MwanaPekee
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 382
- 385
mtachonga na kuweweseka sana, unadhani wana njaa kama wewe, unasema lowasa kafa kisiasa, akiibuka tu hapo hapo mshamuita kwenda kumhojiLazaro Nyalandu naye inaonekana amefanya kosa linalofanana kabisa na kosa lililofanywa na akina Lowassa na Lembeli. Ni kosa la kudhani kwamba unapendwa sana na unamashabiki wengi ambao wataambatana na wewe popote utakapokuwa. Ni kosa la kuona kwa “hakuna mtu mwingine” zaidi yako atakayeweza kufanya kile ulichokuwa ukikifanya katika ubora uleule au hata zaidi yako. Ni kosa la “miscalculation” na kuwa “overoptimistic” juu yako mwenyewe.
Kilichowapata Lowassa na Lembeli sote tunajua. Sasa wamepotea kabisa katika uringo wa siasa, hakuna anayewataja tena. Watu waliodhani kwamba wangewafuata kule waliko, waliamua kubaki ndani ya hema la CCM ambako waliona ni salama zaidi ya kwenda wasikokujua. Hakika lilikuwa ni kosa kubwa la kujivika “Umungu Mtu” lililopelekea kufa kabisa kisiasa.
Cha ajabu sana tena sana, Lazaro naye amecheza mchezo huo kwa namna ile ile ulivyochezwa na L&L. Mwalimu Nyerere alipata kusema, kuna wakati mtu unajiita au kuitwa vile unavyojiita au kuitwa kwa sababu ya mfumo uliopo ndani yake; nje ya huo mfumo si wewe tena; akitumia maneno “Nje ya Muungano hakuna Mzanzibari ila kuna Muunguja na Mpemba”. Hawa 3L’s wameshindwa kuliona hilo kabisa, kwamba wanatazamwa vile walivyo wakiwa ndani ya mfumo uliowajenga, nje ya hapo they are not the same. Zaidi ya hapo Lazaro alishindwa kukumbuka kwamba, yeye katika uringo wa siasa aliibuka tu kama uyoga, hakuwa na background strong sana kama akina Lowassa ambao pia wamepotezwa, lakini bado akashupaa shingo na kudanganyika kwamba ataendelea kuwa on top hata ndani ya mfumo mpya. Goodbye forever Lazaro, tutai-miss sana sauti yako Bungeni.
Sijawai kuona uhai wa Lazaro (kisiasa).
J.L anakula maisha tu kama upo arusha pita mitaa ya Haile Sellasie apo wanapochora choraLembeli Siku Hizi ni Dj aisee haya maisha
Duh..kwa hiyo kutoka kwenda kukaa na kina fazal wa leopard tours mpaka vijiwe vya kuchorachora..ila huyu Mzee kilimuondoa fitina za kipindi kile cha kina lowasa ambapo nguvu ya fedha ndio ilikuwa inaamua..ila Bado wanamuhitaji muda na saa yoyote..hata kwenye msiba wa Mzee sitta alionekana amezungukwa na wana ccm..huyu sitashangaa hata kesho akirudi ccm..maana mfumo alioukimbia wa nguvu ya fedha unamalizwa kabisa ndani ya ccmJ.L anakula maisha tu kama upo arusha pita mitaa ya Haile Sellasie apo wanapochora chora
Mkuu punguza hasira kunywa Maji kwanza
Very true...... lakini tetesi zinasema alikuwa hana mpango wa kuendelea na siasa na ilikuwa 2020 aachane nayo kabisa afanye yake kwa pesa zetu za vitalu alivyouza lakini yote haya anafanya kwa shingo upande baada ya kuona upepo haupungii kwake tena KWISHA HABARI YAKE.
Ila mtoa uzi inaonyeha wazi unajua kushawishi sababu huu ni uzi wa pili kwa leo ukionyesha wazi upo upande fulani.
Hongera!
mtachonga na kuweweseka sana, unadhani wana njaa kama wewe, unasema lowasa kafa kisiasa, akiibuka tu hapo hapo mshamuita kwenda kumhoji
Kwani Akifa kisiasa wewe kinachokuuma nini, anakula kwako au Maisha yake utayaendesha wewe?? Ulitaka aendelee kubaki Ccm .rudi darasani
Kwani huko CCM ni mwanasiasa gani aliye hai na active ?! Ukiondoa bashite na mjombaake ! Ni bora kutoka ukawa huru kimawazo, badala ya kushangilia hata nonsense kwa kusubiri cheoSina uzi wowote nilioutoa leo, labda unilishe wewe maneno
Kuna ukweli kabisa ufisadi na ujanja ujanja wa nyalandu uko wazi kabisa wala haiihitaji PhD kujua anachokifanya sasa ni kutafuta symphathy tu ya watanzania refer issue ya Lucky Vicent hahhahhahhah binadamu bwanaKwa hiyo waliosema kwamba amehama ili kutafuta sababu za kutoa pindi atakapofikishwa mahakamani wamesema ukweli. Duh, hii hatari sasa
Kwenye matumizi ya ID upo vizuri.Sina uzi wowote nilioutoa leo, labda unilishe wewe maneno