Nyakirang'anyi Mauza: Ni tapeli kama inavyodhaniwa?

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Kwa wakazi wa Musoma mkoani Mara jina la MAUZA si geni.

Ni jina kubwa mjini hapa lakini zaidi kuna wanaomjua kwa undani.

Jamaa huyu anamiliki Mgodi katika Halmashauri ya Musoma Vijijini, Wilaya ya Butiama kijiji cha Kataryo, ambao aliujenga kwa ushirikiano na nchi ya Canada, mgodi huo unaitwa CATA Mining (CATA - Canada-Tanzania).

Mauza aliujenga mgodi huu kwa Shilingi Bilioni 108 ambapo kati ya hizo, Dollar Milioni 34 ni mkopo kutoka CRDB na Dollar Milioni 20 ni kutoka TIB.

Bwana huyu, inadaiwa ndiye mwenye kampuni ya Mabasi ya Musoma Bus; ndiye mwenye kampuni ya ujenzi ya Spencon na pia anadaiwa kuwa mmoja wa wafadhili wakubwa wa CCM Mkoani Mara.

Sasa, safari ya Rais Magufuli mkoani Mara (inayoendelea) imekuja kummulika jamaa huyu kama mmoja wa wapigaji wa siku nyingi waliokuwa wakibebwa na “mfumo”.

Wenye data za bwana huyu hebu tiririkeni
 
Kama umefuatilia ziara ya Mhe. Rais huko Mkoa Mara alianza na ufisadi wa Maji Pale Bunda Bil. 9, akaja na Ufisadi wa kuchoma Musoma Hotel ambayo inadaiwa kodi ya Miaka kumi vyote hivyo mdaiwa ni mmoja Bw. NYAKIRANG'ANYI.

Pole sana Mzee hiyo ndio awamu ya tano. Naona giza kwenye kazi zako nzuri za Musoma Express, Nyakirang'anyi Construction, Mining nk. Mzee alikuwa untouchable lkn jiwe keshamuweka kapuni daaaah
 
Ongeza nyama kidogo, binafsi bado sijakuelewa. Hebu mdadavue!!
 
Ongeza nyama kidogo, binafsi bado sijakuelewa. Hebu mdadavue!!
Mkuuu huyo mzeee ndiye alipewa mradi wa serikali wa maji pale Bunda Bil.9 maji hakuna, kule Musoma alibinafsishiwa na serikali Musoma Hotel kitu Nyota 5 alichofanya akapiga kiberti alipwe na bima lkn bima wakastuka. JPM alivyofika Mkoani Mara juzi akazinyaka ndipo akamlipua awekwe ndani fasta. Lkn nje ya kashfa hizo mzee pia ni mjasiliamali pia nilivoeleza.
 
Kama zacharia mi sitaki hata kumsikia, gari zake zilikuwa hazikamatwi zinakimbia zinaweza kushindana na risasi kwa speed. Yaan 3hours mwanza trm safari ya kama moro to dom, trafiki akikamata anapigiwa simu na IGP ama RPC utaanzaje kuikamata gari next time
 
Back
Top Bottom