Equitable
JF-Expert Member
- Dec 24, 2021
- 2,010
- 5,449
Napita hapa mnadani wilayani Maswa nakuta wanafunzi wamekaa sita wa kike wamekaa vibandani. Nawauliza kulikoni hamuendi shule? Wananijibu "jana tulipigwa na leo tusipopeleka hela ya waalimu tutapigwa".
Watoto wa kike wakubwa wamekosa elfu 2 ya kulipia walimu wanaojitolea.
Nimewaambie warudi nyumbani wamegoma na kwenda shule wamegoma. Sina mamlaka ningewachapa.
Sasa. Wazazi wa Maswa wamekosa elfu mbili kwa mwezi kulipa walimu wa kujitolea. Ni fedheha kwao na serikali.
Watoto hawa leo hawatasoma sababu ya wazazi aidha wakorofi au wabahiri au hawana kabisa.
Basi naomba
1. Serikali irudishe ada mashuleni ili shule zijiendeshe au
2. Halmashauri iweke bylaws ya kuwalazimisha wazazi kulipa
3. Wanafunzi wasiadhibiwe kwa kosa la mzazi. Mzazi ndio aadhibiwe.
Ni mimi mpita njia