Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

Cv yake tafadhali

Anamiliki kampuni ya utalii na vitalu vya uwindaji! Hapo mwanzo ilisemekana walikuwa hawakai zizi moja na bosi wake Kagasheki kwani walikuwa wakitoa lugha gongana kuhusu wizara yao! Ni mkali kwa totoz kwani jiko lake ni matunda ya uncle Lundenga! Ni miongoni mwa wanaotaka kukaa mahali patakatifu a.k.a Ikulu!
 
Awajibishwe lembeli kama unacho sema ww nyalandu ni cha kweli.ila kama lembeli alichosema ni kweli basi ww nyalandu uwajibike kwa kusema uongo.
 
huyu nyalandu kwani akwepo bungeni mpaka hayaseme hayo nje ya bunge kwani yeye awajui wanao wauwa tembo mbona pembe zilikamatwa zanzibar kesi aijaenda mahakamani na wachina wanaokamatwa awaruswa kuwataja aliyewapa huu ni usani wa serekali hivyo nyalandu asijifanye anapotosha watu wakati anajua kila kitu
 

Nyalandu Mimi simuelewagi kwakweli....,kwa nini hakusimama kumtetea waziri wake? Na Badala ya kumtetea akanza kampeni Za kuupata uwaziri Kamiki.....Sasa news in circle zinaposema kuwa uwaziri wa utalii anapewa..Lembeli Ndio Anaanzisha kampeni dhidi yake? Tumueleweje...
 
Last edited by a moderator:

Alikuwa pia hapatani na waziri wake alipokuwa wizara ya viwanda...he has always wanted to be a full minister...na hata akiupata labda asiwe na Naibu ..ni one man show type
 
Wakati inasomwa hiyo ripori Nyalandu hakuwepo Bungeni?
Mbona hakunyanyuka kuyasema hayo?
watu wengine ni wanafki.!!!

ana mfariji kagasheki kwamba , eee bwana!!!! zile dili zako mimi nitaendeleza tu mzee usihofu tupo pamoja . sabuni haisafishiki . eti hawa ndiyo wasomi . naamini sasa aliyoandika mmbwambo katika raia mwema iliyopita , hata baraza la mawaziri lipanguliwe hakuna jipya madam ni chama kile kile.
 
Kwa watu makini hii kauli ya Nyalandu ni unafiki uliopitiliza.Hivi huyu Nyalandu alikuwa wapi wakti Kamati ya Lembeli ikifanya uchunguzi hadi kuwasilisha ripoti yake Bungeni?
'
Nyalandu alikuwa wapi wakti watu wakiteswa,kupigwa,kubakwa,kuporwa mali zao na wengine kuuawa?Alikuwa wapi huyu kibuyu?Hivi kuna haki gani ya kumwajibisha Waziri peke yake na kumwacha Naibu wake kwenye Wizara iliyokumbwa na kashfa
???Nyalandu anatakiwa amfuate Kagasheki kwa kujiuzulu au Rais atengue Unaibu wake!
 

Naona anataka kutumia fursa ya unaibu aonekane anachapa kazi kumbe nguvu ya soda, Yeye anashutumiwa pia kumiliki vitalu vya uwindaji wakati ni naibu waziri hapo tayari kuna mgongano wa maslahi. Nadhani naye aondoke tu
 
Nyalandu alishaunda tume yake ambayo imebaini uongo wa ripoti ya tume ya bunge? Tume ya Rais haijaanza kazi huo uongo umebainika vipi? Ukiona kauli za namna hii zinaanza kutolewa jua kuwa mkakati wa kuficha ukweli na kuharibu ushahidi uko kazini. Usishangae wale waliobakwa pamoja na jamaa zao ama wakapewa fedha wakane ukweli au wakatoweka katika mazingira ya kutatanisha!Yaana wanahangaikia sifa ya nchi kwenye macho ya ulimwengu na sio kuhangaikia haki na usalama wa raia. Eti sifa ya nchi imeshuka kiutawala bora, kwani imeshuka leo? Tumuize Dr Ulimboka.
 
Mwandishi wa habari hii hakutimiza kazi yake vizuri. Labda alikuwa na maslahi binafsi na Nyalandu. Nilitegemea baada ya kusikia toka kwa Nyalandu angewasiliana na uongozi wa bunge au Lembeli mwenyewe ili kupata maelezo yake.

Jina la gazeti lenyewe sasa! "Chagadema Daima"
 
Yaani Kusema Ukweli Katika Mawaziri Na Manaibu Waziri Nyalandu Huwa Ni Mkweli Sana. Jamaa Atakuwa Sahihi Ila Tatizo Ni Heading Ilivyokuja.
 
Naona huyu jamaa ana kichwa cha panzi. Alishindwa kuyasema bungeni hadi watu wanawajibika. Kwanini aseme leo kuwa ulikuwa ni uongo? S
 
Hivi majuzi Naibu Waziri wizara ya Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili iliyowang’oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo. Nyalandu anadaiwa kutoa kauli hiyo alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma na Manyara kuhusu mgogoro wa mipaka kati wanavijiji na Hifadhi ya Tarangire.





Nyalandu alikaririwa akisema kutokana na taarifa hiyo kueleza wapo watu waliobakwa wakati siyo kweli. Tanzania imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora kutokana na ukiukwaji haki za binadamu.

Kutokana na kauli hii ni wazi kuwa Nyalandu amemdhalilisha mheshimiwa Rais wa Jamhuri na anapaswa kumuomba radhi haraka sana na ikiwa ni pamoja na kufuta kauli yake kwa Umma. Nyalandu anataka kuuambia Umma kuwa mheshimiwa Rais alikurupuka kufanya maamuzi ya kuwatimua mawaziri wanne waliotuhumiwa katika ripoti hiyo.

Ikumbukwe ni Nyalandu huyuhuyu ndiye aliyesababisha Waziri wake Omari Nundu kuvuliwa Uwaziri yeye alipokuwa Naibu wake wizara ya Viwanda. Ni hatari sana kuwa na watu aina ya Nyalandu wanaotaka madaraka kwa kuwaharibia maboss wao ili wao waonekana wazuri.
 
Hili suala linapaswa kuchukuliwa kwa umakini sana. Ukweli ni kwamba watanzania tunasifa ya kusema uongo na si kwa nyalandu pekee. Vipi kuhusu zile cd za Mbowe kuhusu bomu la Soweto?
 
Hili suala linapaswa kuchukuliwa kwa umakini sana. Ukweli ni kwamba watanzania tunasifa ya kusema uongo na si kwa nyalandu pekee. Vipi kuhusu zile cd za Mbowe kuhusu bomu la Soweto?
Mbowe anaingiaje hapa wewe mama?
 
Hili suala linapaswa kuchukuliwa kwa umakini sana. Ukweli ni kwamba watanzania tunasifa ya kusema uongo na si kwa nyalandu pekee. Vipi kuhusu zile cd za Mbowe kuhusu bomu la Soweto?

Ungekuwa wa kike, mbowe angeshakuchumbia, watu wanajadili hili wewe unakuja na mbowe... shame
 
Kabla ya kuendeleaa na hii mada hebu tuambie ni lini Omary Nundu aliwahi kuwa Waziri waa viwanda na biashara???????
 
Halafu alituambia eti wamarekani wanampendekeza awe Rais ajae wa Jamuhuri. Sijui ni wabebabox wa wapi hao walimpamba hlvyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…