Nyaulawa ameenda na magazeti yake mtandaoni

Nyaulawa ameenda na magazeti yake mtandaoni

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,441
Reaction score
166,938
Salaam,

Waswahili wanasema kazi ya Mungu haina makosa.. Hilo silibishii na wala sina pingamizi nalo...

Nyaulawa aliyekuwa mkurugenzi wa Business Times na pia mbunge wa Mbarali, alikuwa ni mtu wa watu na mpenda maendeleo kwa ujumla... Magazeti yake yote yalikuwa hewani kila siku kwenye tovuti..

Cha kusuikitisha ni kuwa baada ya kifo chake haukupita hata muda wa wiki mbili... Tovuti zote zikafungwa....

Je ni kweli uongozi mpya umeshindwa kuziendesha?

Je sisi kama wana jamii tuliokua tukinufaika na magazeti hayo tunaweza kufanya kitu gani ili yarudi hewani?
 
Unajua kwa nini wenzetu (kwa hapa Tz zungumzia Wahindi na Waarabu) wakiwa na biashara kama itatokea bahati mbaya akafariki bado biashara zao zinaendelea tena na kukua sana??? Wana utaratibu wa kuandaa successors!!!! Je sisi Wa tz ni wangapi tunakuwa na biashara hata tukashirikisha familia, hasa mke na watoto vizuri i.e kuanzia ujanja wote wa ku-deal na biashara??? Tunafanya mambo kwa siri, ukiaga dunia unazikwa na siri zako!!!!! Hata mafisadi RA, Manji, Zhakaria, Mzee Kijicho (Oilcom) na wengine wengi wamearithi biashara zao na zikakua na wataendelea kuandaa wa kuziendeleza.

Tujiulize, our late Nyaulawa alikuwa ameandaa successor?? Kama yupo basi kuna tatizo. Simkumfahamu sana huyu mzee ila ndo hivyo tena.
 
Nyaulawa alikuwa mbunge wa Mbeya vijijini na sio Mbarali!!
 
Back
Top Bottom