tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mchambuzi wa siasa na mwanasiasa mkongwe Said Miraj amesema Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameendelea kuwa mfano bora wa uongozi wa kizalendo usioendeshwa kwa tamaa ya mali binafsi.
Akizungumza kupitia kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa na Jambo TV na kuendeshwa na mtangazaji Wilbeforce Ngoto, Miraj amesema Nyerere aliiongoza Tanzania katika kipindi kigumu cha mpito kutoka ukoloni hadi taifa huru kwa kujenga msingi imara wa umoja, utu na uadilifu.
Soma pia: Wakenya wamjadili Nyerere na Magufuli kuangalia yupi aliweka identity ya Tanzania duniani. Wasema Nyerere ni tajiri baada ya kufa tofauti na Mobutu!
Amesema katika kipindi chote cha uongozi wake, Mwalimu aliweka mbele zaidi maslahi ya taifa badala ya maslahi binafsi, jambo ambalo limeendelea kumtofautisha na viongozi wengi wa vizazi vya sasa.
Kwa mujibu wa Miraj, kipaumbele kikubwa cha Nyerere kilikuwa ni kuhakikisha Watanzania wanakuwa wamoja, wamoja katika fikra, maono na lengo la kulijenga taifa jipya. Ameeleza kuwa huo ndio urithi mkubwa ambao Watanzania wanapaswa kuuenzi na kuutetea.
Amefafanua pia kuwa Mwalimu alikuwa na maono ya mbali kuhusu utunzaji wa rasilimali za nchi, akitolea mfano uamuzi wake wa kuchelewesha uchimbaji wa madini hadi pale taifa litakapokuwa na uwezo wa kunufaika ipasavyo. Miraj amesema maono hayo yameonyesha jinsi Nyerere alivyoona mbali zaidi ya kizazi chake.
Miraj ameongeza kuwa hata baada ya kustaafu, Mwalimu aliendelea kuwa kielelezo cha uadilifu na uzalendo. Amesema licha ya kuongoza nchi kwa zaidi ya miaka ishirini, hakuwahi kujilimbikizia mali.
“Mwalimu aliondoka akiwa hana majengo, magari wala mashamba. Alibaki kuwa mtumishi wa watu hadi mwisho wa maisha yake,” amesema Miraj.
Amesisitiza kuwa ingawa Nyerere hakuwa mkamilifu, mazuri yake yamezidi kwa mbali mapungufu yake binafsi.
“Kama tukipima kwa mizani ya haki, mazuri yake ni mengi kuliko makosa yake. Huo ndio urithi wa thamani wa Mwalimu Nyerere kwa taifa,” amesema Miraj.