Kama huko uliko baba yetu wa Taifa unasoma mawazo haya ya watoto wako uliotuacha huku tukiwa na amani na utulivu uliotukuka, basi naomba usome hapa kwa umakini mkubwa. Yule kijana ambae ulituambia bado mdogo na sasa amekuwa na akapanga kwenye lile jumba jeupe pale magogoni anawanyanyasa wafanyakazi. Hataki kuwasikiliza anawakejeli kama vile wakimbizi katika Ardhi yao uliyoikomboa toka kwa wakoroni.
Habari iko hivi: Mwezi wa kumi mwaka jana walitangaza nia ya kutaka kugoma baada ya kuona wamemuamba awaongezee kimshahara kiduchu tu hakuwasikiliza hadi ilipofika muda wa kugoma mwaka huu tare 3/5/2010 ndio anatoa majibu ya kejeli ya maswali ya mwezi wa kumi. toka huo mwezi wa kumi mwaka jana ameenda kwa jirani zaidi ya mala kumi na kaongeza posho ya kaka zetu walioko mjengoni zaidi ya asilimia kumi , vilevile kanunua mgari ya kifahali V8 kwa idadi isiyohesabika kila wizara inayo zaidi ya kumi haya hayakuwepo wakati wewe upo na hata zile wizara ambazo wewe uliziweka 13 na baadae 18 na mawaziri wako hawakuzidi 20 yeye mawaziri wako 57 na wakianza kwenda mjengoni wanafunga wizara nzima wanaondoka wote.
Tunaomba mwongozo tufanya nini je tumnyime kura kama alivyosema kura zetu hazina UDHU! hata tukimnyima atashinda tu ? Yaani Baba ukituona utatushangaa! TUPE MWONGOZO.