Nyani haoni kundule

Nyani haoni kundule

bahati mbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
578
Reaction score
193
Habari za majukumu wana JF.

Mwanaume baba yake alifariki akiwa na umri wa miaka 3, kwenye upasuaji ambapo alipoingia operation hakutoka na ndiyo ukawa mwisho wa maisha yake. Ukizingatia kuwa baada ya mzee huyo kufariki mama hakuolewa tena ila alizaa watoto 2 nje ya yule mme wake.

Hoja kubwa hapa ni kuwa mwanaume huyo alipofikia wakati wa kuoa miaka 11 iliyopita, alioa mke ambaye kalelewa na mama yaani Single parent.

Wanapokuwa na tofauti katika maisha yao ya kila siku baba anawaambia watoto kuwa mama yenu anataka kuwalea upande mmoja kama alivyolelewa yeye.

Swali linakuja je yeye akalelewa katika mazingira yapi?

Mchango wenu na ushauri unahitajika!!!!!!!!
 
mmmhhh, mambo ya ngoswe mwaachie ngoswe mwenyewe! wakae chini waongee wayamalize
 
Monkey anus.jpg

As a title above
 
Mhhh.......yale yale siku wakikosana na mke wake akimuambia anaenda kwa mama nayeye mwanaume anaacha watoto kwenda kwa mama yake!
 
Mpaka yanawekwa wazi ujue yamekuwa zigo, inatafutwa njia mbadala ya kuendle issue hii.
 
tatizo hapo sio mume kumdharau mwanamke, bali inaonekana mwanaume kajaribu kumfundisha/kumbadili mwanamke inashindika.

Unapokuwa ndani ya miaka kadhaa wewe na mkeo mnapishana kitu fulani, mwanaume hufika mahali na kuona kuwa hubadilishiki hata ikipigwa ngoma na hapo ndio huanza kufikiri mengine labda akijua ni asili ya mwanamke kufanya afanyavyo, na ndipo hufikiri labda ni malezi ya kwao au karithi wa wazazi wake maana labda kaona no way out kaongelea jambo moja mwaka wa 4 mtu habdaliki.

Hapo kikubwa ni mwanaume kuwa mvumilivu kwa mkewe na kufikiria njia mbadala za kumaliza kero. ndoa sio mchezo ina changamoto zake,ndoa ni kama muungano wa tanganyika na zanzibar kero ziko nzito sana lakni pia kuna waznz na wat/nyika wanaendelea kufaidi ingawa kero zipo.kikubwa uvumilivu.na kutochokana
 
Shida niionayo hapo ni wanaume wengi kudhani wao kila kitu wako sawa. Unapoingia kwenye ndoa unatakiwa kuyachukulia madhaifu ya mwenzio kwa njia ya ustaarabu na siyo matusi kwa familia nzima wakati na upande wa pili kunakuwa na madhaifu mengine tena kwa wakati mwingine yanakuwa makubwa kuliko hayo yanayoshikiwa bango.

Ndoa ni MSALABA.
 
Back
Top Bottom