.....ndio maana kuna taarifa zinasema Ripoti ya tume ya Lembeli ina mapungufu....kwani imeangalia zaidi upande mmoja tu.......iundwe tume huru kabisa na watu wote wahojiwe......hizi tume zingine za Bunge zimekaa "kimagumashi"......
Mpaka leo sijui ni nani na katika mazingira gani bunge lilipewa nguvu za kisheria kuunda tume za uchunguzi. Kuna vyombo vya serikali kwa ajili ya kazi hiyo. Wabunge hawana taaluma ya kuchunguza. Mbaya zaidi wanachunguza wao na kutoa hukumu wao.
Nafikiri ingekuwa vyema wakaachia vyombo vya uchunguzi kufanya hivyo na wao wakapelekewa report na kuijadili.
Uzoefu wangu na hizi tume unaonyesha kuwa zinakuwa na mlengo wa kisiasa kwa ajili ya kuwakomoa watu fulani. Bahati mbaya zaidi watuhumiwa hawapewi nafasi ya kusikilizwa.
Kwa mfano ingekuwa busara report za namna hiyo zinaposomwa mawaziri husika wanapewa nafasi ya kuwasilisha hoja zao kabla ya wabunge kuanza kujadili. Hii ingetoa nafasi kwa wabunge kusikiliza pande zote kabla ya kuanza kutoa michango yao.
Kuwapa nafasi mawaziri mwishoni wakati mijadala imesha kamilika siyo haki kabisa.
Na kama hali hii itaendelea basi tutakuwa tunashuhudia mawaziri wakiondoka kila kikao cha bunge.
Ingawa watu wengi hufurahia kung'oka kwa mawaziri lakini kimsingi faida inayopatikana ni ndogo sana kulinganisha na hasara. Waziri huitaji kati ya miezi 6 hadi mwaka ili kujifunza mambo ya wizara husika na kutengeneza mpango mkakati wa kutatua changamoto mbalimbali. Sasa hapa kwetu mawaziri wanapofika hatua ya kuelewa na kuanza mikakati wanaondolewa na kuletwa wengine ambao na wanahitaji muda kujifunza. Hivyo ndani ya miaka mitano unakuta hakuna la maana lililofanyika.
Pili binadamu wote tunajifunza kutokana na makisa. Mtu aliyekosea ana nafasi nzuri zaidi ya kutenda bora zaidi kwani amekuwa anajifunza. Hivyo si busara kumuondoa mtu pale anapokosea.
Hali hii ndo husababisha watu kutenda na kufanya kazi kwa business as usual. Kwani anaogopa kama akileta ubunifu flani na usipozaa matunda chanya ataondolewa bila kupewa nafasi ya kurekebisha makosa.
Hivyo tutaendelea na mambo yale yale kila siku. Hakuna atakayekuwa tayari ku risk kitumbua chake kwa kujaribu kitu kipya kwa kuogopa kukosea.