Nyerere alimlaza Kenyatta baharini!

Nyerere alimlaza Kenyatta baharini!

Kwahiyo Kenyatta mwaka 1961 alikuwa Rais wa Kenya?

Kenya imepata lini Uhuru?

Tanzania Daima inafanikiwa sana kwenye kuwalaghaini!!!

Hivi wewe unasoma kabla ya kutoa comments?

Au kila kitu kwako ni siasa??!!

Nini kisichoelewaka kama sio kufanya makusudi??!!

Ni wazi mmepewa kibarua cha kufanya propaganda kusaidia CCM kwenye mitandao!

Hapa tatizo lako ni gazeti linalomilikiwa na kiongozi wa CHADEMA na sio habari katika gazeti husika!
 
Tanzania Daima kwa uongo, wamekubuhu.

Hamjui hata maana ya kufanya siasa!

Siasa hata pasipo na nafasi ya kufanya siasa!

Tatizo hapa si habari bali tatizo lenu ni mmiliki wa gazeti!

Aliewaajiri kufanya propaganda kwenye mitandao kwa faida ya CCM imekula kwake.

Namshauri awape mafunzo namna ya kuendesha propaganda kwenye mitandao
 
Hamjui hata maana ya kufanya siasa!

Siasa hata pasipo na nafasi ya kufanya siasa!

Tatizo hapa si habari bali tatizo lenu ni mmiliki wa gazeti!

Aliewaajiri kufanya propaganda kwenye mitandao kwa faida ya CCM imekula kwake.

Namshauri awape mafunzo namna ya kuendesha propaganda kwenye mitandao

Ukiona gazeti linaandika uongo ujuwe hata mmiliki ni muongo
 
Huyu mlinzi ametusaidia kujua kuwa kenyatta alikuwa mwanga. Ila hapo kwenye wajukuu kulia na kushoto kaniacha.
 
Kuna tatizo la uandishi au mleta thread ndo kabugi!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kuna tatizo la uandishi au mleta thread ndo kabugi!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Kwenye ukurasa wa pili wa hii thread kuna mdau ame-copy na ku-paste hii habari hivyo nenda katika huo ukurasa usome hii habari.Ukitaka kuelewa soma hilo gazeti ukurasa wa 14

Gazeti liko online.
 
dizaini kenyata alikuwa mganga wa kienyeji na singa yake
 
hata wewe umeshindwa kujua Mombasa kuna ikulu na ndipo alipomtoa mama Ngina
Mimi nafahamu kuwa Mombasa Ikulu ipo, tatizo langu ilikuwa kufahamu Kenyatta alilala bahari gani?
 
Tanzania Daima wameshindwa kufahamu kuwa Nairobi hakuna bahari.

Nawewe mtoto wa magogoni soma habari mpaka mwisho, mbona haikuandikwa kuwa ilikuwa ni nairobi, alie andika kasema ni hapa bongo. Pinga hoja kwa point.
1. Je ni kweli wakati huo jk alikuwa teyari ikulu?
2. Tunajua kuwa jomo alikuwa lupango mda mrefu, je wakati wa uhuru wa bongo alishakuwa huru.

Unajua mzee wa miaka 81 anaweza akasimulia aliyoota zamani akashindwa kufananisha na yaliyotokea kweli
 
Aliekuwa Raisi wa Kenya,hayati mzee Jommo Kenyatta alikuwa akilala baharini ili kumuombea Nyerere atawale Tanganyika.Maelezo hayo yametolewa na mzee Idd Nhende wa Sinza Dar-es-salaam katika mahojiano na gazeti la Tanzania Daima.

Mzee huyo amedai Mzee Kenyatta alikuwa akilala bahari siku tatu kabla ya kutangazwa kwa uhuru wa Tanganyika.Mzee Kenyatta alikuwa anaenda kulaka ufwekeni mbele ya Ikulu na walinzi wake huku wakiwa na soda na kuwaagiza walinzi wake wampige teke ikifika saa sita usiku ili amke na kujitosa baharini.

Kwa maelezo ya mzee huyo wa miaka 81 ni kuwa ilikuwa ikifika saa 2 usiku wote walikuwa wakiekekea ufukweni karibu na lango la Ikulu huku wakiwa wamebeba soda mikeka.Mzee huyo(mlinzi) ameeleza zaidi kuwa alietaka kunywa soda alikunywa na walikuwa wakilala kwenye mikeka hiyo na mzee Kenyatta alikuwa akilala katikati ambapo kulia na kushoto walilala wajukuu zake.Mzee huyu anasema Kenyatta alimwagiza kuwa ikifika saa 6 ampige teke kwenye unyayo ili amke.Baada ya kuamka wote huingia kwenye maji usawa wa magoti na mzee Kenyatta akawa anawamagia maji kwa kutumia usinga wake katika kumuombea Nyerere atawale vizuri Tanganyika.

UFAFANUZI:
Hii habari ni ndefu na katika ukurasa wa 14 haya yalifanyika hapa Tanzania na Kenyatta alikuwa mgeni wa Nyerere wakati huo mzee Kenyatta akiwa kiongozi wa KANU.Mzee Idd Nhende aliteuliwa na Nyerere kuwa mlinzi wa mzee Jomo Kenyatta alipokuwa hapa nchini.

Kwa maelezo zaidi soma gazeti husika online au subiri ununue gazeti hilo kesho.

CHANZO:TANZANIA DAIMA ONLINE

MY TAKE:
Hii habari ni ya ajabu sana na ngumu kuiamini!

Ukishakuwa marehemu kila mtu atakusemea. Watu waache uongo. Azeeke salama huyo mlinzi.
 
Hii stori na mm nilishawahi kuambiwa zamani kidogo, wakati huo kenya bado haijapata uhuru wake na mzee kenyata alikuwa na yy anaendesha harakati za kutaka kenya kupewa uhuru wake baada ya Tanzania,ila pia inasemekana kuwa kenyata alikuwa hataki kulala sehemu moja na wazungu ndio maana akaamua kuwa siku zile za kukaribia mkesha wa uhuru wa Tanganyika yy akaamua akalale ufukweni mwa bahari yuma ya ikulu ya magogoni.wakati huo wazungu wakiwa Ikulu wakienndelea kubiga kilaji, Ikumbukwe kwamba hapa kenyata bado hajakuwa rais na alikuwa hajakuwa na ulizi wa kutosha ndio maana Nyerere aliwateua baadhi ya hao wazee wampe ulizi mzee kenyata, na hata gari aliyokuja nayo kutoka kenya ilikuwa ni moja tu Land rover 109.
 
habari hii hapa na kwa kifupi Kenyatta alikuwa bado mwenyekiti wa KANU na aikulu inayoongelewa hapa nazani ni Magogoni
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=55070
WAKATI taifa likiadhimisha miaka 14 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, mmoja wa wateule wake amefichua siri kwamba kabla ya uhuru, Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta alilala baharini kumwombea aitawale Tanganyika.
Akizungumza na Tanzania Daima nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mzee Iddi Nhende alitoboa siri hiyo akisema kuwa ndiyo maana utawala wa Nyerere uliogopwa na watu wengi duniani.
Kwa mujibu wa mzee huyo wa miaka 81, siku tatu kabla ya kupandishwa kwa bendera ya uhuru wa Tanganyika, Kenyatta ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha African National Union (KANU), alikuwa akilala baharini mbele ya jengo la Ikulu.
"Ilikuwa ikifika saa mbili usiku watu wote tuliokuwa naye tunabeba mikeka na soda tunakwenda kulala ufukweni mbele ya jengo la Ikulu. Tulikuwa tunatandika mikeka yetu, anayetaka anakunywa soda na Kenyatta analala katikati… kushoto na kulia wanalala wale wajukuu zake wa kike.
"Hapo anauchapa usingizi hadi saa sita usiku, akawa ananiambia muda huo ukifika nimpige mateke kwenye unyayo ili kumuamsha… sio jambo rahisi kwa mlinzi kumpiga teke bosi wake, lakini Kenyatta alikuwa jeuri bwana (anasema kwa msisitizo na mshangao).
"Basi nikawa nafanya hivyo, akiamka tu anatuambia tukunje suruali zetu tuingie baharini kumwombea Nyerere ili atawale vizuri Tanganyika, tukawa tunaingia kwenye maji hadi usawa wa magoti, anachukua usinga wake na kuanza kutumwagia maji vichwani," alisema mzee Nhende.
Kuhusu utawala wa Nyerere, alisema watumishi wa serikali walifunzwa ujamaa, kupendana kwa dhati na kuheshimiana huku akisisitiza kwamba haikuwa rahisi kufanya hujuma kama ilivyo sasa.
Alisema hivi sasa wananchi wamechoshwa na rushwa iliyomea mizizi kwenye wizara, idara, taasisi na mashirika ya umma, na kubainisha kwamba wachache wanaopata nafasi wanazitumia vibaya bila kujali maslahi ya Watanzania wengine.
Mzee huyo anaiomba serikali kuwarejeshea heshima ya taifa watu wake na kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kupunguza pengo kati ya masikini na tajiri alilodai ndiyo chanzo cha maovu yanayoendelea sasa. (Kwa maelezo zaidi soma makala ya mzee huyo ukurasa wa 14)
Lembeli alipuka
Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), amesema kuwa Watanzania wanavuna walichopanda baada ya kumdhalilisha na hatimaye kuzika mema yote aliyowaachia Nyerere.
Lembeli alitoa kauli hiyo wakati akitoa maoni yake juu ya kumbukumbu ya miaka 14 baada ya kifo cha muasisi huyo, akisema kuwa Azimio la Arusha, miiko ya uongozi, misingi ya umoja vimezikwa na kuruhusu rushwa kutamalaki, ikiwa ni pamoja na kuifanya fedha kuwa kigezo katika kusaka uongozi.
"Nchi yetu sasa inakabiliwa na fujo, wizi, ujangili, Watanzania kubaguana kwa misingi ya dini, kabila na hata rangi, rasilimali za taifa kutoroshwa na kukithiri kwa ufukara. Tumeruhusu makundi yasiyo halali ya kibepari kujipenyeza ndani ya jamii, hivyo kuvuruga kabisa ustaarabu aliotuachia Nyerere," alisema.
Kwa mujibu wa Lembeli, wananchi wote pamoja na viongozi wanatakiwa kutubu mbele za Mungu kutokana na kuyazika mema aliyowaachia Nyerere.
 
Wakuu tusimlaumu muandishi wa habari na mleta thread bila kutafuta habari zaidi. Muda mfupi uliopita PIUS MSEKWA NA KINGUNGE wakiwa na bado wapo TBC wamegusia suala hilo hilo kwamba Kenyatta Sr. Alikuwa akikesha ndani ya maji BAHARINI akimuombea Nyerere! Hawajasema ni bahari ya wapi.Ila hakupenda kuungana na Nyerere kwenye baadhi ya mambo. Labda kuna ukweli.
 
Back
Top Bottom