madaili
Member
- Mar 6, 2014
- 32
- 27
Siku moja nikiwa safarini kikazi, baada ya mishughuliko ya hapa na pale mchana kutwa niliamua kwenda mtaani kupata moja moto moja baridi
Niliona itakuwa ni vizuri nikiagiza mishikaki ya mbuzi kutoka kwa mzee mmoja maarufu sana mtaani hapo kwa nyama choma ili kuendelea kusukuma vinywaji nilivyokuwa nagegeda...
Wakati ninasubiria mishikaki yangu ambayo mzee alikuwa anaitayarisha, niligundua kuwa pembeni kulikuwa na viumbe wawili wamejilaza kwenye majani...
Niliamua kusogea karibu nione ni viumbe gani na niliweza kugundua kuwa ni mbuzi ndama mmoja mweupe na pembeni yake alikuwa mbwa mweusi na madoadoa meupe.
Wote walikuwa wanaonekana wana majonzi na japo kulikuwa na majani lakini mbuzi huyo alikuwa hayali...
Kulikuwa na vipande vya nyama vilivyodondoka ama kutupiwa upande wao na mchoma nyama, pia na wateja wa kigenge hicho, lakini mbwa naye alikuwa havili.
Nilisogea kwa karibu zaidi ili nione kisa ni kwa nini wanyama hao wapo pamoja katika hali hiyo...
Niliweza kusikia sauti toka kwa mbwa na mbuzi hao wakiongea na mazungumzo yao yalikuwa kama hivi:
Mbwa "Unalia nini?"
Mbuzi "Hawa binadamu noma sana, unajua wamemuua baba yangu, halafu wanamchoma na kumla, ndio maana nipo hapa naomboleza"
Mbwa baada ya kusikia hivyo akamwambia "Rudi kwenu dogo kabla sijakupa makonzi kwenye pembe butu zako hizo, maana unanipa hasira, baba yako yupo salama salimini, mimi ndio wa kuomboleza kwa kuwa anayechomwa ni baba yangu, baada ya baba yako kukimbia. Mimi ndio napaswa kuomboleza hapa"
Sikupenda kula nyama hizo kwa hiyo nililamua kurudi zangu guest kimya kimya kulala nisubirie siku ya pili nirudi kwenye shughuli za kujenga taifa, wakati najitayarisha kulala nilisikia mtu anagonga hodi mlangoni, baada ya kufungua, mlangoni alikuwa ni bosi mchoma nyama akasema "Bosi ulipoondoka nilikuwekea nyama zako lakini hukurudi, mwisho niliuliza unaishi wapi ndio wakanielekeza, nikaja, huwezi kumiss hii nyama kwa kuwa kambwa kenyewe kalikuwa kadogo kadogo tuu"