitu kimoja kizuri alichofanya Nyerere zaidi ya kuongea sana na wanafiki kucheka hata pasipo chekesha.
Angekuwa na mawazo na fikra nzuri japo chembe, leo Tanzania na utajiri ilionao ingekuwa kwenye neema ya ajabu.
I do not see anything in this posting! Is it my problem???
Tunapomsifia nyerere, tunafanya hivyo kwa kumlinganisha na marais wengine tuliowahi kuwa nao na hata marais wengine wa afrika. Kwa kufanya hvyo utaona mengi mazuri aliyoyafanya, lakini pia utaona kwamba kulikuwa na mapungufu ktk utendaji wake, kama tulivyo binadamu wote. Tatizo wengine tumeaminishwa toka tukiwa wadogo kwamba adui yetu ni nyerere na hatupo tayari kuutafuta ukweli sisi wenyewe bila kuwa influenced na watu wengine, pamoja na elimu nzuri tuliyo nayo.
Huwezi kuwa na mafanikio kama hutambui na kuheshimu mafanikio ya watu wengine. Mpeni sifa zake mzee huyo, anastahili. Jilinganishe uwezo wako wewe na ule aliokuwa nao yeye alipokuwa umri wako! Mlinganishe nyerere na babu yako, halafu jiulize wewe na babu yako mmelifanyia nini taifa hili.
Kusema kweli hata mimi sioni kitu hapa kwangu. Nifanyeje ili nione (Unaweza hata kuni-PM kuhusu cha kufanya)
Natanguliza shukrani.
Ahsante sana LTC, ni wazi kabisa hatuna serikali, iliyopo inatumwa na kutumikia wenye mali! RIP baba wa Taifa letu!
Asante sana kwa maelezo haya, hakuna binadamu mkamilifu, sote tuna mapungufu. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!Majimshindo uko sahihi, na mimi nakubaliana na wewe. Wewe si mnafiki kama wengine kwasababu unasema unayoyafahamu na kuyaamini. Lakini, si lazima yawe ukweli wote (absolute truth). Haiwezekani kuwafanya watu wote kumtazama Nyerere kama kiongozi mzuri sana au mbaya sana.
Hata kwenye dini ni hivyo. Kuna watu wanasema Yesu ni Mwana wa Mungu, wengine wanasema ni Nabii tu. Wengine wanasema Mtume Mohamme (s.a.w) ni Nabii wa Mwisho wa Mungu, na wengine wanasema ni Nabii wa Uongo... mlolongo ni mrefu. Je ni nani yuko sahihi zaidi?
Kuna mambo mengi magumu, yatamngoja Mwenyezi Mungu kuja kuyatolea hukumu ya haki. Hapo hakutakuwa na ubishi. Sasa hivi tutaumiza vichwa bure tu.
Mimi kama mimi, namtazama Nyerere, kama kiongozi mmoja mwenye hekima ambazo hazimithiliki, na hafanani na viongozi wengi wa duniani na hususani wa-Tz. Siwezi kumlinganisha Mzee AH Mwinyi, Mzee BW Mkapa ama Mzee JM Kikwete na Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere.
Angalia yafuatayoNyerere, alikuwa binadamu, anayo makosa. Lakini alikuwa akisema tujisahihishe...Alipoondoka madarakani alisema tuyaache mabaya yake lakini mazuri tusiyatupe. Hata alikubali tuache Ujamaa lakini tubaki na Kujitegemea.. Bahati mbaya viongozi wetu wameshindwa kujifunza kutoka kwake. Wanataka kuwasikiliza mafisadi zaidi ya wananchi wao masikini. Hiyo ndio shida iliyopo
- Aliachia madaraka ya rais wakati watu na katiba vinaruhusu kuendelea kutawala
- Alirudi kijijini kwao kulima kwa jembe la mkono na kukokotwa na ng'ombe. Hakuna duniani kiongozi wa namna hiyo labda Uchina ya zamani
- Alijitoa kuelimisha watu wake bure ili wapate kujitambua na kujilinda dhidi ya mafisadi na mabeberu kutoka ndani na nje
- Aliwapa watu wake huduma ya afya bure, ili waweze kuwa na afya waijenge nchi yao
- Aliwakusanya watu wake ktk vijiji ili apate kuwahudumia kwa urahisi zaidi
- Alitaifisha shule za mission ili wanchi wake wa dini zingine kama waislam (ambao si dini yake) nao wapate kusoma, kuelimika ili wapate toa mchango wa kuijenga nchi yao
- Alilazimisha chama chake kuanzisha vyama vingi ili kusaidia nchi iende na wakati na pia kuweka mfumo wa checks and balance (ambao sasa unafanya kazi kama alivyotegemea)
- Alijitolea kusaidia mataifa jirani yaliyokuwa hayapata uhuru yaweze kujikomboa.
- Alizuia maliasili zetu ziendelee kubaki salama hadi hapo tutakapopata utambuzi wa kutosha kuzisimamia ili ziweze kunufaisha uchumi na maisha yetu. Hapo alikataa kuwa kama Mobutu Seseko aliyejilimbikizia mali na wananchi wake wakawa masikini
- Alikataa kuwa na mahusiano na Israel waliokuwa wakwaonea wananchi Wapalestina
- Alipingana hata na Wajerumani, Waingereza waziwazi pale walipokuwa na misimamo ya ubaguzi au uonevu kwa binadamu wengine.
- Alikuwa hana unafiki, na alikuwa yupo tayari kukemea hata taifa kubwa la America lilipochukua msimamo wa kukandamiza mataifa madogo na masikini kwa sababu za kimabavu tu.
- .... orodha ni ndefu sana
Kuna wakati nilipokuwa nikisoma chuo kikuu hapo Dar es slalaam, nilianza kupinga sana siasa zake za Ujamaa na Kujitegemea. Sio kusema zilikuwa si sahihi, bali niliona zilianza kuleta matabaka kati ya wtawala (CCM) na raia, jambo ambalo limedumu mpaka leo. Vile vile niliona kuwa itikadi yake ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa na mapungufu mengi na isingeweza kufanikiwa kama vile ilivyokuwa katika jamii yetu. Nilikuwa nimejazwa kichwani mwangu fikra za Marx na Lenin na ukommunisti. Hata hivyo namheshimu sana kwa misingi ambayo alitujengea na kutuwezesha wengine kusma hadi chuo kikuu na kupata shahada zaidi ya moja, kitu ambacho sikuhizi ingekuwa shida.
naomba katika familia/kizazi cha mwalimu jk nyerere apatikane anayemfanana kwa upendo, uzalendo, akili na busara. Itakuwa ni hazina kubwa kwa taifa!!!
Asante sana kwa maelezo haya, hakuna binadamu mkamilifu, sote tuna mapungufu. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
Sio rahisi ku break through kama mfumo wenyewe ni kama huu! no matter how talented or educated you are! Mafisadi rules na ni kweli lazima kuna walio na talent kama hii au hata kumzidi mwalimu to be honest! lakini mmhh!wapo tena wapo vizuri tu....ila hawapewi nafasi kutokana na mfumo tuliona
Mahesabu na LTC Cometh the hour cometh the man/woman. Msitumie sababu ya current situation kua ni hindarance ya kutoa mtu/watu wenye uwezo,its pathetic reasoning. Sijui hata nianze vp kuwaonyesha fallacy ya reasoning yenu maana it is precisely these situations that are convinient for the 'great' to push through.