Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,583
- 6,633
Kwa wakazi wa Musoma mkoani Mara jina la MAUZA si geni.
Ni jina kubwa mjini hapa lakini zaidi kuna wanaomjua kwa undani.
Jamaa huyu anamiliki Mgodi katika Halmashauri ya Musoma Vijijini, Wilaya ya Butiama kijiji cha Kataryo, ambao aliujenga kwa ushirikiano na nchi ya Canada, mgodi huo unaitwa CATA Mining (CATA - Canada-Tanzania).
Mauza aliujenga mgodi huu kwa Shilingi Bilioni 108 ambapo kati ya hizo, Dollar Milioni 34 ni mkopo kutoka CRDB na Dollar Milioni 20 ni kutoka TIB.
Bwana huyu, inadaiwa ndiye mwenye kampuni ya Mabasi ya Musoma Bus; ndiye mwenye kampuni ya ujenzi ya Spencon na pia anadaiwa kuwa mmoja wa wafadhili wakubwa wa CCM Mkoani Mara.
Sasa, safari ya Rais Magufuli mkoani Mara (inayoendelea) imekuja kummulika jamaa huyu kama mmoja wa wapigaji wa siku nyingi waliokuwa wakibebwa na “mfumo”.
Wenye data za bwana huyu hebu tiririkeni