Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Shukrani za kwanza zimuendee Nyani Ngabu The Don! kwa kuitikia wito wa mahojiano haya ambayo yatakuwa yanahusisha
vitu vingi sana
ikiwemo MAPENZI &MAHUSIANO, MARAFIKI, UTAJIRI&MALI, FURAHA, MAISHA YA UGENINI N.K.
Kiufupi leo tutamjua huyu nyani wa Ikungulyabashashi amefikaje fikaje USA baby...
-
Na kama kawa shoo itasimamiwa na mimi STUNTER pia usisahau kwamba mwisho nitatoa nafasi ya wengine kuuliza maswali yao kuhusu mada tajwa hapo juu,
Ninawaomba wote tuwe watulivu
na leo itabidi tuagize ndizi badala ya kuagiza popcorn...
N.B
Fuatilia kimya kimya mpaka mwisho utakaporuhusiwa kuuliza swali.
KARIBUNI.
USA baby...
-------------
UPDATE
----------
Unaruhusiwa kuuliza swali lako
 
I stay ready!

And if you stay ready you ain't gotta get ready.

So let's get right to it....
Ok,
Ngabu najua una marafiki wengi sana, na pengine wengi wangetamani wawe na urafiki na wewe, je ni vigezo gani ambavyo unaviangalia pindi upatapo rafiki mpya? Au ili mtu awe rafiki yako ni lazima awe na vigezo gani?
 
Huyu jamaa na mfaham vzr sanaaa ila yy hanijui, kuna siku tulikua kwenye bas nikaona ana log in JF ni mzee wa makamu muhun muhun tuu yaani wale wazee vijana ana mambo ya kisela sanaaa
Hahahahah utakuwa umemuwaza Ngabu hahahah.
 
Ok,
Ngabu najua una marafiki wengi sana, na pengine wengi wangetamani wawe na urafiki na wewe, je ni vigezo gani ambavyo unaviangalia pindi upatapo rafiki mpya? Au ili mtu awe rafiki yako ni lazima awe na vigezo gani?

Kwa manufaa ya umahsusi, unazungumzia urafiki upi hasa?

Urafiki wa kimtandao [mfano JF, WhatsApp, nk] au urafiki wa huku uraiani?
 
Kwa manufaa ya umahsusi, unazungumzia urafiki upi hasa?

Urafiki wa kimtandao [mfano JF, WhatsApp, nk] au urafiki wa huku uraiani?
marafiki wa mitaani na kama utapenda kugusia na marafiki wa mitandao pia itakua poa...(ulishawahi kupata marafiki mitandaoni? Ulitumia vigezo gani ili kukubali awe rafiki yako?)
 
Pia unahisi kipi bora kwako, kuwa na marafiki wengi au kuwa na wachache?

Kwangu bora ni kuwa na marafiki wachache lakini wenye ubora.

Kuwa na marafiki wengi ni kukaribisha kila aina ya matatizo tu kwenye maisha yako.

Hivyo binafsi napendelea kuwa na marafiki wachache walio ma ubora.

Wengine waliobaki ni washikaji [acquaintances].

Alafu hebu tuambie, marafiki walishawahi kuwa msaada kwako kwenye msala wowote ule? Nyani Ngabu

Hapana kwa kweli.

Hakuna rafiki hata mmoja ambaye amewahi kuwa msaada kwangu kwenye msala wowote ule.

Hiyo ni kwa sababu mimi ni mtu mwenye kupenda kujitegemea mwenyewe.

Pia nina uwezo mkubwa sana wa kuvumilia hali ngumu.

Uwezo huu ndo hunifanya nisitegemee misaada ya aina yoyote ile toka kwa watu.
 
Hongera sana!
natambua kwamba kwenye marafiki kunakuwa na jinsia mbili yaani ke na Me,
je, ulishawahi kuwa na rafiki wakike ambae baade akageuka na kuwa mpenzi? Je mlidumu kwa muda gani?
 
Huyu jamaa na mfaham vzr sanaaa ila yy hanijui, kuna siku tulikua kwenye bas nikaona ana log in JF ni mzee wa makamu muhun muhun tuu yaani wale wazee vijana ana mambo ya kisela sanaaa
Hahahaha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom