Mwalimu Nyerere alipotangaza kukaa pembeni mwaka 1985 wengi walihuzunika. Yeye alidai anang'atuka. Kiuhalisia hali ya nchi kiuchumi na wakati vilimsukuma kando.
Siasa zake za ujamaa na kujitegemea za kunyang'anya watu mashamba na kuwarundika sehemu moja zilidhoofisha uchumi.
Utaifishaji wa mali za Watanzania wenye asili ya kiasia ambao hauna tofauti na kilichofanywa Uganda kuliondoa mtaji.
Nchi ilikwenda vitani kwa ahadi ya kurejea katika hali ya muda mfupi baada ya vita haikutokea.
Tukumbuke mwalimu Nyerere tayari alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 na nchi ilidorora zaidi. Kwahiyo wakati ulimsukuma Nyerere.
Una haki ya kutoa mawazo yako, Lakini baadhi yetu, na tunakuthibitishia kuwa tupo wengi, Mchango wa Nyerere kwa nchi hii haupimiki. He is the father of the nation. Nyere alileta umoja wa kitaifa, mtu unaweza ukaenda Tabora ukitokea Songea ukaishi bila matatizo. Alijenga taifa ambapo sasa tunajiita watanzania, aliweka misingi mizuri ya uchumi kwa kuleta viwanda vinavyoongozwa na watanzania wenyewe. Watoto wa maskini walisoma bure mpaka chuo kikuu. Mimi nilisoma wakati wa Nyerere na mzee wangu hakuwa na uwezo mkubwa. Nilisoma sekondari bure, nilisoma chuo kikuu bure... Kule Mlimani Enzi hizo tukienda cafeteria kulikuwa na mabomba ya maziwa..mtu unakunywa 'tani' yako. Nikiwa sekondari tulikuwa tunakwenda na sanduku tu na nguo zako. tulikuwa tunapata vitabu vyote bure pamoja na madaftari bure. Kulikuwa hakuna wizi wa vitabu kwani kila mtu ana vitabu husika. shuleni tulikuwa na swimming pool. tunaogelea na kujidai. Shuleni tulikuwa na vviwanja vitatu vya mpira wa miguu, kiwanja kikubwa cha riadha, viwanja vya netball, viwanja vya volleyball, hockey na kadhalika. Tulikuwa na indoor games nyingi tu. Wakati wa likizo tukiwa sekondari tulikuwa tunasafiri kwa kutumia travel warrants na tunapewa chakula cha njiani. Ajira ilikuwa nje nje, makampuni na mashirika mengi. Uzalendo ulikuwa mbele.
Maisha yalikuwa mazuri ila mambo yakaanza kuharibika baada ya vita vya Uganda vya Oktoba 1978...kwa hiyo debate ya Nyerere inaweza kuleta kuleta mjadala mzito kwa baadhi yenu na hasa wale wasioijua historia ya nchi hii. Hivi baadhi yenu mnafahamu kuwa before independence nchi hii ilikuwa na machifu wakitawala maeneo mbalimbali na katika makabila mbalimbali nchini mwetu? Hali hii ilifutwa after independence na nchi ikawa moja.
Kama watanzania tungekuwa makini na yale aliyoyapanga Nyerere nchi hii ingekuwa mbali mno. Vijiji vya ujamaa alivyoanzisha Nyerere vilikuwa na uzuri wake ingawa ni kweli utekelezaji wake ulikuwa na walakini. Ni katika vijiji vya ujamaa ambapo huduma muhimu kwa wananchi zilizogezwa kama elimu (shule), afya(dispensary), maji na kadhalika. Wakati wa Nyerere watu wengi wakiwemo wazee walijua kusoma na kuandika, hali ilifikia almost 90 per cent. lakini ni kweli kulikuwa na mabaya wakati wa ujamaa. Enterpreneurship ilitoweka, uvivu uliongezeka tukiamini kuwa kila kitu kitaletwa na serikali...hali ndio inayoendelea mpaka sasa ambapo watanzania tukiwa humu ndani ni wavivu tukitaka serikali ifanye kila kitu... Nidhamu nayo imetoweka.. mtu umejenga kwenye hifadhi ukibomolewa unataka serikali ikutafutie kiwanja...wabunge nao wakiwa bungeni kila mara wanalia ...'tunataka serikali ifanye hiki...'.
Mjadala wa Nyerere ni pana lakini kwangu mimi mazuri ya Nyerere ni 90% na mabaya ni 10%.