Nyaronyo Kicheere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyaronyo Kicheere

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Megawatt B, Jan 11, 2012.

 1. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wiki iliyopita kuna mwana JF mmoja alimponda sana mwandishi huyu (Nyaronyo Kicheere) ambae sasa anaandika makala zake kwenye gazeti la Mwana Halisi kila Jumatano. Nalikubaliana nae kwa kipengele kimoja tu, cha kuwa kila mtu ana utashi wa kutoa maoni yake. Lakini hoja zake sikuziuunga mkono pale aliposema mwandishi huyu ana hatarisha usalama wa nchi.

  Kwa mtazamo wangu mimi, mwandishi huyu kwa sasa ni kati ya waandishi ambao wapo wazi sana katika uandishi wao na unaona kabisa hana woga wowote katika makala zake. Nimekuwa nafuatilia makala zake kwa wiki kadhaa sasa na nimegundua ni makala ambazo zinagusa jamii walio wengi kwa sasa ambao wanahuzunika na ombwe la uongozi tulio nalo katika nchi yetu. Namfananisha mwandishi huyu na Johnson Mbwambo, Jenerali Ulimwengu na wengineo wengi ambao wako wazi katika kuelezea kile kinachomgusa na kinachowagusa wengine pia. Jaribu leo kufuatilia makala yake kwenye gazeti la Mwanahalisi la leo ( januari 11-17 )uone alivyoelezea Kisa cha matajiri na fukwe za kigamboni . sina nia ya ku promoti gazeti lakini wengi wetu hatuna uwezo wa kununua kila gazeti linalotoka kila siku/kila wiki na si rahisi kuweka hapa makala yote kuwachosha wasomaji. lakini amejaribu kuelezea jinsi gani walala hoi wanaonekana hawastahili kuishi kigamboni na jinsi matajiri wanavyotolea macho eneo hilo.
   
 2. MANI

  MANI Platinum Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Aliyoyasema ni ukweli mtupu subiri tu uatasikia anatafutiwakesi ya uchochezi!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nyarionyo mwenyewe ni mwanasheria, hivyo nadhani anakuwa makini sana anapoandika kuepuka uwezekano wa kushtakiwa
   
Loading...